*Kuthibitisha leo tuhuma za Baraza la Mawaziri
Na Grace Michael, Dodoma
MBUNGE wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Bw. Zitto Kabwe, leo anawasilisha maelezo yake kuthibitisha kauli aliyoitoa bungeni akituhumu Baraza la Mawaziri kutoa maamuzi yanayotokana na
ushawishi watu wenye nia ya kuua mashirika ya umma.
Tuhuma hizo alizitoa bungeni wiki iliyopita wakati akichangia azimio la kuongeza muda wa uhai wa Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC).
Kutokana na tuhuma hizo, Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda alimpa muda wa siku saba ambazo zinamalizika leo, kuthibitisha kauli yake.
Akizungumza na Majira jana, Bw. Zitto alisema leo atawasilisha taarifa hiyo kwa Spika Makinda kama alivyoagizwa.
Katika mjadala huo, Bw. Zitto alipingana moja kwa moja na azimio hilo ambalo lilitaka kuongezwa muda wa miaka mitatu kwa CHC ambapo yeye alishauri liongezwe muda wa kutosha ili kukamilisha majukumu yake.
Hoja nyingine iliyomfanya apinge na kushikilia tuhuma hiyo kwa mawaziri, alisema kuwa maamuzi yaliyofikishwa bungeni yanatofautiana na makubaliano yaliyofikiwa katika Kamati ya Uchumi na Fedha.
Bw. Zitto aliwataka wabunge kukataa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kwa kuwa yametokana na kurubuniwa na watu wenye lengo la kuua CHC kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
Alisema kuwa CHC ni chombo kinachoangalia mali za umma na mashirika, lakini pia kuna kesi mbalimbali za watu ambao wanadaiwa na mashirika, hivyo kwa kutoa muda wa mfupi ni kutaka kuua shirika hilo.
Shughuli zinazofanywa na CHC ambazo mpaka sasa hazijakamilika ni pamoja na urekebishaji wa TRL baada ya kampuni ya Rites kuondoka, kushughulikia uuzaji wa hisa za serikali NBC (T) Ltd, uhakiki wa mashirika yaliyobinafsishwa, urekebishaji wa mashirika 34 yaliyobaki na kukamilisha ufilisi wa mashirika ya umma 24 yaliyobaki, ukusanyaji wa madeni ya iliyokuwa NBC yenye thamani ya sh. bilioni 15.8 na urekebishaji wa kampuni ya TTCL baada ya hatua ya awali ya ubinafsishaji kushindikana na mwekezaji wa Airtel kuonesha nia ya kutoka katika ubia.
Big up Mh. Zitto. Huyu Spika Makinda yuko hapo bungeni kwa ajili ya kulinda maslahi ya wakubwa zake tu hilo linaeleweka. Na huo uthibitisho utaishia kimya kimya hatauweka wazi kama alivyopokea ushahidi wa Mh. Lema kuhusu Waziri Mkuu kutoa maelezo ambayo ni uongo akamezea kimya mpaka leo. Mbona hili limama linakuwa kali sana anapohitaji ushahidi lakini akishaletewa mpole kama maji yaliyoko kwenye chungu. Ifikie mahali akubaliane na uozo ulioko serikalini japo yeye amewekwa kwa ajili ya kulinda madhambi yote ya Mawaziri. Laakini iko siku ataumbuka tena siku zenyewe si nyingi zinahesabika.
ReplyDeleteKinachotakiwa ni Zito kutoa ushahidi , ajabu jamaa anamshambulia spika na kutoa madai yasiyo na msingi dhidi yake, amewekwa amewekwa , ni madai ya kitoto . soma utaratibu Spika anapatikana kutoka chama chenye wabunge wengi , na kwa TZ ni CCM sasa wewe ulitaka wakuchague wewe uwe spika? Mbona hamtumii akili kutoa maoni? kuna tatizo gani Zitto akiambiwa alete ushahidi? wa madai yake ?
ReplyDeleteWewe kama unakereka na Makinda kuwa Spika , utaumia bure ndugu yangu , huyo ndo Spika na hakuna vinginevyo .
