09 June 2011

Yanga yaishangaa TFF kuchangia 'kiduchu'

Na Elizabeth Mayemba

UONGOZI wa Yanga umesema umesikitishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kwamba utachangia sh. 600,000 tu kwa ajili ya matibabu ya
mchezaji wake, Stephano Mwasika aliyeumia kwenye timu ya taifa 'Taifa Stars, huku klabu hiyo ikiingia gharama kubwa zaidi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Msemaji klabu hiyo, Lopuis Sendeu alisema mchezaji huyo aliumia goti kwenye mazoezi ya timu ya Taifa Stars, hivyo TFF ilipaswa kugharamia matibabu ya mchezaji huyo.

Alisema cha kushangaza klabu yake ndiyo inayohaha kutafuta fedha za kumpeleka mchezaji huyo kufanyiwa upasuaji nchini India.

"Hadi sasa hivi TFF haijatoa fedha yoyote zaidi ya kusoma tu kwenye magazeti kuwa watachangia sh. 600,000, kiasi hicho ni kidogo mno kwa sababu mchezaji huyo aliumia kwenye mazoezi ya timu ya taifa, matokeo yake sisi ndiyo tunaoanza kuhangaika ili tupate fedha za kumtibia mchezaji huyo," alisema Sendeu.

Alisema uongozi unawaomba wadau mbalimbali wa soka nchini wamchangie mchezaji huyo, ili akafanyiwe upasuaji aweze kurudi katika hali yake ya zamani.

Sendeu alisema mchezaji huyo aliumia wakati Stars walipokuwa wakifanya mazoezi ya kujiandaa na mechi yao ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika, dhidi ya Afrika ya Kati.

Kwa mujibu wa daktari wa Yanga Juma Sufiani, alisema mchezaji huyo anatarajia kuondoka nchini muda wowote kwenda India kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa goti, ambapo alisema maumivu ya goti kwa mchezaji huyo yalianza kumsumbua tangu mwaka jana.

6 comments:

  1. Kumbe alikuwa anaumwa toka mwakajana, sasa yanga tunalalamika nini TFF kutuchangia sh laki6? Lazima tuwajibike kutibu wachezaji wetu kwa manufaa ya timu.

    ReplyDelete
  2. Ni haki ya TFF kugharamia matibabu,kwani kaumia na timu ya Taifa na ndio maana wachezaji huwa hawajitumi saanna wakiwa ma Taifa kuliko timu zao, nawe kaka hapo juu "Eti kaumia toka mwaka jana sasa Ynga wanalalamika nini" Alikuwa na timu ya Taifa ktk mazoezi kujiandaa na mechi na Afrika kati ilikuwa ni mwaka jana!!sasa wewe unazungumza nini? Matibabu India ya goti ni zaidi ya million 6 au 7 basi TFF ingetowa hata nusu yake kwa Uzalendo!!

    ReplyDelete
  3. Hao jamaa wa TFF wanachojua wao si kula jasho la wachezaji tu ni mahodari sana wakukata hela za mechi lakini kutibu wachezaji ndio hawajui? au ni uroho na ulafi tu mchezaji kuumia kwenye timu ya taifa ni jikumu lao kumtibu

    ReplyDelete
  4. Jamani kwa nini wachezaji wa Taifa na timu kubwa kama Yanga wasinunuliwe Bima? Mtu anayeelewa ili anieleweshe.

    ReplyDelete
  5. Mtoa maoni wa tatu sijui analalamika nini hebu soma hiyo habari vizuri hapo juu kwa umakini.Huyo mchezaji halikuwa anasumbuliwa na maumivu ya goti tangu mwaka jana na atakuwa kajitonesha zaidi katika mazoezi ya timu ya taifa.TFF wanatakiwa kutoa mchango vilele katika matibabu ya huyo mchezaji lakini wausika zaidi ni Yanga.Huo ndio ukweli wa mambo

    ReplyDelete
  6. Kwahakika itakuwa aibu kwa Yanga kuzipokea pesa hizo. Pesa hizo hazitotosha hata nauli ya mgonjwa ambaye lazima atahitajia wakufuatana naye. Yanga zikataeni pesa hizo. Kwakuwa mchezaji huyo ni nyota wa timu ya taifa, hata pindi angeliumia wakati akiiwakilisha timu yake, basi TFF ilibidi vilevile kutoa musaada.

    ReplyDelete