15 August 2011

Mawaziri wanne Kenya wakalia kuti kavu

NAIROBI,Kenya

WAZIRI wa Elimu ya Juu,Bw.William Ruto huenda akatupwa nje ya Baraza la mawaziri wakati Waziri Mkuu, Bw.Raila Odinga atakapowaadhibu waasi ndani ya
chama cha  ODM katika mabadiliko ya baraza hilo ambayo yatafanyika baadaye wiki hii.

Habari kutoka jijini Nairobi zilieleza jana kuwa, mbali na waziri huyo,pia fagio hilo huenda likawakumba Waziri wa Viwanda,Bw. Henry Kosgey,Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,Profesa Hellen Sambili na Naibu Waziri wa Mifugo,Bw. Aden Duale wakati Bw. Odinga atakapoamua kuondoa uasi wa kisiasa kwa upande wake ndani ya serikali ya muungano.

Vyanzo vya habari vya kuaminika ndani ya  ODM vilieleza kuwa Waziri Mkuu huyo amelazimika kutumia mamlaka aliyopewa kikatiba ya kuteua Mwanasheria Mkuu na mawaziri wengine ili kuondoa wabunge waasi wanaotumikia baraza la mawaziri.

“Endapo itakwenda kama ilivyopanga,hatua  hiyo itachukuliwa wiki ijayo(wiki hii), Itakuwa ni kwa ajili ya kuwaondoa  waasi na wale wenye kesi mahakamani.Viongozi wa ngazi ya juu wameshatoa maagizo, "alisema mmoja wa washauri wa Waziri Mkuu ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa akile alichosema itakuwa ni sawa na kutoa taarifa kabla ya  bosi wake.


Alisema, mabadiliko hayo yatakwenda sambamba na uteuzi wa Mwanasheria Mkuu ambaye atachukua wadhifa wa kiiongozi aliyetumikia wadhifa huo kwa muda mrefu,Bw. Amos Wako ifikapo Agosti 27 mwaka huu.

"Inaonekana kukubalika wiki ijayo ili kutoa muda kwa ajili uteuzi wa Mwanasheria Mkuu mpya na baadaye aidhinishwe na Bunge kabla ya Wako kumkabidhi ofisi. Kuna maeneo mengine ambayo yanapaswa kuangaliwa na hatua hiyo itafikiwa baada ya wakuu kushauriana, "chanzo cha kuaminika ndani ya  Ofisi ya Rais kililiambia gazeti la Sunday Nation.

Chanzo kingine ndani ya ofisi ya Waziri Mkuu kilieleza kuwa Bw. Odinga amefikia uamuzi wa kumtema Bw.  Ruto na washirika wake kwa ajili ya maslahi ya chama.(Daily Nation).




No comments:

Post a Comment