22 November 2011

Moto wa Katiba Mpya CHADEMA kutinga Ikulu

*KAMATI Kuu yateua kamati ndogo ya muafaka
*Maandamano yawekwa kiporo kusubiri suluhu
*Mbowe: Hotuba ya rais imetusikitisha sana
*Wanaharakati Dar kutoa msimamo mzito leo


Na Benjamin Masese
Mwenyekiti wa Chadema Bw. Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu tamko la Chama hicho kutaka kuonana na Rais Jakaya Kikwete kumweleza msimamo wa kupinga rasimu ya katiba.

SIKU tatu baada ya Bunge la Tanzania kupitisha muswada wa Sheria ya kuundwa Tume ya Kukusanya maoni kuhusu
Katiba Mpya, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kusitisha maandaano ya nchi nzima kuupinga kama ilivyoeleza awali.

Badala yake chama hicho kimetangaza nia ya kutaka kuonana na Rais Jakaya Kikwete, ana kwa ana kujadili suala hilo kwa njia ya mazungumzo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CHADEMA Bw.Freeman Mbowe, alisema baada ya Kamati Kuu ya chama hicho kujdili suala hilo kwa undani wameazimia kuunda kamati ndogo itakayokutana na Rais Kikwete kushauriana ili kufikia muafaka.

"Kamati Kuu imekaa na kushauriana na kupendekezwa kuundwa kwa kamati ndogo ambayo itakutakuna na Rais Jakaya Kikwete, kushauriana na kuwasilisha mapendekezo yao ili kuafikiana kabla ya kuchukua uamuzi kwenda kwa wananchi na wanaharakati,"alisema Bw. Mbowe.

Majina ya wajumbe

Aliwataja wajumbe wa kamati hiyo kuwa ni yeye mwenyewe, Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Willibroad Slaa, Makamu Mwenyekiti Tanzania Visiwani Bw. Issa Ali Mohamed, Mbunge wa Mpanda Bw. Said Arfi, Profesa Abdala Kapala na Profesa Mwesiga Baregu.

Bw. Mbowe alisema tayari kamati hiyo ilianza kufanya mchakato wa kuonana na Rais Kikwete jana na kwamba iwapo hawatasikilizwa au kupokea ushauri na msimamo kwa kujadiliana wanaturudi mezani na kuamua rasmi kwenda kwa wananchi kueneza kile alichokiita kuwa ni sumu ya kupinga muswada huo.

Akizungumzia hotuba ya Rais Kikwete aliyoitoa mwishoni mwa wiki kupitia  wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Mbowe alisema hawakubaliani na kauli kwamba CHADEMA iliahidi Katiba Mpya kwa siku 100.

"Chadema tunasikitika kuona rais na wabunge wanaendelea kupotosha umma katika suala hili. Tulisema kwamba tutaanzisha mchakato wa katiba mpya kabla ya siku 100 huu ndio usahihi.

"Suala la katiba mpya limetekwa na baadhi ya wanasiasa ambao hawajui ni fursa ya kila mtanzania, wapo wengine wanaona chadema inapinga kuwepo kwa katiba mpya, sisi tunahitaji sana na tunachokitaka wananchi washirikishwe na waamue wenyewe,"alisema Bw.Mbowe.

Alisema chama chake kimekipongeza chama cha NCCR Mageuzi kuungana nao kwa kutoka nje ya ukumbi wa bunge kwa lengo la kupinga muswada wa Katiba Mpya huku akikiponda Chama cha Wananchi (CUF) na vingine ambavyo vilishiriki mjadala huo bungeni.

CHADEMA na Polisi

Katika hatua nyingine CHADEMA imetoa mwito kwa Jeshi la Polisi kuondoa pingamizi la kufanya maandanao na mikutano ya kisiasa mara moja kwa madai kuwa kufanya hivyo ni sawa na kuvinyika haki ya msingi vyama pamoja na wananchi kwa ujumla.

