05 July 2011

Tuko radhi Shibuda atimuliwe-Lissu

Na Grace Michael, Dodoma

SAKATA la Mbunge wa Maswa Magharibi, Bw. John Shibuda na Chama cha Demokrasia na  Maendeleo (CHADEMA) limechukua sura mpya baada ya wabunge wa
chama hicho kuweka msimamo kuwa wako tayari kumfukuza uanachama na kurudi kwenye uchaguzi endapo Kamati Kuu itaridhia na kuona kuwa hafai kuwa katika chama hicho.

Msimamo huo ulitolewa jana mjini hapa na Mnidhamu wa Kambi ya Upinzani, Bw. Tundu Lissu baada ya kuhojiwa na waandishi wa habari kuhusu hatua wanazotarajia kuchukua dhidi ya mbunge huyo baada ya kutangaza vita na chama hicho.

“Tuko tayari kuachana naye na kurejea kwenye uchaguzi... hatuwezi kuvumilia tabia ya namna hiyo ambayo ameifanya wazi ya kupingana na sera ya chama na muda huu ndo namwandia barua rasmi ya kumtaka ajieleze ni kwa nini anakwenda kinyume na  msimamo wa chama,” alisema Bw. Lissu na kuongeza kuwa:

“Hatua ambayo tunaweza kwa upande wetu hapa ni kumtaka ajieleze lakini baadaye suala hili litajadiliwa katika na Kamati Kuu ya chama ambayo ina mamlaka makubwa zaidi yakiwemo ya kumfukuza uanachama na katika hili halina visingizio kwa kuwa amelifanya wazi na msimamo wetu tuko tayari kurudi kwenye uchaguzi...na kama anaweza arudi alikotoka,” alisema Bw. Lissu.

Alipohojiwa kuhusu kauli ya Bw. Shibuda ambaye alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema yuko tayari kuanza kuhubiri mabaya ya CHADEMA na viongozi wake akiwemo, Bw. Freeman Mbowe na Bw. Zitto Kabwe, Bw. Lissu alisema kuwa hana jipya la kuhubiri dhidi ya chama hicho kwa kuwa hana anachokijua.

“Hivi Shibuda atahubiri nini kibaya cha CHADEMA? Ni muda gani aliotumia katika kuyajua hayo anayodai? Kwanza hata vikao sidhani kama kuna vikao zaidi ya vitano ambavyo amehudhuria tangu ajiunge na chama, hivyo hana jipya zaidi ya kusema matapishi ambayo yamekuwa yakihubiriwa kila siku kuwa CHADEMA ni chama cha wachaga,” alisema Bw. Lissu.

Mtafaruku huo wa Bw. Shibuda na chama chake ulitokana na msimamo wake aliouonesha wiki iliyopita bungeni wakati akichangia hotuba ya Waziri Mkuu ya bajeti ya  2011/2012 ambapo aliiomba serikali kuongeza posho za vikao hadi sh 500,000 kutoka sh 70,000 kwa siku badala ya kuziondoa kama CHADEMA kinavyotaka.

Bw. Shibuda pia alipendekeza kubadilishwa kwa jina la posho na kuitwa ‘ujira wa mwia’ ili kuondoa mawazo mabaya yanayotokana na neno posho hizo.

Hatua hiyo ya Shibuda ilikwenda kinyume na msimamo wa Kambi hiyo ya Upinzani hasa CHADEMA ambao tayari wametoa msimamo wao kutosaini posho hizo, endapo fomu zake zitatenganishwa na zile za mahudhurio.

17 comments:

  1. Jambo kama liko katika kamati ni bora ikakaa likajadiliwa kuliko sasa wanapohojiwa nje ya vikao nikuzidisha chuki
    na mparaganyiko ktk chama maana kila mmoja anatoa maoni yake ambayo sasa inajionyesha wazi kuwa hata hivyo walikuwa kama wanamtafutia sababu maana maneno kama haya ni kuongeza mpasuko usio na tija kama chama kinaona hafai ni bora kuitwa akajieleza na kumtimua je? Ikiwa ataonywa
    na kuwemo kyk chama si chuki baina yao itazidi?Itumike busara kuliko jazba!!

