Na Mwandishi Wetu, Tabora
WAKAZI 773 wa Kijiji cha Shela katika Kata ya Usinge Tarafa ya Kaliua mkoani Tabora hawana mahali pa kuishi baada ya nyumba zao 317 kudaiwa kuchomwa moto na
askari wa wanyamapori wakishirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Tabora wakidai zimejengwa katika hifadhi.
Tukio la kuchomwa moto nyumba hizo lilitokea Agosti 15 mwaka huu majira ya saa tano asubuhi baada ya askari hao kufika katika kijiji hicho wakiwa na silaha za moto.
Madai ya kujenga nyumba katika hifadhi hizo yamepingwa na wananchi wa kijiji hicho wakidai kijiji chao ni halali na kinatambuliwa na serikali na kwamba hatua hiyo imechukuliwa kisiasa.
Kutokana na tukio hilo wakazi hao wanaishi chini ya miti wakiwa hawana chakula na mahitaji muhimu ya kibinadamu na wanaoteseka zaidi ni watoto, wazee na akina mama wakiwamo wajawazito ambao maisha yao yapo hatarini kutokana na eneo hilo kuwa na wanyama wakali wakiwamo simba.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Abeid Mwinyi Mussa, akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu jana amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema oparesheni hiyo ilifanywa na Kamati ya Ulinzi na Usalaama ingawa hakufafanuua kama ni ya Wilaya ya Urambo lilipofanyika tukio hilo au ya Mkoa wa Tabora.
Wananchi hao walidai wakati wa zoezi hilo askari hao walikuwa wakipora magodoro na fedha na mifugo huku wakiwatishia kuwaua wale ambao wangeleta upinzani kwao jambo lililowafanya wengi wao kuacha miji yao na kukimbilia milimabni na vichakani kujificha.
Madai ya askari polisi kuchoma moto nyumba hizo na kupora mali za wananchi yamepingwa vikali na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ACP Anthony Ruta akisema hakukuwa na tukio hilo na nyumba zilizochomwa moto vilikuwa ni vijibanda vichache.
Mkazi wa kijiji hicho, Abdallah Mchanjamo alisema yeye alishiriki kuweka mipaka inayotenganisha eneo la kijiji na hifadhi hiyo kwa kushirikana na maofisa ardhi wa mkoa na kuchora ramani ambayo ipo mkoani na wao wanayo lakini anashangaa leo hii wanapoambiwa kijiji hicho kipo ndani ya hifadhi.
Mama mjamzito Peres Bulegea (32), alisema hajui hatima ya maisha yake na watoto wake watano na huyo aliyopo tumboni na wala mahali atakapojifungulia baada ya nyumba yake kuteketezwa kwa moto.
Mume wa Bulegea Bahati Hussein alisema siku ya tukio akiwa nyumbani kwake aliwaona askari hao waliokuwa na silaha wakifika nyumbani kwake wakiwa na magari mawili walikuwa zaidi ya 20 ambapo walianza kuchoma moto nyumba yake na vitu vyote vilivyo kuwemo kikiwemo chakula mabati zaidi ya 60 viliteketea ambapo yeye na familia yake walijificha mlimani wakishuhudia tukio hilo.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mgusa Maduhu amesema wananchi 773 hawana mahali pa kuishi na kaya 317 zimeteketezwa kwa moto na askari hao.
“Kwa ujumla sisi wote hapa kijijini hatuna maisha kwani hatuna chakula, mavazi na nyumba za kuishi kwani hata nyumba yangu iliteketezwa kwa moto na askari hao,’’ alisema Maduhu.
Alisema waathirika wa tukio hilo wanaishi nje katika eneo la Kariakoo kijijini hapo na hawajui hatma ya maisha yao na wanaoteseka zaidi na watoto na mama zao. Alisema watoto zaidi 200 wapo nyumbani hawaendi shule kwa sababu ya mgogoro huo ambao umeibuka kutoakana na masuala ya kisiasa.
Mwenyekiti huyo alisema kwamba kijiji hicho kilianzishwa mwaka 1974 na kupewa namba TB/KJ/359 Shela na mipaka iliwekwa rasmi mwaka 2002 na kina wakazi 7,350 na wanashangaa leo hii wanapo ambiwa walivamia na kujenga kwenye hifadhi.
Jamani utu umeisha, sasa hao watu wataishije?kwa nini wasingewapa muda wahame kuliko kuwachomea nyumba zao!nimeumia sana.
ReplyDeleteNawahurumia sana hao wenzetu, Hivi nyie Mapolisi mliochoma nyumba za wananchi hamna huruma? sio akili zenu hizo ila ni "unga" mnaokula, ngojeni wanyongwe wanaowaletea labda mtaacha kuwasalti wananchi.
ReplyDeleteNi kosa kubwa sana kumdhalilisha Mtanzania halisi kwenye nchi na ardhi yake japo ardhi ni mali ya Taifa. Ni aibu sana kunyanyasa watu kwenye nchi yao bila huruma.
ReplyDeleteInauma sana kuona haki isivyo tendwa,au tuseme ukweli ya kwamba nchi hii inawapenda watu kipindi cha kupigiwa kura tu?? Mtoto wa mtu, mjuu, mzee, babu na bibi, baba na mama, wagonjwa na walemavu wanalala nje ya vijumba vyao vya nyasi usiku na mchana na kuogopa simba na hatari nyinginezo, kama wakimbizi kisa kuwachomea vibanda!! Hao wakubwa mbona wengi wametoka kwa wazazi wao waliokuwa na vijumba aina ya vibanda? Wamesoma bure nchi hii sasa wanasahau walikotoka? Mungu awalaani wote walio shiriki na kuhakiki zoezi hili zima tangu lilipo kuwa linaundwa ili lifanyike. Walaaniwe na Mungu wao na vizazi vyao milele. Mapolisi Tanzania tunajua mnabwia unga na kuvuta Bangi, punguzeni, tumechoka kusikia visa vyenu, magwanda mnayo vaa ni kodi zetu ndogo ndogo sisi mnao tunyanyasa kila kukicha.Shame on you fools.
Hivi kungetokea maafa ya raia kufa katika hilo tukio polisi wangesemaje?Saidi mwema mambo mengine wanayofanya polisi yanavuka mipaka na sijui hao polisi wako wamesoma shule gani.Wamezoe kufanya kazi kama maroboti maana ukishaliswichi tu lenyewe linaanza kufanya kazi.
ReplyDeleteWatanzania wenzangu hebu kwanza tujiulize! Hawa Polisi wa Tanzania walogwa? Nadhani siyo bure.
ReplyDeleteKama wanajua kufanya vituko kwa raia wenzao kwanini wasiende huko Libya?
Watanzania tumechoka na tutakapofanya maamuzi tutaunda Jeshi letu na tutapata Wasamaria wa kutupa silaha tufanye mabadiliko katika Serikali hii ya Kiwete ambayo haimtambui Mtanzania.
Wakati wa uchaguzi kinachotuponza ni Sh.10,000/= kila baada ya miaka mitano.
Tubadilike jamaaaaaaaaaaaaaaani!!!!!!!
Mtanzania mwenye uchungu!