Na Daud Magesa, Mwanza
WAKATI Watanzania wanaendelea kulaani vurugu zilizotokea jijini Mwanza na Dar es Saalam na kusababisha watu kadhaa kuumizwa na wengine makumi
kukamatwa, chanzo cha vurugu hizo imetajwa kuwa ni maslahi ya kisiasa kati ya viongozi wa juu wa halmashauri hiyo.
Viongozi hao ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bw. Wilson Kabwe na Meya wa Jiji hilo, Mstahiki Josephati Manyerere, ambao wanadaiwa kukosa ushirikiano hivyo kusababisha kuzuka kwa vurugu hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusiana na vurugu hizo, Meya Manyerere alidai kuwa Bw. Kabwe hamshiriki katika baadhi ya maamuzi, jambo linalosababisha mgongano hadi vurugu hizo.
Bila kufafanua, alidai kama angeshirikishwa uamuzi wa kuwaondoa wafanyabiashara wadogo katika eneo isiyoruhusiwa juzi vurugu hizo sisingetokea.
Alisema wakati ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji ilipanga shughuli ya kuwaondoa baadhi ya wamachinga waliovamia eneo la msikiti na shule ya awali ya Wahindi, yeye hakushirikishwa katika maamuzi hayo.
Alisema mpango wa zoezi hilo alielezwa Mkuu wa Mkoa, Bw. Abbas Kandoro, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bw. Said Amanzi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Bw. Simon Sirro, lakini yeye (Meya), hakupewa taarifa licha ya kuwa kiongozi wa halmashauri hiyo.
“Maamuzi ya kuwaondoa wamachinga sikushirikishwa na sikupewa taarifa ya zoezi la juzi kama walivyoshirikishwa Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya. Kilichotokea juzi kisingetokea laiti ingeshirikishwa,” alidai Meya huyo.
Kutokana na kutopewa taarifa amewataka wamachinga kuendelea na biashara zao kama kawaida katika maeneo ya Makoroboi hadi suala lao litakapopelekwa katika Baraza la Madiwani litakalokutana hivi karibuni.
Alidai Mkurugenzi anafanya hivyo kwa mazoea ya mfumo wa chama kimoja na kueleza kuwa serikali iwe tayari na hasa halmashauri zinazoongozwa na wapinzani kuridhia kutumia mfumo wa chama husika.
Aliuomba uongozi wa shule na msikiti huo kuendelea kuvumilia hadi ofisi yake itakapolishughulikia suala hilo kwa kuwatafutia wamachinga eneo la kufanyia biashara yao.
Naye Mbunge wa Nyamagana, Bw. Ezekia Wenje alisema yupo tayari kupelekwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita endapo ataonekana amefanya kosa kuwatetea wamachinga kufanya biasahara katika mitaa ya
katikati ya Jiji la Mwanza.
Bw. Wenje alisema katika nchi zote duniani wafanyabiashara ndogo ndogo wamekuwa wakifanya biashara zao katika maeneo yaliyopangwa katikati ya jiji na sio nje ya mji ambako hakuna wanunuzi wa bidhaa zao.
“Nitakuwa tayari kufikishwa The Huegue, hadi watakapokuwa wamepata eneo la kufanyia biashara yao. Kauli za vurugu hizo ni za kisiasa nyepesi," alisema Bw. Wenje.
Alidai suala hilo la wamachinga lipo muda mrefu na kwamba chanzo cha tatizo ni serikali kuwaruhusu wakati wa uchaguzi mkuu, na kuwa hata Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) huwa hawakusanyi kodi kuhofia kura za CCM kuharibika.
Mbunge huyo aliwatembelea waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, na kueleza kuwa uchunguzi wa polisi unaonesha kuwa walijeruhiwa kwa risasi za mgambo wa jiji, wakitumia bunduki aina ya short gun na si polisi kama ilivyodaiwa.
Muuguzi wa zamu katika hospitali ya Bugando, Bw. Ramadhani Simba, alisema mmoja wa majeruhi hao, Bw. Juma Machumu, bado yuko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU).
Wakati huo huo, Jeshi pa Polisi mkoani humo limezuia mikutano ya hadhara ya vyama vya CCM na CHADEMA iliyopangwa kufanyika jana, kutokana na vurugu zilizotokea juzi.
Wilson Kebwe anajulikana ni kada wa CHAMA CHA MAFISADi (CCM) hilo halina ubishi ndio maana hata katika uchaguzi mkuu uliopita alitumia hila kumwondoa katika Uchaguzi mgombea wa CHADEMA. Pia alishiriki kikamilifu katika ufisadi wa kuchakachua matokea lakini nguvu ya umma ikamshinda.
ReplyDeleteinakuwaje mkurugenzi wa mji anakuwa na nguvu kuliko meya?? ktk miji yote duniani meya ndiye mwenye nguvu kuliko yeyote ni kama rais wa mji usika kwa maana yeye amechaguliwa na wananchi na siyo mkurugezi ambaye anateuliwa tu. meya inabidi awe na mamlaka ya kuchagua watu anaotaka kufanya nao kazi ktk mji wake na siyo kuteuliwa mtu
ReplyDeletena watu wengine kwahiyo meya inabidi apewe mamlaka ya kumchagua mkurugenzi wake bila hivyo mgongano wa kimadaraka utaendelea kwa muda mrefu.