    ReplyDelete
  2. WEWE LISU UNATUMIWA NA WACHAGA UNABWATUKA OVYO. NYIE KAMA MNA UCHUNGU NA NCHI HII MBONA HAMSEMI KUHUSU MAKANISA YANVYOFUJA PESA ZA SERIKALI. KUNA SUKARI TANI 5,000 KUTOKA MALAWI ILIINGIZWA BURE KUTOKA MALAWI KUPELEKWA SINGIDA KWA WATOTO YATIMA KANISANI,IKAKAMATWA TANI 4,995 MAKAMBAKO INAUZWA MADUKANI. HILO HAMLISEMI WIZI WENU WA KANISANI. KANISA JINGINE LIKAINGIZA MABATI 4,000 , LIKATUMIA MABATI 200, MABATI 3,800 MZEE WA KANISA AKAENDA KUYAUZA KWA BEI YA SOKO. KWA NINI HAMSEMI HILI?

    ReplyDelete
  3. PIA HAMSEMI KUHUSU SUKARI ILIYOFICHWA NA MBUNGE WA CCM UKO IRNGA NDANI YA MAGODAUNI,POLISI WALIKAMATA LAKINI KESI HAKUNA USHAIDI,PIA HAMSEMI KUHUSU MAFISADI WA EPA,KAGODA NK WANAOENDELEA KUPETA TU BILA HATUA KUCHUKUIWA,PIA YALE MAGAMBA YANAYOELEKEA KUNGANGANIA CCM LICHA YA JUHUDI ZA NAPE HAMUYASEMI,KWELI MMETUMWA NA WACHAGA

    ReplyDelete
  4. eng.mwakapango,E.P.AJuly 5, 2011 at 10:04 AM

    CHADEMA huu ndiyo wakati wa kuonyesha ukomavu wa kisiasa. Muelewe sasa hivi CCM wanatumia kila njia kuhakikisha kuwa mnaanza kugombana na kukisambaratisha chama kwani walifanyaje kuisambaratisha NCCR Mageuzi na Mrema? Shibuda ametoa msimamo wake na hayo ndiyo mawazo yake nyie achaneni na mawazo yake kama mkipiga kura Shibuda atachangia asilimia chini ya kumi sasa kidemokrasia bado msimamo wa chama unabaki palepale. muelewe kuwa watanzania wote ikiwa pamoja na wananchi wa maswa wanawasikiliza achaneni naye nguvu za wananchi zitamhukumu. mkimfukuza Shibuda watakuja kwa mwingine naye watafanya vivyo hivyo. naomba niwashauri CHADEMA kwanza msipoteze muda kabisa itafikia mahari bwana Shibuda atakimbia mwenyewe kurudi kule anakopokea maelekezo ya kusambaratisha chama. vile vile rafiki yangu Tundu Lisu acha kabisa kumwaga mchele kwenye kuku wengi maamuzi ya chama ni siri mpaka pale yatakapotolewa hadharani. Inaonyesha bwana Shibuda amelogwa na mtu aliyemloga amekwishafariki hivi kupona naye si rahisi. Freeman Mbowe na Dr. Wilbroad slaa okoeni jahazi tunawategemea mtumie busara zenu kama mlivyotumia wakati ule bwana huyo alipotoa misimamo tofauti na chama. Mnatakiwa muwape semina elekezi hao waliokuwa makada wa CCM.

    ReplyDelete
  5. Chadema tunawaaminia, ila tunashauri hao makada wanaokimbia vyama vingine (hasa sisiemu) na kujiunga kwa haraka haraka muwachunguze kwanza,maana huwa wana vimelea vya chama alikotoka , halafu muwapokee, lakini kwa kuwa ni uhuru wa mtu, muwe makini nao, wasipewe dhamana kubwa ndani ya chama, maana nahisi huyo shibuda anafanana na MREMA, mchafua vyama vya upinzani makini.

    ReplyDelete
  6. CHADEMA NI CHAMA CHA FAMILIA tu maana TunduLisu , Mbowe , silaa na wengineo mmejaza familia zenu humo , hata mawazo ni kifamilia zaidi , watanzania acheni mkumbo wa siasa za kifamilia, hawajapata madarka wameanza ubinafsi wakipata jee? fuatilieni kwa makini mtawajua ndugu za hawa watu katika chama hiki.UKABILA NA UBINAFSI UMEJAA

    ReplyDelete
  7. aCHA U LO FA WEWE! RIDHWANI, SALMA NA JAKAYA SI FAMILIA NDANI YA CCM? JANUARY NA BWATA HOVYO BABAAKE NAO IMEKAAJE? NAPE NA MOSES JE? KINJIKITILE NA KIKONGWE KINGUNGE JE? KAMA U FAMILIA BASI CCM NAMBARI WANI! NYIE NGOJENI TU 2015 TUTAWATOA NDUKI KAMA HOSNI MUBARAK AU BEN ALI!

