Na Grace Michael, Dodoma
MBUNGE wa Jimbo la Ubungo, Bw. John Mnyika ameijia juu serikali akiitaka kupunguza fedha katika Ofisi ya Rais zinazotengwa kwa ajili ya matumizi ya kitaifa ambazo
alisema kuwa hutumika kwa safari nyingi za rais ili zifanye kazi ya kupunguza umasikini wa wananchi.
Alisema kipindi cha Baba wa Taifa Hayati, Mwalimu Julius Nyerere, hakukuwa na safari nyingi za kitaifa kama zinazofanywa katika kipindi hiki.
Alisema kuwa safari hizo zinatumia mabilioni ya fedha za walipa kodi huku miradi ya maendeleo kwa ajili ya wananchi ikiachwa na fedha kidogo.
Kutokana na hali hiyo, alisema hawezi kuunga hoja bajeti ya Ofisi ya Rais mpaka atakapopewa maelezo ya kutosha kuhusu na matumizi ya fedha hizo katika bajeti ya mwaka jana na matumizi yaliyopangwa katika mwaka huu wa fedha.
Msimamo wa Bw. Mnyika ulijionesha wazi jana bungeni wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti na Utumishi wa umma iliyowasilishwa juzi na Waziri wake, Bi. Hawa Ghasia.
Alisema kuwa haiwezekani Ofisi ya Rais ikatengewa mabilioni ya fedha katika matumizi ya kawaida huku fedha kwa ajili ya maendeleo zikiwa kidogo.
“Kuna kasma ndogo ya matumizi ya Kitaifa ambayo imetengewa kiasi cha sh. bilioni 135 na fedha hizi hazina mchanganuo wowote...na hapa tunatakiwa kupitisha fedha hizi, sitakubali mpaka nipate maelezo ya kina kuhusu fedha za mwaka jana zimefanya nini na nichanganuliwe matumizi ya fedha hizi.
“Hizi fedha ndizo unakuta msafara mmoja wa Rais unatumia milioni 50 na msafara mwingine unatumia mpaka milioni 200, safari zimekuwa nyingi kupita kiasi, tofauti na kipindi cha baba wa Taifa ambaye ukisikia amekwenda Marekani ni kwa ajili ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa (UN), lakini hilo kwa sasa halipo safari ni nyingi kuzidi kipimo, fedha hizi zipunguzwe na ziwekwe kwenye miradi ya kuwaondolea wananchi umasikini,” alisema Bw. Mnyika.
Alikwenda mbali zaidi kwa kuonesha bajeti ya Zambia ambayo alisema kuwa fedha zinazotengwa kwa ajili ya Ofisi ya Rais zinakuwa na mchanganuo unaoonesha wazi kuwa rais atakwenda safari ngapi hivyo akataka maelezo zaidi katika fedha hizo zilizotengwa.
Bw. Mnyika ambaye kabla ya kuchangia chochote alimwomba Mwenyezi Mungu amlinde kwa atakayoyazungumza, ambapo mbali na hilo, aliziomba idara za Usalama wa Taifa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (PCCB) zitumike katika kuondoa kero za wananchi kwa kuwa miradi mbalimbali ikiwemo ya maji, ardhi imegubikwa na rushwa hali inayokwamisha maendeleo ya wananchi.
“Najua nikisema Usalama wa Taifa na TAKUKURU wasaidie haya, wapo watu wanaweza wakaulize hapo wanaingiaje, lakini niseme tu kwamba wanaingia kwa kuwa mnyororo mzima wa miradi imeghubikwa na rushwa hivyo watusaidie katika haya mambo,”
alisema Bw. Mnyika.
Akizungumzia uwajibikaji, alisema kuwa ili nchi iendelee ni lazima iwe na maono pamoja na maadili hivyo akasema kuwa ni lazima mazoea katika kazi naya kifisadi yaachwe na badala yake kila mmoja ajenge utamaduni wa uwajibikaji.
Kutokana na hali hiyo, alisema kuwa umefika wakati kwa Rais Jakaya Kikwete kuanza kusafisha Ikulu kwa kuwa wasaidizi wake wanamshauri vibaya hatua inayofikia kulidanganya Taifa.
“Ipo taarifa aliyotoa rais akisema kuwa ifikapo Julai kuna megawati 260 za umeme zitakuwa zimeingizwa na makali ya mgawo wa umeme yatapungua lakini mpaka sasa ambayo ni Julai makali ya mgawo yanazidi kuongezeka...na katika hili Waziri wa Nishati na Madini na Naibu wake wanatakiwa kujiuzulu huku Ofisi ya Rais nayo
inatakiwa kufanya maamuzi magumu,” alisema Bw. Mnyika.
Akizungumzia suala la mishahara kwa watumishi wa umma, alisema kuwa maelezo yaliyoko ndani ya hotuba ya waziri ni sawa na ahadi hewa hali iliyowafanya wananchi jimboni mwake kumtaka asiunge mkono hoja.
