01 August 2011

Hali ya mwenendo wa bunge hairidhishi CCK

Na Edmund Mihale



KATIBU Mkuu wa Chama cha Kijamii, Bw. Renatus Muhabhi amesema kuwa hali mwenendo wa bunge kwa sasa ni ya kusikitisha kutokana na kuja vituko vinavyofanywa ndani ya bunge hilo kuwa mithili ya komedi.


Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaama jana, Bw. Muhabhi alisema kuwa wabunge kwa namna moja ama nyingine wamejikita kwenye malumbano yanayopotosha hata malengo ya uwakilishi wao na dhana ya kusimamia maslahi ya uwakilishi wao.

Alisema kuwa wamesahau kuwakilisha wanachi na badala yakea wameajikita kwenye malumbano yanayopotosha hata lemgo la uwakilishi wao na dhamana yao ya kusimamia maslahi ya wananchi.

Alisema kuwa wabunge kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia muda mwingi kuwakilisha misimamo ya vyama vyao kuliko wanachi.

"Mtakumbuka kwamba majukumu ya bunge na wabunge hayaishii kuelezea kukosoa na kuichunguza kwa lengo la kuleta ufanisi na maendeleo ya kwa wananchi wake kitu tunachokiona leo katika bunge letu ni kushindwa chombo hicho kujitofautisha na dola kwani wabunge wengi wanaonekana kuibeba serikali kana kwamba wameatumwa na serikali bungeni,"alisema Bw. Muhabhi.

Alisema kuwa wabunge wameakuwa kitumia muda mwingi katika kaujadili mambo amabyo kimsingi hayalengi kumtoa Mtanzania katika dimbwi la umasikini jukumu ambalo wangepaswa kulisimamia
kwa nguvu zote ilikuleta mabadiliko katika maisha yao.


"Ni ukweli usipingika kwamba wabunge wengi wamekuwa watoro katika vikao vya bunge huku wengine wakishia kuuchapa usingizi kwenye vikao kenye vikao hivyo wengine wakiendesha vikao vya makundi ndani ya ukumbi wa huo huku wengine wakiwa wanaendelea na zoezi la uchangia wa hoja kama hayaitoshi wabunge wengine wanaishia kusifu na kuunga mkono hoja na ma kutounga mkono hoja hata kama haistahili kuungwa mkono," alisema Bw. Muhabhi.

Alisema kuwa bunge linapotosha dhana nzima ya chombo hicho cha kusimamia demokrasia  ambacho ni moja ya mhimili mitatu ya uongozi wa taifa hivyo vitendo hivyo havina maana kwa taifa na watu wake.

Alisema Watanzania wanatakiwa kurudishiwa haki yao ya kuona metadata yenye hoja yakinifu za zenye uchambuzi wenye lengo la kuharakisha maendeleo ya nchi na yenye keleta tija.

 

3 comments:

  1. Tatizo ni mfuno dume.ccm wamepata wapinzani hawataki.mpinzani akitoa kauli anaonekana hafai,nani atakubali kuitikia tu ya ccm.upendeleo uliokidhiri,mfano mdogo mnyika alitoa buget ya nishat kuwa kuna nyenzo mbadala za kufua umeme,jk alivoulizwa akajibu kwa hasira kuwa akafue basi,hivi unatarajia wabunge wakubal.hatak mawazo hatak mabadiliko,hilo bunge bado ngumi zitatembea one day.watu hawataki mawazo ya wengine,nani atakubal enzi hizi.hali hiyo itadumu,vijana wanataka nafas zao ziheshimike na mawazo yao.mmmbadoooo

    ReplyDelete
  2. Maneno yote yanayosemwa bado yanakuwa yanatolewa kisiasa zaidi kuliko kujadili kwa kuangalia upana mzima wa uwanja wa mjadala. Wabunge wengi wa CCM, ukiondoa wachache ambao kwa sababu za kukosa nafasi fulani katika chama, wamekuwa wasemaji wa serikali ilhali majimbo yao yakiwa wahanga wa sera mbaya za chama chao. Nini sasa maana ya yote yanayo tokea? Jaribuni kuunganisha tukio kama lile la kule Nzega pale wagombea wa CCM katika kuteuliwa kugombea ubunge, mtu wa kwanza alionekana si raia lakini leo ni mtu wanayemuomba kwenda kugombea kule Igunga, kulikuwa na nini wakati ule? mtu wa pili alikuwa aliyekuwa mbunge Selelii, kwa nini aliachwa na kuchukuliwa mtu wa tatu? Pamoja na kupendwa na wananchi kama Spika bila kujali kama alikuwa pia akikisaidia chama kwa mbinu kubwa na za kisasa, wapi alipelekwa Sitta? Nini basi atakochokifanya aliyepewa dhamana hiyo baada ya mbinu hizo chafu kutumika, kama siyo kuunga mkono hata pale hoja ni kumtoa uhai shangaziye? Ni wabunge wachache sana wa CCM ambao wameweza kuingia bungeni kwa nguvu zao na hoja bali kwa kusaidiwa na nguvu za chama na dola na au rushwa na ujinga wa wapiga kura!

    Nakubali kurekebishwa.

    ReplyDelete
  3. Tatizo ni ukandamizaji wa wazi unaofanywa na spika, naibu wake na wenyeviti wa bunge dhidi ya hoja za wapinzani. Wabunge wa upinzani wamekuwa wakinyimwa uhuru wa kuwasilisha hoja zao kikamilifu kitu ambacho ni tofauti kwa wale wa chama tawala. Hata nyumbani kwako kama utakuwa katili au dikteta na kukandamiza mawazo ya watoto ipo hatari kwa watoto hao kugeuka wajeuri. Endapo itatokea hali hiyo, lawama lazima ibebwe na mzazi. Uendeshaji mbovu wa bunge ndiyo umesababisha hayo yote yanayotokea. Wanaosimamia mijadala bungeni ndiyo wa kulaumiwa!

    ReplyDelete