    ReplyDelete
  8. Kuna mijitu humu inatumia kamasi badala ya ubongo, huo ufamilia wa chadema uko wapi, mwingine anasema hawaongelei kuhusu epa, kagoda nk, hivi nani alietoa list of shame, mamluki wa ccm sijui ni chekechea maana hata wangekuwa darasa la saba wangekuwa na ufahamu kidogo,hovyo kabisa Chama Cha Mafisadi(ccm)

    ReplyDelete
  9. HUU NI WAKATI HASA WA KUCHAMBUA PUMBA. CHADEMA LAZIMA MUELEWE KUWA MAKAPI YA CCM MYAOGOPE KAMA UKOMA KWANI HAO BADO WANA DAMU YA UFISADI. KWAO MASLAHI YAO BINAFSI WANAYAWEKA MBELE KULIKO YA TAIFA. INASIKITISHA KUONA BAADHI YA WATU BADO WANA MAWAZO MUFILISI ETI KUSEMA CHADEMA NI CHA FAMILIA,MBONA HAMUKISEMI CCM AMBACHO NDIYO KINAONGOZWA NA FAMILIA ZA AINA MOJA? ACHENI KUWA NA AKILI ZA ULAMBA VIATU, MTAKUFA MASKINI HUKU WENZENU WAKINEEMEKA NA KODI ZENU. HUU NI WAKATI WA MABADILIKO HASA KWA VIJANA MNAOKAA VIJIBWENI HUKU HAMJUI MTAKULA NINI! INASHANGAZA SANA.KUMBUKENI SAA YA UKOMBOZI NI SASA. SISI BADALA YA KUPANDA JUU TUNAZIDI KUSHUKA, ANGALIA MGAO WA UMEME, SHULE ZA KATA, JE KATIKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI MMEYASIKIA HAYO? BADILIKENI.

    ReplyDelete
  10. Tatizo kubwa la CHADEMA ni Mbowe,yeye ni milionea,anajidai eti hataki posho,mbona posho ya chai anachukua,amekiuzia chama magari yake mabovu kwa bei mbaya,mbona hajahojiwa?au kwa kuwa ni chama cha baba mkwe wake?wewe Lissu na Zito hamjui mlifanyalo,Tena nawaambia Chadema bila kuondoa ukaskazini wenu,nchi hii mtaisikia tu.

    ReplyDelete
  11. shida kubwa ya chadema na wanachama wake ni jazba,hawana hoja.fanyeniuchunguzi mtajionea kati ya wabunge wote wa viti maalum muone ni wangapi wanatoka kaskazini,acha kutukana tu.shida yenu kuanzia kwa chairman upstairs ni zero

    ReplyDelete
  12. chadema hakuna demokrasini ubababe tu kwanza mtu kama freman mbowe hawezi kuwa kiongozi hana busara yeyote,slaa kakimbilia chadema baada ya kuangushwa kura za maoni kama shibuda hivyo vichwa vyote vya uongozi chadema vimejaa visasi ni mwendawazimu tu anae shabikia chadema.consevartive inawapa pesa za misada mahesabu yake ya matumizi hayajulikani chacha wangwe kutaka kujua zaidi mka mmaliza,kafulila kataka kutumia demokrasi kugombea vijana kwa kuwa muha mmemfukuza,zito anaishi kama fisi kwa matumaini mkono udondoke apete riziki.slaa na mbowe wataendelea kungombea uraisi mpaka wafe.ata uteuzi wa wabunge wakuteuliwa chadeama ni mizengwe mitupu chadema ni ngo ya mtei.

    ReplyDelete
  13. Shibuda Ni Mtu anayejulikana kwa kuwa na misimamo hasi na wengine, kwa hiyo hilo alilolifanya ni la kawaida kabisa.msitegemee hata siku moja mkakubaliana naye jambo.Sasa kinachotakiwa hapa ni usara zaidi na ujasiri.Akiendelea kukaa Chadema siku ya kutoka atawaharibia chama.Bora mumuwahi mapeeeema!

