Na Humphrey Shao
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleimani Kova, anatarajia kuingia studio kurekodi wimbo akishirikiana na msanii
Khamisi Ramadhani (H Baba).
Akizungumza na wadau wa sanaa katika Jukwaa la Sanaa jijini Dar es Salaam juzi, H.Baba alisema atawashirkisha viongozi wa juu kuimba ikiwa ni njia mojawapo ya kuelimisha jamii kupitia muziki.
Alisema katika wimbo huo atawashirikisha wasanii wenye majina makubwa katika fani hiyo, wakiwemo Ally Kiba,Tunda Man, Joti, Masanja na Mpoki.
"Kama ilifanikiwa kuwachangisha watu katika tamasha lililofanyika Uwanja wa Taifa kuwasaidia waathirika wa mabomu ya Gongolamboto, hata wimbo huu tutafanikiwa na kuwa mfano wa kuigwa wa viongozi wengine," alisema.
Msanii huyo alipata nafasi ya kutoa mada katika Jukwaa la Wasanii changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika fani yao, ikiwemo kuibwa kwa kazi zao.
Alisema kuwa, pamoja na wasanii nchini kuwa na majina makubwa, lakini hawana mafanikio kama ilivyo kwa wsanii wa nje ya nchi.
H Baba alisema kuwa, sababu kubwa ya kushindwa kupata mafanikio, mabli ya kuibwa kwa kazi zao, pia wasanii kukosa ushirikiano na kuwafanya wezi wa kazi zao kuwaibia kwa urahisi.
kamanda kova, nenda kaimbe kama nchi yetu inaongozwa na Msanii then hata watendaji watakuwa wasanii pia. Mathlani umekosa kazi za kufanya nenda kaimbe mashairi. Ningekuunga mkono kama ungefanya harambee kuliko kuuza sura kwenye tv eti upate hela za kusaidia waathirika wa mabomu ya gongo la mboto. Kwani lazima ufanye ubongo wa flave? Ndiyo maana mnaambiwa mnashirikiana na majambazi kwa hamjui nyadhifa na majukumu yenu katika jamii!!! Kauze sura baba!!!!!!
ReplyDeleteHii ni sawa na mjaluo kuimba taarabu,hiyo sauti ya kukwaruza na bongo freva wapi na wapi?anyway hata Museveni alitoa single,jaribu baba unaweza kuwa star
ReplyDelete