30 August 2011

Gari lapinduka na kuua watano

Na Cresensia Kapinga, Songea

WATU sita wameteketea kwa moto papo hapo huku miili yao ikiwa haitambuliki na wengine wawili kujeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria
kupinduka na kuwaka moto katika Kijiji cha Chunya kilichopo wilayani Mbinga mkoani Ruvvuma.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoani hapa Bw. Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 12 jioni katika Kijiji cha Chunya kwenye barabara ya Mbinga Mbambabay ambapo gari lenye namba T 270 BDG Landrover likiwa linaendeshwa na dereva Steven Ngoko (32)lilipinduka na kuwaka moto na kusababisha vifo vya watu sita papo hapo.

Aliwataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni Jeremia Masalo (38) mkazi wa nchi jirani ya Msumbiji na Anna godrfei (3) mkazi wa Mbambabay ambao wote wamelazwa katika hospitali ya Serikali ya Wilaya ya Mbinga kwa matibabu.

Alisema kuwa watu waliokufa majina yao hayajaweza kufahamika kutokana na maiti hizo kutotambulika kwa kuwa zimeungua vibaya na zote zimepelekwa  katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya wilaya ya Mbinga. Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo mkali na kwamba polisi wanamsaka dereva.



 


No comments:

Post a Comment