08 July 2011

Mafunzo yafungiwa mwaka mmoja

Na Mwajuma Juma, Zanzibar

TIMU ya netiboli ya Mafunzo ya wanawake imefungiwa kwa muda wa mwaka mmoja kucheza mechi ndani na nje ya nchi kwa kitendo cha kumpiga mwamuzi
Hadia Ahmada ilipocheza na JKU.

Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Ufundi na Nidhamu ya Chama cha
Netiboli Zanzibar (CHANEZA), kupitia barua yake ya Julai 5, mwaka huu, na kusainiwa na Katibu wa kamati hiyo, Restuta Lazaro.

Kwa mujibu wa barua hiyo imeeleza kwamba, wachezaji wa timu hiyo
na kocha wao, Tatu Rashid, walimshambulia mwamuzi huyo mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

Katibu wa kamati hiyo alisema kuwa,  pamoja na kutoa adhabu kwa timu
hiyo, pia wamefutiwa matokeo yote ya michezo waliyocheza katika ligi
hiyo inayoendelea mjini  Zanzibar.

"Tumeifungia timu na kocha wao kucheza mechi ndani na nje ya nchi,
pia tumewafutia matokeo yote ya uwanjani katika ligi hii," alisema Restuta.

Hata hivyo, alisema kuwa haki ya rufani imetolewa kwa upande ambao
utaona haukuridhika na adhabu hiyo.

Katika mchezo huo ambao ulichezwa Julai 4, mwaka huu, Mafunzo
ilifungwa mabao 44-35, mchezo ambao ulichezwa saa 10:30 za
jioni katika Uwanja wa Gymkhanah.

No comments:

Post a Comment