“Kinachojaribu kuoneshwa hapa kuwa nyongeza ni asilimia 40 lakini imehusisha mambo mengi na si mishahara peke yake hivyo waziri anatakiwa katika kuhitimisha aeleze ukweli wa hali halisi ya suala hili,” alisema Bw. Mnyika.
Alisema kuwa bajeti hiyo inahusu ofisi nyeti kuliko zote, kwa kuwa hata kwa mujibu wa katiba pamoja na kasoro zake, inaeleza wazi mamlaka makubwa ya rais na kiongozi mkubwa wa nchi lakini ni mwajiri na mwajiriwa mkuu, hivyo utumishi wote wa umma bila kujali Waziri Mkuu, mawaziri na watumishi wengine wanafanya kazi
kwa niaba ya ya Rais na tafsiri yake hapo ni kuwa upungufu wowote wa utekelezaji wa bajeti iliyopita anayetakiwa kuwajibika ni ofisi ya Rais.
Kutokana na hali hiyo, alitaka maelezo ya kutosha kutoka serikalini.
Great thinker always have a valiant mind like you! You are a hero bro, keep it up
ReplyDeleteNinajivunia kutoka jimbo la Ubungo..Je Mtanzania mwenzangu, jiulize kama mbunge wako anakusaidia wewe na Watanzania wengine??
ReplyDeleteKama hatusaidia japo kwa kusema ukweli na kuihoji serikali, basi 2015 haina haja ya kumchagua...
Pongezi kaka Mnyika, wapeleke mchakamchaka wazee wetu waliozoea kwenda bungeni kusaini form za posho..
Nasema, Watanzania wenzangu, hili liwe bunge la mwisho lenye wabunge mizigo kwetu..
Aluta kontinua..mapambano bado yanaendelea
facts za serikali ya Zambia ziko wazi wazi.Haya sasa kazi kwetu....
ReplyDeletekweli tukisema hoja iungwe mkono kwa style hiyo tutafika?kwangu me naona itakuwa haina tofauti na ile mikataba hewa,si ilipita hivyo hivyo.aah tumechoshwa bwana.big up Mnyika kwa kuona mbali.
pumba tupu
ReplyDeleteWamesha zoea wizi na posho kila kona unategemea wataweka mambo yao wazi?Ikulu inafanyiwa ukarabati kila mwaka sijui ni kitu gani kinacho jengwa kila mwaka tena kwa mabillioni ya pesa za walipa kodi.Na kwa maana nyingine ni kwamba hata hao wajenzi ni sawa na wajenzi wa kuokotwa mitaani.
ReplyDeleteIt is high time the government of Tanzania learnt to be transparent and patriotic. Apparently you 'bless' by your 'good' words but you 'curse' by actions. EPA, Rada,Richmond etc prove the case! Have you heard Mwai Kibaki going for a 'begging mission' abroad? Now I conclude that JK is still the Minister of foreign affairs. I agree with Museveni's speech in recent AU meeting, African presidents must stop adoring foreign aid. Utilize your local resources and terminate with immediate effects the so called UFISADI which lamentably has turned out to be a national anthem!
ReplyDeleteMh. Mnyika. Wewe ni kati ya wabunge vijana na wapya bungeni lakini hoja zako zimekwenda shule. Inaonesha wazi kuwa hauko bungeni kusubiri 'sitting allowance' na kupiga makofi. Unawakilisha siyo tu wananchi wa Ubungo bali watanzania wote wenye moyo wa uzalendo. Jipe moyo na endelea kumtegemea Mungu ktk vita dhidi ya ufisadi. Wewe pamoja na wabunge wote wenye uchungu na Tz bila kujali ushabiki wa vyama tupo pamoja nanyi. Tanzania ni nchi tajiri lakini uchumi wake unahujumiwa na wajanja wachache. Wake up Tanzanians, the time is now or never!
ReplyDeletekipindi cha kuweka mambo wazi na kiwe sasa.inabidi tuungane kwa pamoja nasi kuhoji kama walipa kodi na si kuwaacha wabunge peke yao wakimwanyumuka mjengoni.na kuwepo na katiba inayotuhusisha kama wananchi nasi kuchangia na kuwaondoa maadui wanaokwamisha maendeleo ya nchi tunapoona ndivyo sivyo ktk misingi ya kidemokrasia iliyo huru kama kwa wenzetu.maana unawezakukuta bado tupo kwenye ukoloni mamboleo kimya kimya.kama nyadhifa za juu zinajulikana hata kabla ya uchaguzi tena kukiwepo na usimamizi wa kimataifa?pia kuna mikataba mingi tu ya utata.hizo nazo zinaweza kuwa features za huo ukoloni. Nashukuru kuona sasa tunajitahidi kuamka,2010 mambo yalionekana kwenye ballot.sasa wazee huko nadhani 2015 wanaisubilia wakiwa na hofu.kwa style hii tutaondoa mmoja mmoja...kwa amani tu.
ReplyDelete