06 June 2011

Wawili wasakwa kwa mauaji Rukwa

Na Juddy Ngonyani,Sumbawanga

JESHI la Polisi mkoani Rukwa linawasaka watuhumiwa wawili wanaodaiwa kuhusika na tukio la mauaji ya mkazi wa Kijiji cha  Pito katika manispaa ya sumbawanga
Bw. Selestino Kayawaya (55).

Kwa mujibu  wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa Bw.Isunto Mantage, tukio hilo lilitokea mwishoni mwa mwezi uliopita ambapo marehemu alikuwa na mwenzake aliyetajwa kwa jina la Emmanuel Simwaka wakiwa njiani kurejea majumbani kwao kutoka matembezini.

Alieleza kuwa wakiwa njiani walivamiwa na watu wawili ambao walifyatua risasi na kumpata Bw.Kayawaya sehemu za tumboni hatua iliyomsababishia kuvuja damu nyingi na kisha kufariki dunia huku mwenzake akijeruhiwa kwa risasi mguuni.

Kamanda Mantage alisema kuwa mara baada ya watu hao kutenda kosa walitokomea kusikojulikana huku majeruhi wa tukio hilo wakikimbizwa katika hospitalini.

Alisema kuwa  chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana na hakuna mtu yoyote anayeshikiliwa  na jeshi hilo ila akasema uchunguzi unaendelea.

No comments:

Post a Comment