Na Mwandishi Wetu.
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe amesema uamuzi wa kutoka nje ya bunge wakati Rais Jakaya Kikwete akihutubia ulikuwa wa chama uliofikiwa kwa kura lakini yeye
hakukubaliana nao, ndio maana aliamua kutokwenda bungeni siku hiyo.
Akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha TBC1, Bw. Kabwe alisema yeye asingeweza kuingia bungeni na kutoka wakati Rais Kikwete ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu, na ambaye amefanya mambo mengine mkoani Kigoma kuliko marais wengine anahutubia.
"Kuliko kuingia na kubaki ndani wakati wenzangu wanaondoka, kitu ambacho kingekuwa kibaya zaidi, niliona ni bora kutoingia kabisa kwa kuwa rais ndiye alama ya bunge na amiri jeshi mkuu," alisema.
Bw. Kabwe ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, alisema ni kweli waliafikiana kwa kura na walio wengi wakaafiki kutoka lakini yeye alitofautiana, pamoja na kutambua kuwa chama kinaweza kuchuykua hatua, kwani hiyo ndiyoi gharama ya demokrasia.
Hata hivyo, alisema uamuzi huo usifikiriwe kuwa ni mgawanyiko amekanusha kuwa jambo hilo lisifikiliwe ni mgawanyiko bali mtazamo tofauti wa mawazo.
Mhe Zitto amekomaa kisiasa na hakubali kuburuzwa na akina Mboewe.
ReplyDeleteMENGI YATAJITOKEZA HAPO MBELENI,NA SI KWA CHADEMA TU HATA CCM PIA KUTAZUKA MIZENGWE MINGI TUU,MAANA HAKUNA MTU ANAKUBALI KUSHINDWA KILA MTU KAJIWEKEA KUSHINDA TUU!!NA PIA TUTASHUHUDIA WALIORUBUNIWA, KULAZIMISHWA, KUTISHWA NK, TUNAJUWA ZITTO NI KIONGOZI MKOMAVU,SHUPAVU NA ANA BUSARA NDIO MAANA AKACHUKUWA UAMUZI HUO HONGERA SANA BWANA MOGO. LAKINI PIA WATAMZUSHIA KUWA NI MAMLUKI WA CCM!! NI KAWAIDA YETU WA TZ
ReplyDeleteMhe Zitto wewe ni kiongozi mwenye kutumia busara achana na hao wasijua siasa ni nini.
ReplyDeleteWanataka kukiua chama chetu.
Mh.Zitto kumbe si mstaarabu kiasi hicho.Kaka sifa zako zitakufikisha pabaya! We umeona wapi siri za kikao zikazungumzwa kwenye vyombo vya habari? Acha sifa na unafiki Mh.Zitto.CCM wanakupoteza hao...uwe na adabu na uongozi wako wa Chama chini ya Mh.Mboye na Mh.Slaa.Kwani wewe mamluki? Chunga sana matendo na maneno yako...yatakuponza.
ReplyDeleteKuwepo kwa zitto na kutokuwepo inaleta maana kuwa wote walikubaliana kushinikiza kudai haki za watu walioibiwa kura na NeC ili kumpa ushidi Jk ambapo ni kweli wameiba kura yetu ndio maana watu wa mjini jk hakushinda ila kijijini ambapo nako wameongeza kura kwani watanzania walimchoka, ila ninawaaza wanachadema na watanzania na hata hao wabunge wetu na Dr slaa wasifanye mambo ambayo yatawagharimu tutafute muafaka kwa kuwaambia watazania kuwa kura tumeibiwa na ushindi huo bandia NeC imempa Jk nafasi hatuna la kufanya kwa sasa ila kukaa na jk na kuongelea mambo yatayoweza kuimarishwa kama tunataka mabadiliko na maendeleo,na amani kwa kumshinikiza jk kuwepo na tume huru ya Uchaguzi ambapo Watanzania watawachagua viongozi hao kama tunavyowachagua Wabubge na Rais wapendekeze kutoka kila chama ili watanzania wawachague na ni kwa miaka mitano, pia tubadilishiwe Katiba kwani nilikuwa nikisoma hiyo katiba iliyopo inamkinga rais akishatangazwa kutoshitakiwa na baadhi ya mambo ambayo kwa sasa hatuwezi kufanya lolote.