    ReplyDelete
  14. Na wewe Tindu pia ujue siku yako ikifika utatimuliwa pale utakapopingana na fikra za hao wachaga. Wabunge wa Chadema wanatakiwa waseme zidumu fikra za Mbowe,Mtei,Ndesa,Lymo ni hawa ndio wenye chama na Slaa iko siku watamuua akisha wakamilishia mambo yao.Shibuda kaa sawa kumbuka ya mbunge wa Tarime hao ni Mafia kwenye mapesa hata baba zao wanauwa.

    ReplyDelete
  15. HIZO ZOTE NI HARAKATI,,,,HAIJATOKEA NA HAITOTOKEA SIKU HATA MOJA MAMBO YA MWANADAMU YAKAWA BILA VIKWAZO....MUHIMU NI KUSIMAMIA YALE YENYE UKWELI...NA UKWELI NI HUU: CCM IMECHOKA....HAKINA KIPYA KWA MUSTAKABALI WA TAIFA LETU....NI UGUMU TU WA WATANZANIA KUNG'AMUA MAMBO...CHAMA HAKINA DIRA WALA MWELEKEO..WANAKALIA AJENDA ZA UDINI, UKABILA, UFISADI, MABAVU!!! TUNDU ENDELEA KUWAAMBIA UKWELI IPO SIKU HISTORIA ITAWEKA MAMBO SAWA.

    SHIBUDA KUWENI NAYE MAKINI...ALIWAHI KUMCHANGIA KIKWETE PESA ILI ACHUKUE FOMU (RAIS MBOVU KULIKO WOTE DUNIANI...HAJUI HATA KWANINI NCHI YAKE NI MASKINI!!!) SHIBUDA ALIKUWA ANAMKUBALI NA NADHANI BADO ANAFANYA HIVYOO...

    ReplyDelete
  16. TANZANIA SIJUI TUMEROGWA...NO HAPANA....SHIDA YETU SISI NI MIFUMO MIBOVU YA CCM...NCHI HAIENDELE!!! WATANZANIA WENGI HAWAENDELEI...BALI WATU WACHACHE NDANI YA CCM WANANUFAIKA...WANAUTAJIRI WA KUTISHA...

    RAIS WA NCHI ANAOMBA MISAADA KUTOKA KOREA..MIONGONI MWA NCHI TULIZOKUWA KTK HALI MOJA YA UMASKINI...LEO WANATOA MISAADA KWETU...ALAFU KIONGOZI ANAONA SAWA TU...
    WATANZANIA MKIWAENDEKEZA KINA SHIBUDA NA WENZAKE WA CCM ALIKOKUWEPO HATUTAKUWA NA NCHI HAPO BAADAYE....
    TANZANIA NI NCHI TAJIRI LAKINI VIONGOZI WETU NI MASKINI WA FIKRA ENDELEVU...WANANCHI WENGI UANGALIA TU LEO ATAVAA NINI,,,ATAKULA NINI BILA HATA KUVIFIKIRIA VIZAZI VYAO VIJAVYO...KICHEFUCHEFU...WAKIJA WATU WANA AKILI ZAO MNADAI WACHAGA...

    DHAMBI YA UBAGUZI ILIOANZISHWA NA CCM ITAWATAFUNA HATA WAO...TUWE MAKINI NCHI YETU ISIPELEKWE KUZIMU NA CHAMA CHA MAFISADI (CCM) KILICHOKOSA DIRA!!!

    ReplyDelete
  17. Kama CHADEMA ni chama cha Familia au Kabila Mbona hamsemi CCM kuwa Chama cha WAislamu maana kuna viongozi wengi wa juu wanaoteuliwa ni waislamu.Acheni upungufu wa kuona mbali na Tumieni elimu zenu kuchambua mambo na kama elimu zenu haziwatoshi njooni tuwafundishe.Otherwise Naomba vyama vya siasa kabla ya kumpa mwanachama yeyote toka chama kingine nafasi ya kugombea ubunge awe mwanachama kwa angalau miaka mitano akijifunza sera na misimamo ya chama husika

    ReplyDelete