Na Amina Athumani
KUNDI la muziki wa kizazi kipya la Tanzania House of Talent (THT), litawasindikiza wanyange wanaowania umalkia wa Kanda ya Kaskazini litakalofanyika katika
ukumbi wa Snow crest jijini Arusha, Ijumaa.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Jazz Promotion inayoratibu mashindano hayo, Emma Mroso, alisema kundi limeandaa burudani mpya kwa ajili ya mashabiki wa urembo watakaohudhuria shindano hilo.
Alisema maandalizi kwa ajili ya mashindano hayo yamekamilika, na kwamba jumla ya warembo 13 watapanda jukwaani kusaka nafasi hiyo.
Mshindi katika mashindano hayo, atashiriki mashindano ya taifa ya Miss Tanzania ngazi ya Taifa, ambapo washiriki katika shindano hilo wanatoka katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Manyara.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa, wanyange hao wananolewa na Glory Mwanga, atavua taji hilo siku hiyo.
"Mashindano ya mwaka huu yameboreshwa katika kila idara, kwa upande wa burudani mwanamuziki Lina na kundi la THT watatoa burudani," alisema.
Alisema leo warembo hao watapata nafasi ya kutembelea wadhamini wa mashindano hayo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na wadhamini hao.
Mashindano hayo yamedhaminiwa na Redd's, Vodacom, Tanzaniteone, snow Crest hotel, Arusha Mambo, Arusha Art, Cybernet, Creative Studio, Ndeku Hair Salon, Little Roses, Jzz Collectoin, Safariland, na Adventure limited.
No comments:
Post a Comment