ReplyDeleteMarekebisho madogo ni 'Mh.Mbowe' na si 'Mh. Mboye'Samahani kwa usumbufu wowote uliojitokeza.
ReplyDeleteZito ni mamluki nasisitiza
ReplyDeleteUnaweza kudai haki kwa njia za busara siyo kutoka nje wakati rais anahutubia. kwani walipoingia kwenye uchaguzi hawkujua kwmab rais akishatangazwa hakuna pa kupinga. wasingeingia kwenye uchaguzi. wao wajijenge bungeni na kujenga hoja nzito ili 2015 wapate dola
ReplyDeleteZITO tunakuheshimu sana, kwa kitendo chako cha kutokuhudhiria Bungeni si kibaya. Ila kuanza kutoa siri za maamuzi ya kikao tena kilichofanyika kwa kupiga kura ambayo ni demokrasia si cha kiungwana. Ulitakiwa ukae kimya na kutuambia tu maamuzi yale ni ya chama. lakini ukianza kusema ohh wewe ulipinga na hukupendezwa inaonesha unajali sana maslahi yako kuliko ya chama.
ReplyDeleteMimi mtazamo wangu ni tofauti na Mr Kabwe,hata CCM huwa wanakuwa na mipango ya ndani ya Chama na wote waliopinga na walioafiki wkishamaliza wanaokuwa wengi uo ndo unakuwa msimamo wa chama na wote wanasimamia hilo,sasa we Zitto ni naibu katibu mkuu wa chama mmekaa mkapiga kura na kuamua kuwa na msimamo fulani,hata kama wewe hauafiki unakaa kimya,sio unaenda kwenye vyombo vya habari na kuanza kuropoka..Kwani unadhani kwenye CCM wote walitaka Sita aondolewe USPIKA? Mbona wamekaa kimya na kuafiki? Chonde chonde kama uwezi kuwa na heshima kwenye Chama usituaribie,hama mapema ujiunge na wenzako wasio na misimamo.Haki ya Mungu sikuelewi hata kidogo.
ReplyDeleteZitto kwa kweli alichokifanya cha kutoingia ni stahili yake ya kupinga kwani alitakiwa kama mbunge awepo wakati rais anahutubia na hivyo aliwaunga mkono wenzake.Tatizo la huyu Bwana mdogo ni kwamba bado anahitaji kuufikiri zaidi kwamba uamuzi wa wengi ambao ulitumia kura halali na yeye akiwa kiongozi ni uamuzi wa wote,na unachukuliwa kama uamuzi wa kikao kama yeye anaanza kutoa siri kwamba yeye hakukubali anataka nini?? ili iweje?? aonekane ni mwema sana,au mtiifu sana kwa rais,au ni nini hasa,yeye ni naibu katibu mkuu wa chama ametoa siri za kikao,je hayo ndiyo maadili,Mimi naona Chadema kama chama kina miiko na maadili na kanuni za chama,na kanuni hizo kwa vyovyote aziruhusu jambo kama hili.zitto atofautishe kuongea na marafiki zake na kuongea na waandishi wa habari,waandishi wa habari wanaandika kila kitu na ndivyo wanavyopata ujira wao.Ningemwomba tu kwa sasa ameteleza lakini wakati mwingine awe makini kwa vyombo vya habari.MUNGU AKUBARIKI ZITTO,MUNGU AIBARIKI CHADEMA,MUNGU AIBARIKI TANZANIA.