Najua mlimzoea Sitta ambaye tayari alikuwa mguu pande mmoja CDM na mwingine CCJ , na akatumia uhasama wake na wanamtandao wenzake waliomuingiza JK madarakani kuwapendelea akiwa spika .
Sasa mazoea hujenga tabia , mmezoea mnadhani kila spika anatakiwa kufanya kama Sitta. hapo ndipo unapokosea ukitaka hivyo hakikisha caham chako kinakuwa na wabunge wengi na kinaunda serikali . kwa kuwa ndg yangu usichoelewa ni kwamba hata kama angekuwa spika anatoka chadema lazima watu au wabunge wa vyama vingine wangelala.
Haya Shibuda anataka posho iongezwe hadi shilingi laki tano -HAPO VIPI?- .
Mnamuhusudi Sitta na hamkumbuki kuwa yeye ndo aliasisis POSHO , akajenga ofisi ya spika Urambo, akapitisha mfuko wa jimbo? na mengine kedekede , hamuoni hayo ila mnaona Makinda anawabana na kupendelea acheni ushamba.
Wala usijisumbue kupeleka ushahidi huo, maana hautafanyiwa kazi yoyote chini ya uongozi wa Bunge hili la kishabiki. Ile kuagizwa ufanye hivyo ilikuwa ni kufunika kikombe tu ili ................
ReplyDeletehapa tunachotaka ni KATIBA yetu, hii ndiyo itakuwa sulihisho la matatizo yetu yote haya, zaidi ya hapo tutaendelea kutwanga maji tu.
nawe uliyeocomment hapo juu naona umeandika tu kwasababu ulikua hutumii kalamu afu nafikiri uko chama moja na spika ndo mana unamtetea kama zito hatumii akili wewe ndie unaetumia akili kwa kushabikia ujinga mkubwa kiasi hicho jaribu kufanyia akili zako update kiongozi
ReplyDeleteMbona mnaongelea hawa ma-ajenti waliowekwa kwa kunufuisha chama tawala? Shibuda, Mrema hawa ni ma-ajenti hivyo wako kwa ajili ya kuvuruga tu na hata siku moja hawatakaa waikosoe serikali ili itende haki kwa wananchi wake. Kazi ya Wabunge ni kuichachafia serikali pale inashindwa kuwajibika. Cha ajabu wabunge wengine haswa wa CCM hawana ubavu wa kutetea wananchi waliowachagua badala yake wanaitetea serikali hata pale inaposhindwa kutekeleza mambo muhimu kwa wananchi wake kutokana na viongozi waliopewa dhamana kuwa na tamaa ya kujilimbikizia mali na kuwasahau watanzania walio wengi kwamba nao wanastahili. Na hii ndio imesababisha wengine kuitwa mafisadi wanaotakiwa kujivua gamba. Kwa huyu ndugu unayemtetea Makinda huyu lazima asakamwe kwa sababu Mbunge anayetoa hoja nzito lazima anamnyamazisha. Hebu jiulize kwa nini afanye hivyo. Ina maana yeye yuko pale kwenye kiti cha Uspika ili alinde maslahi ya vigogo tu na si vinginevyo.
ReplyDeleteNyie CCM ni wajinga sana. Kazi yenu ni kulinda maslahi yenu tuu kichama wala hamwafikirii walalahoi. Kama kamati ilikataa kuifuta CHC kwanini waziri bado anganganie kuwasilisha mapendekezo ya kulifuta. Haitaji akili ya shule kuhua kwamba waziri ameshinikizwa kwa maslahi binafsi. Na wewe anonymous akili yajo iko tumboni kama hao wenzako wa CCM. Kama unazungumzia kanuni mbona Lema aliwasilisha ushaidi kule Arusha mpaka leo Spika yuko kimya? au kukaa kimya ndio kanuni yenyewe inavyosema kama huwezi kuchangia positively bora ukae kimya sio kurukia mambo usiyoyajua.
ReplyDeleteAcheni ushabiki wa kisiasa wa vyama vyenu,kiutaratibu Zitto anatakiwa kuwasilisha maelezo ni swala la kanuni za Bunge ambazo hazijatungwa na spika,jambo la muhimu ni kujadili kuwepo au kutokuwepo kwa CHC.
ReplyDelete