Na Benjamin Masese
RAIS Jakaya Kikwete amelitaka Jeshi la Polisi nchini kufanya mabadailiko ya utendaji kazi haraka, ili kuhimili mabadiliko ya teknolojia kwa kuwa kila kitu kimebadilika
duniani.
Pia amelitaka jeshi hilo kuajiri wanawake kwa wingi hadi ifikie hatua liwe na Mkuu wa Jeshi hilo mwanamke.
Rais Kikwete alitoa maelekezo hayo Dar es Salaam jana wakati akifunga sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya uhuru yaliyofanyika Chuo cha Polisi Dar es Salaam. Rais pia aliwatunuku vyeo wahitimu 290 wakiwemo wakaguzi sita na maofisa wanne baada ya kufuzu mafunzo.
Alisema idadi ya wanawake walioajiriwa ndani ya jeshi la polisi hairidhishi kama ilivyo kwa sekta zingine, ambazo wameonesha umahiri mkubwa wakati wa utekelezaji wao majukumu yao. Alisifiwa wanawake kwa kutowahi kupatikana na rushwa kama ilivyo kwa wanaume.
Rais Kikwete alisema hivi sasa dunia imebadilika na inafanya kazi kwa teknolojia ya hali ya juu, huku Tanzania inaonesha haijafikia kiwango kinachostahili.
Rais Kikwete alisema kuwa kuna haja kubwa ya mifumo ya mafunzo inayotolewa vyuoni kufanyiwa maboresho ya haraka ikiwemo kutoa mafunzo kwa vitendo ili kuwa na maofisa wenye elimu, nidhamu, maadili na uwezo wa kufikiria haraka.
Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Shamsi Vuai Nahodha, alisema kadri nchi inavyozidi kupiga hatua ya kimaendeleo, kiuchumi, kisiasa, kielimu na kijmii ndivyo migogoro inazidi kuongezeka.
Bw. Nahodha alisema kutokana na hali hiyo, kuna haja ya jeshi la polisi kuanzisha mafunzo ya utatuzi migogoro kwa njia ya migogoro.
No comments:
Post a Comment