LONDON, Uingereza
ROMAN Abramovich atavunja mkakati wa Jose Mourinho wa kutaka kumsaini Michael Essien kwa pauni milioni 18.Lakini, kunaweza kutokea badiliko moja kwa
Chelsea la mchezaji wa kiungo wa zamani, Roberto Di Matteo kurejea klabuni kuungana na aliyekuwa kocha namba mbili wa timu hiyo, Andrea Villas-Boas.
Kocha wa zamani wa Blues, Mourinho anamtaka mchezaji kutoka Ghana, Essien mwenye 28, ili kuongeza nguvu katika timu yake ya Real Madrid.
Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, billionea wa Chelsea Abramovich amesisitiza kuwa, Essien hawezi kwenda kokote au kuungana na Mourinho.
Mourinho alimsaini Essien katika timu ya Chelsea wakati alipokuwa kocha wa timu hiyo kwa ada ya pauni milioni 24.4, Agosti 2005.
Mchezaji huyo amebakiza miaka minne katika mkataba wake wa sasa ambao unamfanya alipwe pauni
110,000 kwa wiki na anafurahia kubakia katika timu hiyo ya Stamford Bridge.
Chanzo cha juu katika Chelsea kilisema: "Abramovich hatamuuza."
Di Matteo amekuwa akitaka changamoto baada ya kuachwa na timu ya West Bromwich Albion.
Atachukua nafasi ya Paul Clement, aliyekuwa msaidizi wa Carlo Ancelotti katika miaka miwili, ambaye inaonekana ataondoka.
Gianfranco Zola naye anaweza kujiunga katika benchi la ufundi la Bridge .
No comments:
Post a Comment