ReplyDeleteni haki yake kidemokrasia! msimshambulie
ReplyDeleteZitto kuwa makini sana na unachosema. Inakuaje unatoa siri za ndani kwenu kama umeanza mapema hivi, ni mangapi utayasema maana huu ndio mwanzo wa safari yenu Kuwa makini na unachokifanya, samaki moja akionza wote wanaoza hata kama yupo ambaye hajaoza huwa na harufu mbaya kama wale waliooza. Hata kama useme hukukubaliana nao kinachojulika ni kuwa Chadema walitoka nje ya Bunge na sio kwa majina ya watu kutajwa. Nawapongeza sana maana kama ni ujumbe umefika kwa wakati na ndio maana yamebaki majadiliano sasa na kinachofuata ni utendaji. Zitto badilika mzee maana ni sawa na maisha ya ndani ya nyumba ukifunua kila paa la nyumba unaweza usiishi na ndivyo ilivyo usifunue paa la chama chako hata siku moja
ReplyDeleteHakika huyu bwana mdogo Zito ni Mamuluki wa CCM, Chadema kuweni macho huyo ndo anaweza kuuza hata siri za Chama chenu. Msaliti na anapenda sifa, basi rudi CCM ili usaidiwe kujenga Kigoma zaidi.
ReplyDeletechadema naiman mlimchagua huyu jamaa mkiwa mnamwamin.ila kiukwel mwangalien sana,hapo jinsi ya kumkanya hebu tumieni busara maana watanzania tunawaamini sasa mkianza kugawanyika kama vyama vingine watu wataona chama hakina mwelekeo,
ReplyDeleteKINGINE;Am sure zitto ni mchokonoaji mzuri wa mambo ila sasa unataka watanzania wakose iman na wewe hebu kua kama zaman wakat hujapata jina. sasa ukikaa kimya kidogo inatia mashaka
Zitto amekomaa anajua mchele na chuya ni ktu gani. Anafaa hata kuchaguliwa waziri atumie uwezo wake kulichangamsha na kubadili utendaje wa mabaraza ya CCM tuliyoshuhudia kwa muda mrefu.
ReplyDeletezitto, uamuz wa chama ni wa wanachama wote, iweje wewe upingane nao. jitahid kuzuia hisia zako binafsi, ndio maana uamuzi huu ulifikiwa kwa kura.
ReplyDeletehapa zitto kama chadema kinakushinda nenda ccm, hapohatujengi tunabomoa, mpaka hapa tunajua zito wewe nipapeti wa ccm.
ReplyDeleteZito kuwa makini 2mekusoma toka mda mref unaweza hama usituharibie chama chetu ambacho wattanzania tuamini ni chama cha ukwel tumain jipya kuleta maendeleo
ReplyDeleteSio Zitto hata Mheshimiwa Shibuda hakuafikiana na uamuzi wa kutoka nje na ndio maana yeye alikwenda kwenye sherehe za kuwapongeza na akashikana mkono na rais. Mheshimiwa Shibuda alisema yeye yuko pale kwa ajili ya wana Maswa walomchagua na si vinginevyo.
ReplyDeleteHaya tuone waendelee kugoma, kususa na kujifanya wajuvi, kisha majimbo yao yatelekezwe kwa muda wa miaka 5 kama wananchi huko kwenye majimbo watawachagua tena. Zitto amesema kweli, isitoshe huwezi kuwalinganisha wabunge wengine wa Chadema na Zitto, yeye amekwishaonja adhabu ya kufungiwa bungeni anajua madhara yake!
Zito tumewashudia akina Tambwe Hizo, Dr.kabourou na wengine wengine ambao walishindwa Camp na kurudi walikotaka...naamini hata wewe Zitto mlango upo wazi kabisaaaaaaaaaa, na dalili ya mvua ni mawingu mie naona inakaribia kunyesha and isitoshe nilijua haya yatatokea na tena kwa wewe naona umechelewa sana, tuachie Chadema, Zitto nakufahamu ulikuwa kigeu geu hata kwenye migomo UDSM, sasa kama unaona wakati umefika ondoka kimya kimya tuachie CHADEMA IDUMU
ReplyDeleteZITO mhh kwako wewe uwajibikaji wa pamoja ndani ya chama ni upi?
