01 August 2011

Vodacom yaipa muonekano mpya M pesa

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Mawasiliano ya Vodacom imezindua muonekano mpya katika huduma yuke ya M pesa ili kuendana na kauli mbiu 'Kazi ni kwako'


Huduma ambayo kwa sasa itahusishwa na Superman ikiwa ni ishara ya kuonesha uwezo ubora wa huduma imekuwa ni  ukombozi katika kubadili maisha ya mamilioni ya Watanzania mjini na vijijini kwa kuleta ufanisi wa kifedha kupitia simu ya mkononi.  


Akizungumuza katika uzinduzi huo Ofisa Masoko wa Kampuni hiyo,Bi. Mwavita Makamba alisema kuwa vodacom kupitia huduma hiyo inazungumzia kubadili maisha ya watu kwa kutumia mtandao madhubuti wa kielektroniki unaoendesha huduma hiyo.
 
"Superman ni kielelezo maarufu duniani ikiwa ni ujasiri, uhodari kasi na usalama kitatumika kama kitambulisho sokoni," alisema Bi. Makamaba.

Alisema kupitia huduma hiyo hakuana sababua ya nmaru kaupanga foleni ama kusafiri umablia mrefu kwa ajili ya kufanya malipo ama kutuma na kupokea fedha katika akaunti ya m-pesa kwnye simu ya mkononi kupitia vituo vya mawakala zaidi ya elfu tisa.

"Wakati mfanya biashara wa anapowaza usalama wa kuhifadhi fedha zake na njia ya rahisi ya kuzipata pindi anapozihitaji mpesa humpatia suluhisho kama ilivyo kwa wanafunzi ambao kwa sasa kupitia mpesa wanalipa gharama ya mikopo kwenye Bodi ya Elimu ya Juu bila usumbufu huku kwa ujumla jamii ikiendelea kufurahia njia rahisi zaidi ya kutuma kuhifadhi na kupokea pesa," alisema Bi Makamba.  

No comments:

Post a Comment