Bw. Mbowe alisema baada ya taarifa kutolewa na Jeshi la polisi walitii agizo hilo lakini wamestushwa na kauli ya Rais Kikwete kuwaagiza wabunge wa CCM kufika kwenye majimbo yao na kuzungumza na wananchi juu ya muswada wa Katiba Mpya.

Alidai iwapo wabunge watafanya mikutano na wananchi watakuwa wameanzisha ligi ya mikutano na maandamano na kuliomba jeshi la polisi kuondoa pingamizi hilo.
       
 Sakata la Jairo           

Akizungumzia suala la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. David Jairo, ambaye bunge liliazimia kuchukuliwa hatua Bw. Mbowe alisema msimamo wa chadema uko pale pale kama wabunge walivyopendekeza bungeni.

Alisema hakuna sababu yoyote ya Bw. Jairo, Waziri wa wizara hiyo Bw.  William Ngeleja, Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Philemon Luhanjo, pamoja na watumishi wengine kuendelea kuwa watumishi wa umma na kwamba msimao wa CHADEMA ni kuona wakifukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani.

Alisema hatua zisipochukuliwa mapema kabla ya bunge kuirejea Januari 31, mwakani hapatatosha kutokana na kile alichodai kuwa ni uzembe huku kukiwa na ushahidi wa ubadhirifu huo kufanywa kwa makusudi.

Kwa upande wake Dkt. Slaa pamoja na Mbunge wa Singida Mashariki Bw. Tindu Lissu, walikituhumu CCM kwa maelezo kuwa kimetumia 'ujangili' kupitisha muswada wa katiba mpya usio na maslahi kwa wananchi.

Wakati huohuo wanaharakati mbalimbali wanatarajia kutoa tamko zito kuhusu Muswada huo leo Jijini Dar es Salaam huku kukiwa na taarifa kuwa kulikuwa na vikao vya hapa na pale vya jumuiya hizo chini ya Jukwa la Katiba tangu Ijumaa wiki iliyopita.

"Tutatoa tamko letu kesho (leo) ili wananchi watuelewe na wajue wazi msimamo wetu baada ya Bunge kupitisha Muswada wa Sheria ya Kuundwa ya Katiba Mpya,"alisema mmoja wa mwanarakati ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa kuwa si msemaji rasmi wa kundi hilo.

Awali katika mdahalo wao Jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, Jukwa la Katiba walitishia kuhamasisha wananchi kufanya maandamano ya nchi nzima yasiyokuwa na kikomo kupinga muswada huo kwa madai kuwa ulipaswa kusomwa mara ya kwanza bungeni na sio mara ya pili.

28 comments:

  1. KATIBA INAMRUHUSU RAIS KUUNDA TUME YA KUZUNGUKA NCHI NZIMA KUPATA MAONI YA WANANCHI,HATA KAMA RAIS HUYO ANGEKUWA NI SLAA.SASA NYIE CHADEMA MNACHOTAKA NI NINI ? KWA URASIMU MNAOUTAKA ITATUCHUKUA MIAKA 100 KUPATA KATIBA MPYA.

    ReplyDelete
  2. Hayo ni maoni yako kama mtanzania lakini nashindwa kukutambua kiukweli kama wewe ni mtanzania wa kizazi gani.

    Nimesema hivyo kwasababu,hauoni utofauti kati ya kamati inayoundwa na wananchi inayoundwa na rais tena mwenyekiti wa chama caha CCM.

    Kama umeamua kuunda katiba mpya basi kuna haja naye awe serious kwa kufanya transparency ya mchakato huo.

    Kama wewe ni mtu makini,angalia kamati na sekretariate yake iundwe na rais,huyo ndio aunde bunge la katiba,tume yake ndiyo isimamie uchaguzi wa kura za maoni kwa wananchi na kutoa matokeo,UNAWEZA KUPATA PICHA NI KATIBA ya namna gani itakayoundwa.

