*Asamoah atua na kuanza mazoezi
Na Elizabeth Mayemba
UONGOZI wa Yanga, umetema wachezaji wanane katika usajili wa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.Akizungumza
Dar es Salaam jana, Msemaji wa Yanga Louis Sendeu alisema wamefuata taratibu za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuwaacha wachezaji hao mapema ili watafute timu nyingine kipindi hiki cha usajili.
"Tumezingatia kanuni katika suala hilo na pia ni wakati muafaka kwa wachezaji walioachwa kutafuta timu nyingine za kuchezea msimu ujao," alisema Sendeu.
Alisema kati ya wachezaji hao, watatu wamekatishiwa mikataba yao na wanane wameshamaliza.
Msemaji huyo aliwataja waliokatishiwa mikataba yao ni Nsa Job, Yahaya Tumbo na Nelson Kimath ambao tayari wamelipwa fedha zao.
Sendeu alisema wachezaji ambao wamemaliza mikataba yao ni Athuman Idd 'Chuji', Razak Khalfan, Waghana Ernest Boakye na Isaack Boakye pamoja na kipa Mserbia Ivan Knezevic.
Alisema Kamati Usajili bado inaendelea na utaratibu wake wa usajili na mara baada ya kukamilisha wataweka hadharani majina ya wachezaji wote.
Sendeu alisema mchezaji raia wa Ghana, Kenneth Asamoah aliwasili nchini jana na leo anatarajiwa kuungana na wenzake kwa ajili ya mechi yao ya kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, inayotarajia kuchezwa kesho Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Wachezaji wa zamani wa Yanga waliobakia ni Yaw Beko, Shadrack Nsajigwa, Fredy Mbuna, Chacha Marwa, Nadir Haroub 'Canavaro', Juma Seif 'Kijiko', Kigi Makassy, Nurdin Bakari, Davies Mwape, Jerson Tegete, Shamte Ally Godfrey Bonny, Bakari Mbegu na Job Ibrahim.
Wengine ni Omega Seme, Abuu Ubwa, Idd Mbaga, Salum Telela,Mohammed Mbegu na Stephano Mwasika.
Wachezaji wapya wanaodaiwa kusajiliwa na klabu hiyo ni Said Mohammed, Oscar Joshua, Haruna Niyonzima, Kenneth Asamoah, Godfrey Taita, Julius Mrope, Rashid Gumbo na Pius Kisambale.
kwa nini mmemtoa chuji?alafu fanyeni mpango mzibe pengo la ngassa mwaka huu mashabiki tunataka round ya kwanza tu dalili za ubingwa tuzione kazi njema.
ReplyDeletevipi kuussu usajili wa Niyonzima inakuwaje mimi SALEH SUNDAY yanga wa ukweli
ReplyDelete