ReplyDeletewewe bado kijana sana naona kilichokusukuma hapo si kingine zaidi ya ubianafsi.
unapopima mambo kwa mtazamo wa kigoma ccm imefanya nini, wakati ww ni kiongozi wa chama ambaye unatakiwa kuangalia nchi nzima unakosea kaka yangu.
je kama kikwete amefanya mengi na anafaa sana kama ulivyosema kwanini haukumuombea kula kwenye kampeni.
ilikuwa busara kufanya ulivyofanya lakini usingeenda public kuojiwa na vyombo vya habari HASA TBC.
KIKULACHO KI NGUONI KWAKO
nafikiri wakt wa wewe kuamua hatma yako ndani ya chadema imefika.
Jamani kwani wenzangu hamkujua kama zito ni kibaraka wa CCM!! kwa msimfahamu yulesio mpinzani halisina chama cake kinamfahamu ndio maana wapo makini nae...kwa mtu wa kawaida huwezi kutegemea kiongozi wa chama aende kuropoka mbele ya vyombo vya habari akieleza kwani nini aligoma kuwaunga mkono wenzake..hii nikatika kutafutamtafuruku kusudiakivuruge chama...wana kigoma kuweni makini na huyo mtoto...keshanunuliwa zamani..kama shitambala
ReplyDeleteZitto tuachie CHADEMA yetu,Tangu ulipochaguliwa kwenye kamati ya madini umebadili msimamo kabisa.Unachokipata huko kimekulevya hatutaki mitafaruku kwenye chama chetu,kama umechoka hama nenda huko CCM watakupa uwaziri nadhani unajipendekeza wakufikirie.Hata USA wanampinga OBAMA mpaka leo ACHA UNAFIKI
ReplyDeleteMhe Zito ni mzigo kwa chama cha CHADEMA NI TIME BOMB UELEWA WAKE NI MASHAKA MATUPU AMA NI MBINAFISI, OPPORTUNISTIC, CALL HIM ANY NAME, YEYE SI MSEMAJI WA CHAADEMA ILIKUAJE KUANIKA MAAMUZI YA KIKAO? NAMTABILIA MWISHO MBAYA SANA KISIASA, MUNGU AMBARIKI
ReplyDeleteSioni sababu ya kumsakama Zitto kuwa eti anatoa siri za chama kwani tayari Mbowe alikwisha lisema hilo alipokuwa anasisitiza kuwa uwamuzi wa kutoka nje ya bunge ulipigiwa kura kikaoni,na kuwa wako waliounga mkono na waliokataa.
ReplyDeleteJamani demokrasia si "NDIO MZEE" kila mara. Mambo ya NDIYO MZEE yaliishia na Nyerere na mfumo wa chama kimoja. Upinzani ndani ya chama unakijenga zaidi chama badala ya kukiuwa
Zitto Kimeo,Anaogopa Kufunikwa na Tundu Lissu pamoja na Mnyika.Anasoma alama za Nyakati,Mimi namuomba aanze mapema kama Shitambala kule mbeya,Aondolwe mapema sana!!!
ReplyDeleteZito alisema yeye kwa mtazamo wake na hisia zake. Si mtazamo wa chama. mbona amejieleza vizuri kuwa msimamo wa chama ulikuwa hivi na yeye vile. Binafsi nampongeza kwa upeo wake wa kufanya maamuzi. Inaonekana CHADEMA kuna YES BWANA nyingi!!!. Ukiwa na mtazamo tofauti na wakuu huyo ni msaliti mkubwa wa kutupwa! Hiyo si demokrasia ya kweli.
ReplyDeletePia sijaelewa kwa wemni wa wachangiaji kuhusiha maamuzi ya Zito na CCM. Mbona kuna vyama vingi kama NCCR Mageuzi ambao walisema wanamhitaji iweje leo ahusishwe na CCM?