    Hivyo basi CHADEMA tayari hili wameshaliona ndio maana wanajitahidi kutengeneza mazingira ya kuwa wazi kwa wananchi ili mwisho siku katiba iwe kwa waslahi ya wananchi sio kwa maslahi ya chama fulani ie.CCM ili kiendelee kuwa madarakani.

    Sasa sijui hualiona hili? kama umeshaliona utata wa nini kuona chama makini kinatafuta muafaka kwa njia ya amani.

    Gwa Ntegeye
    Kigoma

    ReplyDelete
  3. NAona hata shule yake ni ndogo ( mchangiaji wa kwanza hapo juu) hajui kutofautisha kati ya katiba itakayoundwa kwa kushirikisha wananchi na ile itakayokuwa ya Chama Cha Majambazi(CCM), nasema hivyo kwa 7bu coni dhamira ya dhati ktk kupata katiba mpya toka kwa utawala wa kibabaishaji uliojaa udugu, urafiki na ushemeji na kufanya nchi kuwa hobela hobela.

    ReplyDelete
  4. wananchi tusiwe wajinga tuwasaport watu wanaotutetea hii nchi kwa sasa aieleweki

    ReplyDelete
  5. Tunapotoa mawazo tujue kuwa kila mtoa mawazo ana akili timamu.Lakini kuna watu wanaodhani kuwa ukipingana na chadema basi wewe ni mjinga.Huo sasa ndiyo ujinga mkubwa zaidi.

    ReplyDelete
  6. Huyo ndipo uwezo wake ulipofikia tumvumilie kwa vile hatujui lengo lake nini. Hamna haja ya kutunga katiba mpya iwapo machinery ni hiyo hiyo. Tuliruhusu mwaka 1977 matokeo yake tukayaona, vile vile mara mbili miaka ya tisini. Basi hiyo iitwe kamati ya Rais na sio ya WANANCHI na kama NI WANANCHI tushirikishwe ipasavyo kuanzia chini ndio tunajua uchungu wa katiba hii mbovu. Kingine hatutaki Wazanzibar watuwakirishe kwa mambo ambayo sio ya muungano mbona sisi hawakutushirisha kwa yao. Tunaomba Rais acha jaziba jenga jina lako kwani unaogopa nini? Huwezi kuilinda CCM daima na ufisadi hauwezi kuisha CCM

    ReplyDelete
  7. Mchangiaji wa kwanza sio mtu makini au ana maslahi na huu mfumo mbovu wa wachache kuamua hatima ya maisha ya wengi.SELFISH.

    ReplyDelete
  8. Mchangiaji wa tano umeongea kitu ambacho watu wengi hawakitaki. Ni kweli wachangiaji wengi hasa wa CDM hawaheshimu mawazo ya watu wengine kitu ambacho ni hatari. Kwani uhuru wa kujieleza ni suala zuri sana.

    Tukirudi katika mada, CHADEMA kwa mtazamo wangu wamekosea. Kwani wameshindwa kuchangia mambo yao ambayo yengekuwa na umuhimu mkubwa bungeni ambapo na wananchi wengeweza kupata kusikia nini walichochangia badala yake wamesusa sasa wanataka kwenda kuchangia kwa Rais hiki ni kichekesho cha aina yake.

    Ukitaka kwenda peponi lazima ufe. tukumbuke kura za maoni za uanzishaji wa vyama vingi asilimia 80 zilikataa vyama vingi lakini bado ile tume ilishauri serikali ianzishe mfumo wa vyama vingi. Kwa hiyo tusiogope Rais kuteuwa mbona alivyomteua Zitto kwenye kamati ya Madini awakusema amekosea? Tunapaswa tukatoe maoni yetu kwenye kamati ndilo la msingi.

