Na Godfrey Ismaely
BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepata pigo kubwa mara baada ya kumpoteza Mbunge wa Baraza la Wawakilishi kupitia Jimbo la Uzini, Bw. Mussa Khamisi (CCM) na
mkewe Bi. Mwanaheri Twalib vifo vilivyotokea kwa nyakati tofauti mara baada ya kupata ajali juzi mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewana afisa Habari wa Tasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)Bw.Almas Juma Mbunge huyo alifariki jana majira ya saa nane usiku kutokana namshutuko alioupata juu ya taarifa za kufariki kwa mkewe.
Marehemu alipata nafuu kidogo na hivyo kupewa taarifa ya kifo cha mkewe lakini mara baada ya kupata taarifa hiyo alizidiwa na kupoteza maisha.
Akitoa taarifa juu ya kifo hicho jana Bungeni mjini Dodoma, Bi. Makinda alisema juzi asubuhi alitoa taarifa juu ya kutokea kwa ajali hiyo ambayo iliwahusisha mbunge huyo, dereva wake Bw.Chizani Sembonga pamoja na mkewe wakati wakitokea Zanzibar katika mazishi ya kaka wa Mkewe Bi. Mwanaheri, ajali iliyotokea katika eneo la Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Bi. Makinda alisema, jana asubuhi kabla ya kuanza shughuli za bunge aliweza kuwasiliana na mbunge huyo akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kitengo cha Mifupa na kumueleza kwamba anaendelea vizuri.
Bi. Makinda alisema kutokana na pigo hilo kwa bunge kikanuni, bunge limempa mamlaka ya kuahirisha shughuli zote za bunge pindi mbunge anapofariki dunia wakati shughuli za bunge zikiendelea.
Kwa mujibu wa taarifa za awali juzi, Bw.Silima alitokea Zanzibar kupitia Dar es Salaam wakiwa pamoja na mkewe na dereva ambapo walikuwa wanawahi katika kikao cha Bunge huku mkewe akiwahi katika kikao cha Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho kilipaswa kufanyika juzi mjini Dodoma.
Juzi mara baada ya Bi. Makinda kutoa taarifa za kifo hicho cha mke wa mbunge Bi. Mwanaheri wabunge wote walisimama kwa muda wa dakika kadhaa kwa ajili ya kumuombea dua marehemu pamoja na mheshimiwa Silima (marehemu kwa sasa) ili Mungu aweze kumpa nguvu apone haraka akiwamo dereva wake kwa ajili ya kurejea katika shughuli za ujenzi wa taifa.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Zelothe Stephen alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 2:15, kwa kuyahusisha magari matatu likiwamo la mbunge huyo lenye namba za usajili T509 AJC aina ya Toyota Corrola , ambapo dereva huyo wa mbunge akitokea Morogoro kwenda Dodoma alikuwa katika mwendo kasi hivyo wakati akitaka kulipita lori ambalo lilikuwa mbele yake alishindwa kudhibiti mwendo na kugonga katika tairi la nyuma na kupoteza mwelekeo.
INNALLILLAH WAINA ILLAIH RAJIUN,tunawaombea makaz mema ya huko akhera marehemu woote,hakika hakuna atayebaki ktk dunia hii,wote sisi ni wasafiri,issue ni nani anatangulia kuondoka,ni msiba mzito,lakin tunasema yote ni mipango ya ALLAH (SW).
ReplyDelete