Na Mwandishi Wetu, Mbeya
BAADHI ya mashabiki wa burudani jijini hapa hususan wa muziki wa kizazi kipya, wamesema wanalisubiri kwa hamu Tamasha la Fiesta kama ilivyo kwa mikoa
mingine, licha ya hivi karibuni kupingwa na mwanasiasa mmoja jijini hapa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, mashabiki hao walisema wanashangazwa na mwasiasa huyo kutaka wakazi wa Mbeya kulisusia tamasha hilo ambalo limepangwa kufanyika wikiendi hii, bila ya sababu za msingi.
Hivi karibuni mwanasiasa huyo, alisema anajipanga kuhakikisha kwamba tamasha hilo halifanyika jijini Mbeya kwa kuwa wakazi wa Mbeya wanahitaji vitu vya maendeleo na burudani.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake aliyejitambulisha kwamba ni mdau wa muziki, Thobisa Mwangosi alisema burudani kwa vijana ni muhimu baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu hivyo ni vizuri angalau siku moja, wakapata nafasi ya kufuta machungu ya maisha kupitia muziki.
"Hapa tuacheni mambo ya siasa. Maana siasa katika nchi hii imeharibu mambo mengi mno. Najua wapo watu wanaojaribu kutumia vyeo vyao kuharibu mfumo mzima wa Fiesta, ila wale wenye akili lazima tuwe wakali na
kupambana na watu hao.
"Kwa kweli kama siasa zitaingia katika mambo ya burudani itakuwa ni hatari sana, mtu kama ana hoja zake, anatakiwa azipeleke bungeni kwa kuwa hii inaonesha kwamba kuna kitu kati ya waandaaji na mwanasiasa huyo," alisema Mwangosi.
Alisema wao kama wapenzi wa burudani wanalisubiri kwa hamu tamasha hilo la Fiesta kwa kuwa tayari wameshajiandaa, kikamilifu kwani hiyo ni siku yao maalumu kwa wao kutoka.
Mwangosi alisema watu wanaolipinga tamasha hilo hawalitakii mema taifa, wanataka kurudisha maendeleo ya vijana nyuma kwa kuwa wengi wao kwa sasa wamejiari kupitia sekta hiyo ya muziki.
Alisema kwa upande wake, anaweza kusema mwanasiasa yeyote awaachie burudani zao ili wasahau kero zao angalau kwa siku moja, maana vichwa vyao vinawaza mambo mengi hadi kufikia kupasuka.
Fiesta inadhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Shirika la Ndege la Precision Air na GAPCO.
mbunge ana mamlaka ya kukataza au kupiga marufuku kitu chochote kisifanyike ktk jimbo lake bila kuhusisha baraza la madiwani? nisaidieni kwa hili coz mi mpaka sasa huwa naskia mkurugenzi tu ndo huwa anaruhusu au anakataza
ReplyDeleteMie naona mbunge yuko sahihi hasa katika zama hizi za UKIMWI, kuna mtu anaweza kuniambia huko ilikopia hiyo fiesta wamefaidika na nini? Kwani Mbeya hakuna burudani mpaka fiesta ije? Kama watu hawajui ni kwamba wanao faidika na shughuli hiyo siyo watu wa mbeya bali ni wamiliki wa kazi hiyo na watutumishi wao ambao wanaolipwa posho za kujikimu wakiwa safarini lakini wasanii wanokuja kuvuja jasho jukwaani waulize wanalipwa kiasi gani utashangaa!
ReplyDeletembunge mwenyewe nae ni msanii ktk fani hiyo hiyo ya muziki
ReplyDeleteFiesta haina maana zaidi inaongeza kasi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI
ReplyDelete