Na Peter Mwenda
JESHI la Polisi Tanzania limeanza kutumia michezo ili kutoa elimu kwa jamii kufuata sheria za nchi ili kujiepusha na matendo maovu.Akizungumza na viongozi wa
dini ya kiislamu wa Mfuko wa Mwinyibaraka Islamic Dar es Salaam jana, MKuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema alisema wameanzisha michezo katika mikoa mbalimbali nchini ili kutumia nafasi hiyo kuwabadili vijana kuacha nyendo zinazochangia uhalifu.
"Tumeanzisha Kombe la Kova katika mkoa wa Dar es Salaam, Mkoa wa Mwanza kuna Kombe la Kamanda Sirro na mikoa mingine tunaendelea kufanya hivyo hivyo" alisema Mwema.
Alisema michezo inatengeneza ajira na kupunguza vijana kujihusisha na vitendo vya uhalifu hivyo Jeshi la Polisi linakwenda mpaka katika ngazi ya Kata kuhamamisha vijana kujiunga na michezo.
"Mashindano hayo nia yetu ni kutengeneza ajira na hapo hapo taaluma na vipaji vya wachezaji wazuri vitajitokeza" alisema Mwema.
Alisema jeshi la polisi linatimiza wajibu wake wa kazi kutumia gharama au nguvu na hiyo inatokana na baadhi ya viongozi kutotii sheria za nchi na kusababisha kupotea kwa amani na utulivu kunakowatisha hata wawekezaji.
Mwema alisema jeshi lao limeanzisha mpango wa kufuata sheria bila kushurutishwa kutoa elimu kwa viongozi wa dini na baadaye watakutana na viongozi wa siasa ili kuondoa hofu walioanza kuwa nayo wananchi.
No comments:
Post a Comment