30 August 2011

Beyonce atangaza kuwa mjamzito!

LOS ANGELES, Marekani

MWIMBAJI nyota wa muziki Beyonce, ametangza rasmi kuwa ni mjamzito ambapo anatarajia kupata mtoto wake wa kwanza.Mwanamuziki huyo ambaye ni mke wa
rapa mahiri Jay-Z, aliweka wazi suala hilo katika sherehe za utoaji tuzo za Video Bora za Muziki za MTV.

Gazeti la Daily Mail, limesema mwimbaji huyo wa Single Ladies alionekana kuwa na furaha na kuonesha wazi tumbo lake kwa wapiga picha ambapo aliwaambia,"Pateni kitu cha kushtua" huku akipozi kwa ajili ya kupigwa picha.

MTV nayo baada ya muda iliandika katika Twitter: "OMG Beyonce ametoa tangazo kubwa 'Mtoto'.

Alipoanza kutumbuiza wimbo wake wa Love On Top, Beyonce aliwaambia mashabiki, "Ninataka ninyi mhisi penzi ambalo linakuwa ndani yangu."

Baada ya kutumbuiza, aliweka chini kipaza sauti na alitoa koti na kushika tumbo lake, huku mwanamuziki Kanye West akimpongeza Jay-Z katika umati wa mashabiki.

Beyonce alioana na Jay-Z Aprili 2008 mjini New York.

Alieleza kuhusu mipango yake ya kuanza kuwa na familia katika mahojiano aliyofanya na Piers Morgan hivi karibuni.

Alisema "Kila wakati nilikuwa nikisema nitakuwa na mtoto nikiwa na umri wa miaka 30. Kwa sasa nina umri wa miaka 29.

"Lakini pia nilisema nitastaafu nikiwa na umri wa miaka 30. Kwa hiyo sijui. Siwezi kustaafu, ninakwambia.

"Mungu pekee ndiye anayejua, Mungu pekee ndiye ajuaeye."

Beyonce aliyekuwa amevaa gauni refu jekundu ambaye mwezi ujao anatimiza umri wa miaka 30, alipata tuzo ya ubunifu mzuri wa video katika wimbo wake wa Run the World (Girls), akimshinda Lady GaGa kwa wimbo wa Judas, Britney Spears kwa Till the World Ends na Bruno Mars kwa wimbo The Lazy Song.

Tangazo lake kuwa ni mjamzito liliwafanya wasanii wengine kuzizima, akiwemo Lady GaGa ambaye alifungua onesho.

GaGa jukwaani aliungana na Brian May kupiga gita. Lady GaGa baadaye alipata tuzo ya Video Bora Yenye Ujumbe kwa wimbo wa Born This Way.

Miongoni mwa wasanii nyota waliohudhuria hafla hiyo ni Jessie J, Ne-Yo, X Factor judge Kelly Rowland, Katie Holmes, Kim Kardashian, Miley Cyrus na Jersey Shore.

No comments:

Post a Comment