06 June 2011

Ukomeshaji utumwa kuadhimishwa Z'bar leo

Na Mwajuma Juma, Zanzibar

KANISA la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar leo linaadhimisha miaka 138 tangu kukomeshwa kwa biashara ya Utumwa Afrika Mashariki na kuwataka Watanzania
kuienzi historia ya siku hiyo.

Hayo yameelezwa na Msaidizi Katibu wa Kanisa hilo James Kaleza alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Kanisa hilo Mkunazini Zanzibar.

Alisema biashara ya utumwa ilikomeshwa Juni 6, mwaka 1873 ikiwemo kufungwa Soko la Watumwa lililokuwa katika eneo la Mkunazini mjini Zanzibar, baada ya kusainiwa mkataba kati ya Serikali ya Sultani na Uingereza.

Alisema biashara ya utumwa ilisitishwa Zanzibar baada ya
mvumbuzi Dkt. David Livingstone kutoa hotuba kali nchini Uengereza ambayo iliwavutia wanafunzi wa vyuo vikuu vya Oxford na Cambirdge kuhusu madhila ya biashara ya utumwa yaliyokuwa yakifanyika Afirika Mashariki.

“Leo hatuna tena biashara ya utumwa hapa Zanzibar wala Afrika, soko lile halipo tena yapo mabaki ya historia ambayo yamefichwa, alisema Katibu Msaidizi huyo na kushauri siku hiyo iwe naadhimishwa kitaifa kulinda historia.

Alisema uhuru wa kwanza wa Muafrika ulipatikana Juni 6, mwaka 1873 baada ya kukomeshwa kwa biashara ya utumwa na kusisitiza umuhimu wa vizazi vipya kutembelea maeneo ya historia, yakiwemo mapango yaliyokuwa yakihifadhi watumwa kabla ya kuuzwa Ulaya.

Alisema biashara ya utumwa ilianza kufanyika Zanzibar baada ya kuingia Wareno na baadaye iliendelea baada ya waarabu kushinda vita hadi ilipokomeshwa na wamisionari walioingia Afrika Mashariki kupiga vita biashara hiyo.

5 comments:

  1. Ama huyu Askofu mpuuzi na mbumbumbu. Kwani Utumwa ulikuwa Zanzibar peke yake?. Kwanini aiadhimishe maeneo ya kwao Tanganyika walikokuwa wakikamatana na kuuzana.

    Kwa taarifa kuwa hakuna M-Zanzibari aliyekuwa Mtumwa na kuuzwa maana biashara ya Utumwa na kukamata watu ikifanywa na Watwana wa Ki-Tanganyika

    ReplyDelete
    Replies
    1. mimi nadhani hujaenda shule au kujiendeleza kufanya tafiti kama babu zako walikamatwa na kuuzwa, kwa vile umeficha sura yako sijaweza kukutambua pengine ni mjukuu wa hao watumwa, ila umejisahau

      Delete
  2. Ama huyu Askofu mpuuzi na mbumbumbu. Kwani Utumwa ulikuwa Zanzibar peke yake?. Kwanini aiadhimishe maeneo ya kwao Tanganyika walikokuwa wakikamatana na kuuzana.

    Kwa taarifa kuwa hakuna M-Zanzibari aliyekuwa Mtumwa na kuuzwa maana biashara ya Utumwa na kukamata watu ikifanywa na Watwana wa Ki-Tanganyika

    ReplyDelete
  3. Wewe hapo juu huna hoja na hujui historia, inaonekana umeharibiwa na msahafu wewe. Soma historia usisome msahafu pekee yake! Wewe huelewi kwamba Zanzibary ilijaa watu wa Tanganyika na waarabu toka Omani? Kwa ukweli wazanzibar weusi ni watanganyika kwa asili yao. Pemba na Unguja vilikuwa visiwa tupu. Watanzania bara wakaletwa viswa vya Zanzibar na waarabu waliowatesa sana babu zetu. Waraabu walichagua kukaa Pemba hasa. Na huku unguja wakaweka waafrika kulima karafuu. Hawa walikuwa ni watumwa wanyamwezi hasa. Na hawa ndo walikuja kudai uhuru wao wengi wao waliupenda ukristo kwa kuwa ulikataza utumwa. Ni utamaduni wa waarabu uliwalazimisha baadhi yao kuwa waislamu hata leo. Soma historia ndugu yangu. Usibaki na msahafu pekee yake. Kwa taarifa yako hakuna mwenye Zanzibar yake kwa asili wote walitoka nje waafrica wakitoka Bara na Waarabu wakitoka Omani kuja kufanya makao yao ya Biashara Zanzibar. Na biashara yao kubwa ikawa kununua na kuuza waafrika kama watumwa. Wengi wa mababu zetu walichinjwa kama mbuzi na hao waarabu wenu. Wanawake walibakwa ili kuona watazaa watoto wa jinsi gani waarabu au weusi. Wanawake walichinjwa na kutolewa mimba ili waone kitu kilichokuwa ndani. Hawa ndio waarabu unaowahusudu sana wewe. Labda na wewe una mbegu ya kiarabu.

    Ndugu yangu Zanzibar ni ya Watanzania Bara toka zamani. Kisiwa kilipogunduliwa na waarabu wakasema kiko nje ya Tanganyika wakaifanya himaya yao. Wakiwaleta waafrika wa bara kuja Zanzibar kama watumwa. Waafrica hawa ndo wamekaa pale miaka nenda rudi wakaja kudai uhuru wao. Ndo hao leo wakina Komandoo, Balozi Seif Idd, Sepeku na wakina Karume ambao damu yao imechanganyikana na waarabu. Maalimu yeye ni mwaraabu kabisa na hata ndiye anayetaka sana babu zake waalabu warudi kutawala Zanzibar akidai Zanzibar ilikuwa ni ya waarabu wa Omani eti ndio walioigundua. Na kumbe Zanzibar ilikuwepo tangu siku zote. Sisi tunasema Mwaraabu harudi Zanzibar tutachinjana sana kama agenda ya kurudisha mwaraabu itafanikiwa. Na bahati mbaya sana waalabu wanatumia umbumbu waafrika wenzetu wa Zanzibar kwa kigezo cha uislamu ili kurudi kuitawala Zanzibar hatutakubali hata kidogo. SIsi vijana tumeisoma historia yetu na kuielewa hatutakubali tena kurudi utumwani.

    ReplyDelete
  4. wewe unasema maneno ya kuupalilia ukabila wacheni maneno yasio na maana, Waarabu walitawala mpaka Bara na wakaanzisha ustaarabu wa kuvaa nguo, Kujua hiki nini na kufanya bishara za kubadilishana. Kama kweli unaujua utumwa sio wa kuandikwa, kwani wanunuzi wakubwa wa biashara hizo ni Wazungu waliokuja Zanzibar, kuona nirahisi kusafirisha na kuchagua waliowataka kwa Kazi zao. aliye kuwa hatii ambri ya kuuzwa ndio wanaouliwa au kuteswa. Je fkiria sasa utumwa bado upo unalilia kwenda Ulaya unajua unaenda kufanya nini huko si uleule utumwa umekuwa wa kileo tu. wachakuropoka.

    ReplyDelete