    Hao wanaharakati wenyewe wa Tanzania njaa tu nao kwani wakipata nafasi hautawasikia tena. Huu ni mtazamo wangu Msinitoea macho

    ReplyDelete
  9. Ndugu yangu acha kufikiri kwenye Box, mchakato ndio katiba yenyewe sasa ukikubali hapa huwezi kurudi nyuma mbele. Katiba tunayoitaka kwa mfumo huo wa Rais ni mbovu. Kumbuka muswada unataja Rais (wa Muungano) na kushirikiana na Rais wa Zanzibar, hawa ni watu na sio taasisi (Urais), hawa sio malaika na sio miungu, wana madhaifu, wanahisia na kikubwa wana maslahi pia kwenye swala hili. Kwanini tusitafute njia ambayo Rais hawezikuwa na mamlaka makubwa kiasi hiki? Tafakari

    ReplyDelete
  10. Baadhi ya mawazo ya watanzania yanatisha. Katiba wanayoitaka CCM itatamka eti, Rais, awe wa CCM, Chadema,CUF au NCCR, ateuwe Kamati ya Kukusanya maoni ya kuandika Katiba yenyewe! Kabla ya Kwenda mbali, ndicho kilicho fanyika kabla ya muswada huo kusomwa kwa mara ya pili. Anna Makinda, sijui kama alielekezwa na Mtukufu Rais, ila aliteua wajumbe ambao walitakiwa kwenda katika majimbo 10 katika Jamhuri ya Muungano. Waliishia wapi ndugu zangu? Je Spika hakuwakataza kutekeleza majukumu yao? Sasa hapo tusemeje? Mbaya zaidi inasemekana wajumbe wa kamati hiyo, yuko mzee Vijisenti! Nadhani kuendelea kufafanua swala hili ni kujiongezea maji machungu tu mwilini mwangu. Badala yake tutafakari na kuunga mkono hatua njema za Chadema zenye mshiko. Kinachotisha zaidi nipale Watawala hawaoni kuwa kimbunga cha mabadiliko yanatokea dunia nzima. Mfano, je nani angedhani Al-Bashiri ya Syria angebanwa kiasi kile? Au jana tu Majemadari wa Misri wamejikuta wanapambana na wananchi waliochoshwa na mfumo mbovu? Sio Gadafi tu keshaondolewa. Hivi sote tunataka hayo yatokee? Mimi nadhani Katiba mpya tuitakayo tutaipata. Hofu yangu ni kuwa ni kwa garama gani? Mpira uko katika uwanja wa Serikali na CCM. Tuombe watumie busara na si hasira!

    ReplyDelete
  11. Ndugu zangu hakuna mtu ambaye hataki katiba mpya. Suala lililokuwepo mezani ni kukusanya maoni. Ukitaka kujua kusema ni mbali na kutenda hiyo kamati ya CDM iliyoteuliwa aina hata mwanamke mmoja je unafikiri kweli wanaweza kuitendea katiba vizuri ikiwa wao wenyewe wameshindwa hata kumtupia mwanamke mmoja ina maana wanawake wa CDM hakuna mwenye sifa?

    Mwenyekiti na katibu wote wawepo kwenye hiyo kamati ni kituko kingine hiki.

    ReplyDelete
  12. Nadhani mchangiaji wa kwanza ni Jaji Warema

    ReplyDelete
  13. Nawasapoti Chadema kwa asilimia 100.Nyie ndo watetezi pekee wa wanyonge mliobaki Tanzania.Huyo mtu wa kwanza kuchangia anaonekana ni mshirika wa mafisadi,na fikra zake ni za kibabe kama za CCM.CCM lazima watambue kwa sasa watanzania tume elimika na tunajua kutofautisha mazuri na mabaya.Hatudanganyiki kirahisi kwa sasa.Chadema nawahakikishia mko pamoja nasi sisi wa familia za wanyonge ambao tumeshaelimika na tuna uwezo kama hao mafisadi(wezi wa mali ya umma)

