17 August 2011

Masaburi: Niko tayari kuwalipa Mtemvu, Zungu

Na Rachel Balama

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Dkt. Didas Masaburi, amesema atakuwa tayari kuwalipa fidia wa sh. bilioni 5 wabunge wawili wa Dar es Salaam, iwapo mahakama itaamua
hivyo, kama wabunge hao wanataka kulipwa faini.

Hatua hiyo imetokana wabunge wawili wa Jiji la Dar es Salaam,  Bw. Abbas Mtemvu (Temeke) na Bw. Mussa Zungu (Ilala) kudai kuwa aliwatukana wakati alipofanya mkutano na waandishi wa habari mjini Arusha.

Dkt. Masaburi alikaririwa na vyombo vya habari katika mkutano huo alisema kuwa wabunge hao wanatumia makalio kufiri badala ya vichwa vya, suala ambalo pia limefikishwa kamati Kamati ya Maadili, Kinga na madaraka ya Bunge.  

Alitoa kauli hiyo Dar es salaam jana, alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua kama atakuwa tayari kuwalipa fidia wabunge hao.

"Wao si wanadai nimewatukana na kuwadhalilisha na wanataka niwalipe sh. bilioni 5, nitawalipa endapo mahakama itaamua hivyo," alisema Dkt. Masaburi.

Alisema kuwa wabunge hao wamekuwa wakimwandama baada ya kuvunja Bodi ya Shirika la Usafirishaji Mkoa wa Dar es Salam (UDA) na baadaye kujipa jukumu la kuvunja Bodi ya Shirika la Maendeleo Mkoa wa Dar es Salaam (DDC), hatua mbayo ilibatilishwa na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, ikifafanua kuwa hakuwa na mamlaka hayo.

Bw. Masaburi alisema kutokana na mikataba hiyo, ndiyo maana wabunge hao wanajitahidi kumnyamazisha ili asiendelee kukagua miradi na kuibua uozo uliochangia jiji kukosa mapato.

Alisema lengo la baadhi ya wabunge hususani wa Jiji la Dar es Salaam kumtaka ajiuzulu kutokana na kashfa aliyoibua, ni kumfanya asitimize ukaguzi wa mali za jiji na kuwasihi wabunge hao waache kutafuta umaarufu kwani baadhi yao ni miongoni mwa watakaoumbuka kutokana na kuuza viwanja na mali zingine za jiji.


Alisema, amefanya ukaguzi wa mali za jiji na kugundua ubadhirifu, ndipo alipoamua kuvunja bodi za UDA na DDC kwa maslahi ya umma na wananchi kwa ujumla kwa kuwa ni watu wachache walikuwa wakinufaika na mali hizo na ndio maana wanataka asimamishwe.

Alisema kuwa mbali na kuvunja bodi hizo mbili pia atafanya ukaguzi kwenye jengo la Machinga Complex na atakapogundua kwamba kuna ubadhirifu ndani ya jengo hilo hatua zitachukuliwa dhidi ya wahusika wote.

Alisema kuwa lengo la kwenda kukagua jengo hilo ni kuangalia mikataba kutokana na kuwepo kwa tetezi kwamba kuna watu wamepewa mabanda ambao si wa machinga na ndio maana hadi leo hawajaweka biashara.

"Kuna tetesi kwamba kuna watu wamepewa mabanda ambao si walengwa na pia kuna mikataba ya ovyo na nikibaini kama hayo yote yapo nitawachukulia hatua," alisema Dkt. Masaburi.

Wabunge hao wa Dar es Salaam waliingia katika malumbano na Bw. Masaburi baada ya kuafikiana na hatua zilizochukuliwa na serikali kuagiza uchunguzi dhidi ya madai ya uuzaji holela wa UDA, tuhuma ambazo pia zinamhusisha Bw. Masaburi.

5 comments:

  1. Masaburi anatakiwa awe Kimya
    ni wakati wa kukaa Kimya ili kukujenga Chama

    TEMBELEA
    http://malariasugu.6te.net

    ReplyDelete
  2. MAKABURI KOMAAAAAA NAO HAO HATA KAMA HUNA MAMLAKA YA KUVUNJA HIYO BODI, WAZIRI MWENYE MAMLAKA ANATAKIWA KUIVUNJA KAMA KWELI SABABU ULIZOTOA ZINA UKWELI. MPE WAZIRI SABABU ZA KUIVUNJA BODI NA UMSHURI AFANYE HIVYO MAANA KUKAA KIMYA KWA WAZIRI (NA KUBATILISHA UAMUZI WAKO) KUNAONESHA KUWA WAZIRI NAYE NI BENEFICIARY WA HIYO MIPANGO FEKI

    ReplyDelete
  3. Mtu hawezi kufumbia macho uozo eti kisa anajenga chama. Ni kipi bora kukaa kimya kwa malengo ya kujenga chama au kuendelea kuzungumza kwa maslahi ya taifa zima. Nadhani Masaburi hapaswi kuteteleka juu ya harufu yoyote ya ufisadi katika mali za jiji. Mwisho wa siku ukweli utajulikana na tutajua ni yupi mwenye makosa.

    ReplyDelete
  4. mpaka sasa nipo dilema, ila napenda kushauri kuwa tuwe na udesturi wa kufanya kazi na sio kukomoana. kinachoonekana hapa ni kukomoana kwa maana mh masaburi anafanya haya kwa sababu ya ugomvi wake na wabunge wa Dsm, kinyume chake asingefanya hizo ziara na kuwasaidia wananchi kwa namna moja na nyingine. ila tufahamu kuwa viongozi wetu hawa kwa ajili ya maslahi ya wananchi au nchi kwa ujumla bali ni kwa maslahi yao binafsi wanapotofautiana ndio wanarudi kwa wananchi na kujisafisha. othman

    ReplyDelete
  5. MASABURI hapaswi kukaa kimya hao wanaotaka ukae kimya na hao wanaodai hana mamlaka WANATAKA KUTUFUNIKA; jitoe mzee utugombelezee wananchi iko siku historia itakukumbuka usijali fitina zao! Fisadi na wakala wa fisadi anaonekana waziwazi, wamezoea kuutumia umaskini wetu kutunyonga; TUKO NYUMA YAKO MZEE MASABURI FUATA SHERIA USIMUONEE MTU WALA USIMUONEE MTU HAYA. (kila jambo huanzia mahali fulani)

    ReplyDelete