15 August 2011

Mahakama yamnusuru mbunge kupimwa UKIMWI

HARARE,Zimbabwe

JAJI wa Mahakama Kuu ya Zimbabwe,amesema kuwa mahakama hiyo haiwezi kuwashurutisha watu kufanyiwa vipimo vya UKIMWI, hivyo ikatupilia mbali mashtaka
yaliyokuwa yakimkabili mbunge wa chama cha upinzani  nchini humo.


Bw.Siyabonga Ncube,kutoka chama kidogo cha upinzani cha  Movement for Democratic Change (MDC) alikamatwa mwezi uliopita akishutumiwa kumwambukiza virusi vya UKIMWI mwandishi wa habari wa gazeti la serikali.

Wawili hao walikuwa kwenye mahusiano kuanzia Agosti 2009 hadi Julai 2010 na mwandishi huyo anadai kuwa aliambukizwa virusi hivyo vinavyosababisha ugonjwa wa UKIMWI ndani ya kipindi hicho cha  mahusiano yao.


Umuzi huo wa Mahakama Kuu umekuja baada ya awali mahakama moja nchini humo kuamru, Bw. Ncube kwenda kufanyiwa vipimo hivyo, lakini mbunge huyo akakata rufaa katika mahakama hiyo  akipinga uamuzi huo.

Akitupilia mbali mashtaka hayo juzi, Jaji  Maphios Cheda alisema kuwa anakubaliana na upande wa utetezi kuwa malalamiko hayo hayana msingi.


Kabla ya kutolewa maamuzi hayo,Bw. Ncube ambaye alikuwa akikana mashtaka hayo alikuwa akikabiliwa na kifungo cha miaka 20 jela.(Sunday Nation).



No comments:

Post a Comment