    ReplyDelete
  14. sheria inayoruhusu 'mwinyi' kuteua tume ni lazima hiyo tume itakua 'royal' kwake na kama ni hivyo haiwezi kua 'holistic' ktk kukusanya maoni kwani tayari 'bwana wao' anayomambo anayoyataka na ameshataja kwenye sheria hiyo!!! watanzania wenzangu, kazi ya 'kuratibu' ukusanywaji maoni na'kuratibu' maoni kuna-implications pale...kuratibu ni kuchukua mawazo wao wanayoona ni ya msingi, off course, hatakama hayaleti tija bali kuendeleza 'ubwana wa mhisaniwao'...hayo nayo yatakua ni maoni kwani wapo watakaotoa!!! katiba ya wananchi iweje tume, hadidu za rejea n.k afanye rais!!???..kwanini kamati isiundwe na bunge kupendekeza mfumo halafu bunge lithibitishe baada ya kujadili kwa kina! hayo yatakua ya wananchi sasa kwa kupitia uwakilishi. ndugu zangu watanzania mnaohangaika kutafuta haki, HII SHERIA IME TUMULIKA MCHANA, KATIBA ITAUCHOMA!!!! Chadema watusaidie kwa kweli, wamuone yule 'bwana' wamueleze na watuletee mrejesho!!

    ReplyDelete
  15. hapa nivema raisi akapokea mawazo ya kila upande,ya waliotoka bungeni nawaliobaki bungeni yote hayo ni mawazo.yafanyiwe kazi.Hata waliopo upinzani walikuwepo katika tawala za chama kimoja,sio jambo la ajabu katika democrasia.Ina maana hata leo hii ridhiwani akijiunga na upinzani hana kosa ni haki yake,heshimu hata neno dogo la masikini katika mjadala huu,maana ndo uhai wa taifa siyo wa ccm wala cuf au chadema.Vyama vitapita ila taifa litakuwepo daima..

    ReplyDelete
  16. Watanzania!!. Ama kweli bado kuna kazi kubwa na safari ndefu.
    Siasa za zidumu fikra za mwenyekiti bado zinatutafuna. Mawazo haya ambayo yanadumaza uwezo wa kufikili ndiyo yanaisumbua jamii hii ya Kitanzania.
    Tatizo letu Watanzania, tunafikili tunajua mambo wakati tunaendelea kuwa bingwa wa copy & paste. hata ukitembelea blog nyingi zote zinafanya hivyo hivyo. Magazeti yanaandika habari hata bila ya uchunguzi sanifu. Wanasiasa wanakuja na kikra za ajabu na wananchi wanawaunga mkono bila hata ya kuelewa na kuwa na ulizo.
    Kwa akili hii ya Copy & paste ndiyo maana unasikia watu wanakubaliana na jambo furani hata kama hawajalifanyia uchunguzi wao wenyewe kama ni kweli kwa vile tu mtu furani ''Mwenyekiti'' amelisema(fikra za mwenyekiti).
    Kwa mtaji huu kwa sasa tuna jamii ambayo haijui nini inakitaka na hii inatokana na kutojua nini ilichonacho.
    Kwa sasa watu wengi wanatolea mfano matukio yanayotokea mashariki ya mbali na kulinganisha na Tanzania bila hata ya kufanya uchunguzi wa kina katika maswala ya kihistoria, kisiasa, kiuchumi na mashinikizo ya nje. Hii kwangu ni kama vile copy & paste.
    Ukosefu wa kifikra ni umaskini mkubwa ambao kama hatutafanya juhudi za kuuondoa, tutabakia kuwa nyuma.
    Tanzania ya sasa kila mtu ni mwana siasa bila siasa.

    ReplyDelete
  17. Kazaneni ili mkifika ikulu mkagawane kama mlivyogawana UBUNGE. Watanzania angalieni wanasogea HAO. Mkifanya mchezo watafika nahapo kilamahali mtaona masawe, nkya,lema, mongi,olomi, lymo n.k nawengine wa pependi katika jahazi hilo watavuta wa kwao mtabaki ahaaaaaa

    ReplyDelete
  18. TUSILALAMIKE! TUEPUKE MALUMBANO, TUSIOGOPE! TUJADILI,TUVUMILIANE! TUKUBALI/KUKATAA KWA HOJA NA TUTOE MUELEKEO!

