BERLIN, Ujerumani
TIMU ya taifa ya wanawake ya Brazili, juzi iliichapa Equatorial Guinea mabao 3-0, katika mechi ya Kombe la Dunia kwa wanawake iliyochezwa nchini
Ujerumani.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Uingereza (BBC), washindi hao wa pili barani Afrika, walishika uwanjani wakiwa wanajua kuwa, tayari wametupwa nje ya michuano hiyo.
Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika, timu hizo zilikuwa suluhu, lakini mabao yaliyofungwa na Erika na Christiane, baada ya mapumziko yaliiwezesha Brazili kuibuka na ushindi.
Katika mechi nyingine, Australia iliifunga Norway mabao 2-1 na kukata tiketi ya kucheza hatua ya mtoano ya michuano hiyo.
Mbali na matokeo, Equatorial Guinea ilionesha kiwango kizuri, kama walivyokuwa wakishinda katika mechi zao zote za kirafiki.
The first half was an even affair with Brazil's five-time World Player of the Year, Marta, ably marshalled by the Africans' defence.
Nahodha wa Equatorial Guinea, Anonman, alikuwa mhimili mkubwa, ambapo hakuwapa nafasi washambuliaji wa Brazili.
Baada ya mapumziko, Waamerika Kusini hao, walitafuta njia nyingine na kufanikiwa kupata bao kupitia kwa Erika.
Erika aliumiliki mpira kifuani akiwa ndani ya eneo la hatari, na kupiga shuti la mguu wa kulia na kujaa wavuni.
Bao la pili lilipatikana muda mfupi baada ya Christiane kutumia makosa ya mabeki wa Equatorial Guinea na kufumua shuti kali lililojaa wavuni.
Bao la tatu alifungwa kwa mkwaju wa penalti na kuiwezesha timu yao kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Equatorial Guinea wameaga mashindano hayo bila ya kuwa na pointi yoyote, lakini kumbukumbu yao kubwa itakuwa mchango wao waliouonesha katika mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment