Na Mwandishi Wetu
MSANII wa kizazi kipya, Diamond Platinumz, juzi aliwapa burudani nzuri wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Sangara iliyopo Chanika mkoani Pwani.Katika burudani hiyo, mwimbaji
huyo anayejiita Rais wa Wasafi alitumia nafasi hiyo kuwapa raha ya nyimbo zake zinazotamba hivi sasa.
Nyimbo alizopanda nazo jukwaani ni Nenda kamwambie, Nitarejea na Mbagala ambao unatamba nchini.
Airtel Tanzania, pamoja na burudani hiyo, pia imejiingiza katika mchakato wa kukuza vipaji vya wanafunzi katika mpira wa miguu.
Kampuni hiyo mwaka huu kwa kushirikiana na nyota wa zamani wa Manchester United, Andy Cole, walizindua mpango maalumu wa kuibua na kuendeleza vipaji vya soka kwa wanafunzi.
Onesho la Dimond lilikuwa la kuvumbua vipaji na kuwaelimisha wanafunzi mambo mbalimbali ya kijamii na masomo.
Onesho hilo lililodhaminiwa na Airtel Tanzania, lilipambwa na wanenguaji wanne wa msanii huyo.
Aidha waadhamini wa shoo hiyo Airtel walisema bado kampuni itaendelea na mtindo huo wakuwazawadia wanafunzi wa shule mbalimbali burudani ili kuwafanya wanafunzi waweze kupumzika baada ya kuwa kwenye masomo kwa muda mrefu
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, alisema wataendelea kuandaa burudani kwa wanafunzi na kutoa zawadi mbalimbali.
"Tutaendelea na utaratibu huu wa kuwapa burudani wanafunzi ambao ni fleva za airtel mashuleni, hii inawasaidia wanafunzi wafurahie na kuburudika wakiwa masomoni," alisema.
Mbali na burudani hiyo, pia Airtel iliwazawadia wanafunzi wa shule hiyo fulana, madaftari na kofia.
Burudani ya Flava za Airtel kwa shule za sekondari hufanyika kila mwezi mara moja, ikiwa na lengo la kuibua vipaji mbalimbali vya sanaa kama kuimba, kuonesha mavazi na kucheza muziki.
No comments:
Post a Comment