    "MAENDELEO HUJA KUTOKANA NA MGONGANO WA MAWAZO NA HATIMAYE KUCHAGUA KILICHO BORA"

    NB: HATUWEZI KUFIKIRI SAWA!

    ReplyDelete
  19. Mchangiaji wa tano umeongea kitu ambacho watu wengi hawakitaki. Ni kweli wachangiaji wengi hasa wa CDM hawaheshimu mawazo ya watu wengine kitu ambacho ni hatari. Kwani uhuru wa kujieleza ni suala zuri sana.

    Tukirudi katika mada, CHADEMA kwa mtazamo wangu wamekosea. Kwani wameshindwa kuchangia mambo yao ambayo yengekuwa na umuhimu mkubwa bungeni ambapo na wananchi wengeweza kupata kusikia nini walichochangia badala yake wamesusa sasa wanataka kwenda kuchangia kwa Rais hiki ni kichekesho cha aina yake.

    Ukitaka kwenda peponi lazima ufe. tukumbuke kura za maoni za uanzishaji wa vyama vingi asilimia 80 zilikataa vyama vingi lakini bado ile tume ilishauri serikali ianzishe mfumo wa vyama vingi. Kwa hiyo tusiogope Rais kuteuwa mbona alivyomteua Zitto kwenye kamati ya Madini awakusema amekosea? Tunapaswa tukatoe maoni yetu kwenye kamati ndilo la msingi.

    Hao wanaharakati wenyewe wa Tanzania njaa tu nao kwani wakipata nafasi hautawasikia tena

    ReplyDelete
  20. Ndugu zangu hakuna mtu ambaye hataki katiba mpya. Suala lililokuwepo mezani ni kukusanya maoni. Ukitaka kujua kusema ni mbali na kutenda hiyo kamati ya CDM iliyoteuliwa aina hata mwanamke mmoja je unafikiri kweli wanaweza kuitendea katiba vizuri ikiwa wao wenyewe wameshindwa hata kumtupia mwanamke mmoja ina maana wanawake wa CDM hakuna mwenye sifa?

    Mwenyekiti na katibu wote wawepo kwenye hiyo kamati ni kituko kingine hiki

    ReplyDelete
  21. Tunapotoa mawazo tujue kuwa kila mtoa mawazo ana akili timamu.Lakini kuna watu wanaodhani kuwa ukipingana na chadema basi wewe ni mjinga.Huo sasa ndiyo ujinga mkubwa zaidi.

    ReplyDelete
  22. Mlengo wa CDM wa mpinzani-mpinzani-mbabe-haambiliki,ni sawa na mla nyama-ya-mtu Misri,Syria unawatafuna prejudice tupu.we're not at zero.Rais anapewa madaraka makubwa?NI SAWA KWA SABABU KACHAGULIWA NA WENGI.wivu wa mke mwenza na nchi ya ahadi,mtaharibu tz km misiri!

    ReplyDelete
  23. Tunataka katiba ya nchi na si ya CCM kama kuna watu wana wasiwasi na mchakato wa awali ni bora wakasikilizwa ! Nchi hii ni wote kama Wabunge walikuwa na nia njema kwa nini walipeleka haraka haraka katiba si mahari !Kuna wabunge wa CCM waliongopa kwama eti walipita kwa wananachi !Uongo mtupu! Hatima ya watanzania iko juu yao wote !Rais ni binadamu ana utashi, anaweza kupendelea,anaweza kuwa na chuki,anaweza kuwa muungwana, anaweza kuwa na upendo,anaweza kuwa mzalendo, anaweza kuwa dikteta,anaweza kufanya chochote cha kumfurahisha na kuudhi wengine kama ambavyo baadhi ya teuzi zake zinavyoacha maswali mengi,kwani wanaogopa ni nini? Leteni katiba kwa wananchi!