Chadema wataamua wenyewe kuwachukulia hatua au kutowachukulia hatua wabunge ambao hawakuwepo bungeni kwa kutofautiana mawazo kuhusu swala la kususia hotobu ya Rais. kama Zito alivyosema hakuna mgawanyiko kwasababu ya tofauti ya mawazo wanaosema kuna mgawanyiko ni ccm na vibaraka wao "baadhi ya magazeti" ili kutaka kuwapotosha wananchi wajue kuwa CHADEMA hakuna umoja na ili hali sio kweli, tumewashtukia hadanganyi mtu. CHADEMA OYEEE
ReplyDeleteTUENDAPOKO SINTA SHANGAA ZITTO AKIJIUNGA NA CCM. MZEE SIFA MBAYA SIRI ZA CHAMA HAZITOLEWI NJE!
ReplyDeleteZITTTTTTTTTTTTTTTO HUNA MAANAAAAAAA
ReplyDeleteTUNAWASHUKURU WASOMI WAKUU MLIOUNGA KONO CHADEMA SHIDA NIKWA WALEWASIKUBALI KUSEMA UKWELI NIKAMA NAO NI WADOGO WA KIKWETE
ReplyDeleteKwa kweli Zitto unapenda sifa sana dogo wewe mamluki kabisa...anaharibu chama hizo ni siri za chama kwani zinawahusu watu wengine lol
ReplyDeleteHIVI NINYI MNAODAI KUWA CHADEMA WATUMIE NJIA ZA KISTARABU KUDAI HAKI MBONA HAMZITAJI? NILINI CCM WALIWEZA KUKUBALIANA NA MTU YEYOTE MWENYE KUTUMIA USTARABU AU KUELEZA JAMBO LOLOTE LA KWELI? CCM WAKIAMBIWA JAMBO WANASEMAGA NI UZUSHI HATA KAMA UNAO USHAHIDI WA KUTOSHA,SASA HUO UTARATIBU MNAOTAKA NI UPI AMBAO CCM WATAUKUBALI? TATIZO LA WATANZANIA WENGI HAWAFIKIRIAGI KWA KINA HIVYO NI RAHISI KUTOA MAWAZO KWA KUIGA TU AU KUSEMA JAMBO BILA KUFANYA UCHUNGUZI...WABUNGE WA CHADEMA KUTOKA NJE NI NJIA AMBAYO IMESAIDIA KUIBUA MJADALA NA NI SAHIHI...MBONA WATU MNATOKAGA NJE WAKATI WA MAHUBIRI AU SALA..KWANI KIKWETE AMEMZIDI MUNGU?
ReplyDeleteZITTO KUSEMA HIVYO NI UTOTO TU,NA KUTAFUTA SIFA
Kutofautiana ni jambo la kawaida hata ktk siasa. Powell hakukubaliana na siasa za Bush kuhusu Irq. Na akasema hadharani hatakichagua chama chake katika uchaguzi. Powell bado ni mwana Republican na hakuna aliyemwona msaliti. Zito yuko sahihi kueleza msimamo wake hata kama ni hadharani. Unaweza ukatofautiana na hoja yake lakini siyo kumhukumu kwamba ni makosa yeye kuwa na mtazamo tofauti.
ReplyDeleteMaoni mengine yanayotolewa yanaonesha watu wanaoyatoa WAMEFILISIKA kuwaza. Zitto hajasema kuwa alikataa kuburuzwa na wala hajasema kuwa ambao waliunga mkono maamuzi ya kikao waliburuzwa. na wala hajasema kuwa msimamo wake ni kwakuwa yeye ni dini fulani au alikuwa anapinga msimamo wa watu wenye dini au wanaotoka mahala fulani. Sasa wewe unayehusisha uamuzi wa Kabwe na dini yake, au sehemu anayotoka au usaliti katika chama ujue kuwa UMEFILISIKA KUWAZA. Acha kuweka sumu katika jamii na ndani ya chama. wakwanza kuumia mambo yakiharibika unaweza kuwa wewe mwenyewe. Tuache kufanya MASIHARA na mambo tete yanayoweza kuliangamiza taifa.
A.M.BAKARI
Hamisi Ally Maguu
ReplyDeleteChadema; kubalini yaliyopita mjipange upya kwa ajili ya 2015 hasa mkizingatia kupata Muarobaini wa uchakachuaji wa kura badala ya kulia kutomtambua raisi.
