01 August 2011

Lampard kuwekwa benchi na Wilshere

LONDON, Uingeza

MUDA wa Frank Lampard kuendelea kudumu katika kikosi cha kwanza cha England,  umekwisha.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 ambaye ni nyota wa Chelsea, ameichezea timu ya England mechi 86, anaweza kuitwa kwenye timu ya taifa kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Uholanzi Agosti 10.


Gazeti la Mail la jana lilisema kwamba,  kama itatokea Jack Wilshere au Scott Parker kuumia, ndipo kunaweza kumfanya Lampard kuanza kucheza katika kikosi cha kwanza cha England.

Ingawa Kocha wa England, Fabio Capello, ataendelea kumwita Lampard, Mtaliano huyo anahisi kuwa, mkiungo huyo ameshindwa kuonesha matunda, huku Wilshere mwenye miaka 19, akionekana kuwa mzuri zaidi katika nafasi ya kiungo kwenye kikosi cha England.

Licha ya kukosekana kwa Steven Gerrard kutokana na maumivu ya korodani, Lampard anaweza kuanzia katika benchi katika mechi dhidi ya Uholanzi.

Kwa miaka minne, makocha wa England wamakuwa wakiumiza kichwa jinsi ya kuwachezesha Lampard na nyota wa Liverpool, Gerrard katika sehemu ya kiungo.

Lakini, sasa hatima ya mchezaji huyo wa England iko kwenye hatihati, baada ya mchezaji wa Arsenal, Wilshere, aliyeichezea timu ya taifa mechi tano kuonekana mzuri.

Hata Parker,  kama alivyo Lampard, naye anaonekana kucheza vizuri zaidi akiwa na kijana kwa kuweza kuwasaidia washambuliaji.

Lampard alitolewa licha ya kuifungua bao England katika mechi dhidi ya Uswisi.

kwa siku hiyo, nafasi yake ilichukuliwa na Ashley Young, ambaye naye anaonekana kuwa mchezaji muhimu zaidi kwa England katika kuhakikisha inafanikiwa katika michuano ya  Euro 2012 .

No comments:

Post a Comment