    ReplyDelete
  24. kwanza ninashukuru wote mliochangia hoja hii, lakini ni muhimu kama watanzania tujaribu kutumia akili zetu wenyewe kabla ya kutumia akili za wanasiasa tena wanasiasa wabinafsi.Nchi yetu inaongozwa na katiba na sheria zake,katiba hii ndiyo uliyotumiwa wakati wa uchaguzi na katiba hii ndiyo ile ile inayompa mamlaka Rais kuunda tume ya kukusanya maoni kama inavyompa mamlaka ya kuunda tume ya uchaguzi. kama kweli wanasiasa hasa CHADEMA wanasema kweli basi wasingeshiriki uchaguzi hadi ipatikane tume huru ambayo labda wajumbe wake hawateuliwi na rais.Pili kama wangetaka Rais asiunde tume bas ilitakiwa katiba iliyopo sasa ifanyiwe marekebisho katika vifungu vinavyompa mamlaka Rais ya kuunda tume ili sasa tume hiyo iundwe kutokana na namna wao wanavyotaka, lakini kwa sasa huo unaofanywa ni uzushi wa kuwadanganya watanzania ambao wengi ni mbumbumbu wa mambo na wasiotaka kutafakari mambo badala yake wanafuata mkumbo wa wanasiasa uchwara na wabinafsi.Mwisho katika kuunda kambi ya upinzani bungeni Chadema walitumia kanuni na sheria zinazotokana na katiba hiyo hiyo kuvibagua vyama vingine vya siasa wakisema katiba inawaruhusu wao kuuunda kambi ya upinzani bungeni kwa sababu wanao wabunge wa kutosha kwa mujibu wa kanuni na sheria, vipi leo watake Rais avunje katiba na sheria zilizopo kwa ajili yao? nasema CHADEMA ni matapeli wa kisiasa hawana hoja. Bungeni wamekimbia leo wanataka kuonana na Rais wamechoka sanaaaaaa

    ReplyDelete
  25. RAIS WANGU MPENDWA CHUNGA HAO MAFIA UNAPOKUTANA NAO ALIKA VIONGOZI WA DINI WASHUHUDIE MAZUNGUMZO YENU KWA SABABU UKIKUTANA NAO PEKE YAKO HAO JAMAA WAKITOKA NJE TU WANABADILI MANENO NA WATAKUZULIA MAMBO AMBAYO HAMJAYAZUNGUMZA,CHUNGA SANA HAO HASA HUYO MWENYE MIWANI HAPO JUU ANAYOFICHA MACHO YAKE. HAO WANATAKA IKULU KWA UDI NA UVUMBA. HAMNA TATIZO KATIKA MCKATO WA KATIBA KWA SABABU WANANCHI NDIO WATAKAOSEMA WANATAKA NINI ILA KINACHOTAFUTWA HAPO NANI KIDEDEA KATIKA KULETA KATIBA MPYA NCHINI JAMBO AMBALO NI UPUUZI WA WANASIASA. HATA HAO WANAHARAKATI WAMEJAA WACHAGA WATUPU NA MAANDAMANO HAYO YANAFANYWA KWA NIABA YA CHADEMA. MLAANIWE NA UKABILA WENU. MAJIRA BRAVOOOO MAANA TUNALIANDIKA NI PAPO KWA HAPO LAKINI MWANANCHI ANACHAGUA ANAYEPONDA CCM HUANNDIKWA HARAKA NA ADMINISTRATOR LAKINI UKIWAPA UKWELI HAWA JAMAA MAONI YAKO HAYATOKI

    ReplyDelete
  26. wastarabu na wenyehekima hawa bishi au kukubali jambo lolote bila kutafakari kwakina juu ya matokeo ya jambo lililo mbele yao. NDUGU YANGU MTZ MWENZANGU UMEWAHI KUJIULIZA NI KWANINI HILI SWALA LAKATIBA LIWE CHANZO CHA MVUTANO KATI YA WANA SIASA WA CCM NA CDM NA SII WANANCHI NA WANASIASA YAANI WATAWALA NA WATAWALIWA? tafakari!