Na we Zitto si iseme tu kama umepandikizwa na CheCheMee
ZITTO KABWE, UKO SAHIHI NI HII INADHIHIRISHA UKWELI WAKO KWA WALIOKUCHAGUA NA SIO KUBURUZWA NA CHAMA CHAKO. NAWSHANGAA WANOSEMA ATI WEWE NI MAMLUKI HAWAJUI DEMOKRASIA NA WALA SI WANASIASA. KWANZA WEWE NI MKONGWE KULIKO HATA HAO WA JUU YAKO UMEKOMAA KAKA KEEP IT UP GOOD. STAND ON YOUR STAND BOY.
ReplyDeleteNafikiri ni wakati muafaka kwa Zitto kurudi kwao yaani CCM. Asisite hatokuwa wa kwanza, angalia dk Kaburu, Nswanzugwako,Hiza na wengineo wengi.Walipomaliza kazi zao walizotumwa walirudi CCM na wakatunukiwa vyeo.Haya bw Zitto amua sasa kwani tumeisha kukubaini.
ReplyDeletemnamuonea bure mtoto wa watu, yeye amejaa busara, akaona haina haja ya kumfuata mtu mwenye tamaa ya uongozi hata anapoukosa kwa kura, waliambiwa na NEC wapeleke ushahidi wakasita, hamna cha kuchakachuliwa wala nini, zitto amejua wameshindwa kihalali
ReplyDeleteKama Zitto hakuingia Bungeni, hana tofauti na waliotoka. Yeye alitangulia kutoka muda mrefu kabla ya wenzake.
ReplyDeleteTatizo lake ni kueleza njia mbadala aliyotumia.
Wote walitoka ndio maana hakuna aliyekuwemo Bungeni wakati Raisi akihutubia. Hawana tofauti yoyote.
zitto una unafiki wa kijipendekeza kwa jk ikiwezekana kalambe miguu yake. hufai kabisa kuwa chadema. chadema ni chama cha watu makini na sio kama wewe zitto kimeo wa siasa
ReplyDeleteMHESHIMIWA ULIKOSEA SANA,CHAMA KINA NGUVU KULIKO WEWE,NA HIYO NDIYO DEMOKRASIA,KUNA WATU JIMBONI KWAKO HAWAJAKUCHAGUA WEWE LAKINI WEWE NDIYO MBUNGE WAO,HIVYO WABUNGE WA CHADEMA WALIOPIGA KURA YA KUTOKA WALIKUWA NI WENGI HIVYO ULIKUWA HUNA BUDI KUUNGANA NAO KWA KUTOKA NJE! UNAMTII MWENYEKITI WA CCM KULIKO WAKO WA CHADEMA!
ReplyDeleteki-ukweli nionavyo mimi zitto kabwe chadema wanapaswa kumuangalia kwa makini sana kwani atakivuruga chama muda si mrefu. Anadhani kwa kutumia umaarufu wake anaweza fanya atakalo ndani ya chama. Ni afadhali aenguliwe mapema ili AJIRUDIE CCM kwani sio mwana mapinduzi na mpiganaji kama tulivyomjua mwanzoni na ndi maana hata ushindi aliopatakwenye jimbo lake mwaka huu ni mwembamba sana na kidogo tu jamaa wa CCM angemwangusha. Hiyo ni ishara ya kuchokwa hata na wapiga kura wake
ReplyDeleteKitendo cha Mhe. Zitto kukaidi Msimamo wa Chama kinaleta kichefuchefu. Imebaini wenzetu Chadema wana kazi kubwa huko mbeleni wasipoangalia. Sikutegemea kuona Kabwe kwa nyadhifa zote alizonazo ndani ya Chama na Bungeni kwamba angeweze ku behave namna hivi. Imedhihirika kuwa Zitto ni Mnafiki, mwoga na Msaliti. Haya ndiyo sura ya Zitto. Nashukuru kwa kunyimwa Uwenyekiti wa Chama aliokua anagombea, pia Chama iliona mapema kuwa hawezi kupewa Overall ya Kiongozi wa Kambi Rasmi. Kama angekuwa ndiye Mwenyekiti wa chama kama ilivyokuwa ndoto yake pia na Kiongozi wa Kambi Rasmi Bungeni, leo tungekua na agenda gani na Zitto. Huyu bwana pamoja na kwamba anamwagiwa sifa huyu ni hafai kabisa. Kwanza amelewa pesa za mishahara na shangingi vitu hakutegemea kuvipata kwa umri wake leo. Akumbuke kama chama kingemtosa wakati akifukuzwa Bungeni wakati ule au endepo Angeshindwa Ubunge safari hii nadhani kauli zake hizo angekuwa amezibadili.