    ReplyDelete
  27. SI KWELI KATI YA WATAWALA NA WATAWALIWA BALI NI KATI YA WANASIASA KWA WANASIASA AMBAO WANAWATUMIA WAJINGA WAO ILI WAONEKANE VIDEDEA KWENYE SUALA LA KATIBA MPYA. HAPO TATIZO LIKO WAPI? KINACHOTAKIWA NI WANANCHI WANATAKA NINI. CHAMA TAWALA NA SERIKALI YAKE IMEELEZA JINSI GANI WANANCHI WATAKAVYOTOA MAONI YAO NA CHADEMA WANATAKA WANAVYOTAKA WAO WANANCHI WASHIRIKISHWA,SASA HUU NI MVUTANO WAO WA KIJINGA HAPO WANANCHI WAMESEMA NINI? WAO WANABURUZWA TU NA WANASIASA.HAO WANAHARAKATI KAMA WANAVYOJIITA KAMA HAO KINA NKYA,SIJUI BARIKIELI,ELIOFOO KAWATIZAMENI MAISHA YAO YA KILA SIKU YALIVYO NA RAHA NA WANAISHI BILA SHIDA YOYOTE HAWA WANAPATA MISAADA KUTOKA ULAYA KISHA WANAGAWANA NA KUNUA MAGARI YA KIFAHARI NA KUJIJENGEA MAHEKALU SASA UPAYUKAJI WAO NI KUWAONYESHA WAZUNGU KUWA WANAFANYA KAZI KWELIKWELI ILI MISAADA IJE ZAIDI. HIZI NGO ZOTE NI ULAJI TU NA WEWE MWANANCHI UNATUMIKA KAMA MGONGO WA KUKUPANDIA WAFIKIE MALENGO YAO YA KIMAISHA.CHUNGA SANA WEWE MWANANCHI. KATIBA NI YAKO NA UJITAHIDI USHIRIKI KUWADHIBITI WANASIASA NA WANAHARAKATI WAONGO. MAHATMA GHANDI NI MFANO WA WATETEZI WA WANYONGE. SOMENI MAISHA YAKE MUONE KAMA ALIISHI KAMA WANAVYOISHI HAWA JAMAA ZETU WANAOJIITA WATETEZI WA WANANCHI

    ReplyDelete
  28. TUNATAKA KATIBA MPYA TU INAYOLENGA WATANZANIA WOTE NASIO CHAMA KMOJA LAZIMA KIELEWEKE KWA KWELI WATANZIA TUJUE KUWA CHADEMA IMETUELIMISHA SANA NA IMETUKOMAZA KISIASA NA WALE WANAOTUNGA KATIBA KWA MASLAHI YAO BNAFSI WAMESHACHELEWA SANA KWANI TANZANIA YA SASA SIO YA KIPINDI KILE SISHANGAI CHADEMA KUPINGA KATIBA YA WATU BINAFSI NA TUJIULIZE WATANZANIA RAIS KUWA NA MAAMUZI NA MAJUKUMU MENGI NDICHO KINACHOSABABISHA PIA NA KATIBA INATEULIWA NASIO MAWAZO YA WATANZANIA AU UGUMU WA MAISHA NAUPATA MIMI TU WATANZANIA WENZANGU? NA HII NI KWA SABABU YA MFUMO MBOVU WAKATIBA NAOMBA TUSIRUDIE KOSA LILILOFANYWA NA WALIOTUTANGULIA KUONA JUA CHADEMA KUEI NA MSMAMO MATHUBUTI NA KUTOKA NJE YA BUNGE KWAN KUKIMBIA TATIZO SIO KUMALIZA TATIZO BALI NI KUONGEZA MUNGU AWASAIDIE KULETA AMAN TANZANIA

    ReplyDelete