ReplyDeleteAsifikiri sisi tuliye barabarani ni wabumbavu wala hatuna uwezo wa kuongoza nchi au maeneo fursa ikitokea.
Asifikiri kwamba watu hawaoni anakoelekea. Safari anazofanya asifikiri watu hawajui. Kumbuka Karamagi alisaini mkataba usiku London lakini watu walijuwa na ikatolewa nje sembuse yeye bwana mdogo. Achunge sana, aache tamaa za kutaka sifa na kipato haramu. Kama ameona ameichoka Chadema si aondoke!!!!! Akumbe kuwa hana umaarufu kuzidi Chadema kwa leo. Ni Chadema ndiyo imekufikisha hapa ulipo leo na wala siyo vinginevyo. chunga sana. Wako wapi waliokuwa wanatisha: Kina Mrema, Kabourou, Masumbuko Lwamai, Tambwe Hizza na wengineo. Kama hujuwe nakutaarifu kuwa huo ni mtego wa kukumaliza kisiasa. Ukitapikwa na Chadema usifikiri utakuwa salama NCCR au CCM. Utabaki makapi. CCM ina watu maarufu sana kuliko wewe, ukitapikwa utavuma na punde kidogo utafutika katika ulingo wa siasa. Kula kidogo, itumikie nchi hapo ulipo. Usifikiri kuwa kina Karamagi, Lowassa, Msabah au CCM wanakutazama kwa jicho la wema ukizingatia hasara ambayo umeshiriki kuipotezea serikali heshima ya kuvunjika kwa baraza zima la mawaziri na kuunda jipya huku gharama ya mamilioni ya pesa kwa kutekeleza mchakato huo. Yapo mengi tungekushauri ila hatuna ukaribu na wewe. Acha tu tukufikishie ujumbe huu kupitia safu hii. chunga sana
Tunawesa kusema kuhusu kina Shibuda na wengine, hao wanasameheka kwa sababu kwa mfano,huyu Mhe.Shibuda yeye amepikwa na kuwiva ki-CCM. Yeye hana ideology ya Upinzani. Ni juzi tu amejiunga si kwa sababu ya mapenzi ya Chadema bali ni kutaka kuingia Bungeni kwa kuikomoa CCM waliomchezea rafu na kuionyesha kwamba anapendwa na wananchi wake. Ila siyo kama mkongwe tena kinara kama Zitto.
ReplyDeleteMh. Zito
ReplyDeleteNakupa pongezi kwa kuonyesha njia si kwa Chadema tu bali hata kwa WaTZ lazima tufike mahali ambapo tukubali kujitoa kwa maslahi ya kizazi kijacho, tunapotumia hukumu ya bila hekima tunapotosha maana nzima ya demokrasia, na si kila kitu kinachosemwa au kuamuliwa na wengi lazima ukifuate, hebu tuangalia akina Mama Kilango, Selelii, Sita nawengine hata pale CC ya CCM ilipotoa vitisho lakini waliendelea kuwa na msimamo ulioleta changamoto nyingi na mageuzi katika uchaguzi hatimae Chadema ikaonekana bora, siasa ni mtazamo na maamuzi pia ni mtazamo kama watoa mada wengine, hukumu ni kujadili hatma ya maamuzi kichama kwa faida ya nchi si kundi la watu.
lazima tujenge utamaduni wa kuheshimiana na si kuchafuana.