24 June 2011

Tuko tayari kupoteza mabilioni ya rada -Membe

Na Grace Michael, Dodoma

SERIKALI imesema iko tayari kupoteza mabilioni ya fedha yanayotakiwa kulipwa na Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza endapo haitakuwa tayari kupitisha
fedha hizo serikalini.

Fedha hizo ni pauni milioni 25 sawa na sh. bilioni 75 zinatakiwa kulipwa na
BAE kama tozo ya fidia ya mauzo ya Rada baada ya uchunguzi kubaini kwamba Tanzania ilizidisha malipo ya chombo hicho.

Akisoma kauli ya serikali bungeni jana, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Bernard Membe, alisema pamoja na kampuni hiyo kuwa na masikio lakini imeshindwa kusikiliza kilio cha wengi na imeonesha dharau ya wazi wazi dhidi ya serikali ya Tanzania.

Waziri Membe aliwaomba wabunge bila kujali itikadi zao kuungana na serikali katika msimamo huo kulinda heshima ya nchi.

Alisema ni aibu kwa kampuni ilikwapua fedha za walipa kodi kupanga tena matumizi ya fedha hizo na kwamba kitendo hicho kinadhihirisha jinsi inavyodharau watanzania jambo ambalo haliwezi kuvumiliwa.

Alitahadharisha kuwa serikali haitaruhusu Asasi za kiraia za Uingereza kuja nchini kama Kampuni ya BAE inavyotaka kufanya kwa kisingizio cha kutoa misaada kwa asasi hizo.

“Tanzania ni nchi masikini lakini haiko tayari kudharauliwa kiasi hicho, serikali yake, Taasisi zake na Asasi zake kutoaminiwa, kuruhusu hilo kufanyika ni kuruhusu kuibiwa kwa mara ya pili, hatutaruhusu asasi hizo kuingia hapa nchini,” alisema Bw. Membe.

Alisema ili kuhakikisha serikali inafuatilia suala hilo kwa umakini na kushinikiza fedha hizo kupitia katika mfuko wa taifa bunge limetuma timu ya watu wanne kwa lengo la kukutana na Kamati husika na kufanya mazungumzo na wabunge wa Bunge la Uingereza kuhusiana na suala hilo.

Kamati hiyo pia itakutana na viongozi wengine wenye ushawishi mkubwa nchini humo kwa lengo la kuwashawishi au kuishinikiza kampuni ya BAE kutoa fedha hizo kwa serikali ya Tanzania bila masharti yoyote.

Timu ya wabunge inaongozwa na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Bw. Job Ndugai, Bw. Mussa Zungu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, Bi. Angellah Kairuki Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala na Bw. John Cheyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali.

Waziri Membe alieleza bunge kuwa katika kushughulikia suala hilo tayari amefanya mazungumzo na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika kujua kama serikali ya nchi hiyo inaunga mkono msimamo wao au la.

Alisema Waziri huyo alimhakikishia kuwa  msimamo wa nchi hiyo haujabadilika na kuwa wanaunga mkono fedha hizo kurejeshwa kwa Serikali ya Tanzania kwa matumizi yaliyoanishwa.

Alisema kuwa serikali inashangazwa na uamuzi huo wa BAE wa kutaka fedha hizo zipitie kwenye asasi za nchini Uingereza kwa kuwa fedha hizo si za misaada kama kampuni hiyo inavyotaka kuuaminisha ulimwengu.

“Fedha hizi ni za tozo kwa fedha zilizokwapuliwa na BAE kutoka Tanzania, hatuko tayari kukubaliana na uamuzi wa BAE ambao una lengo kuiondolea heshima nchi yetu.

Una sura ya makusudi ya kuonesha kutoamini dhamira ya serikali ya Tanzania kutumia fedha hizo kama zilivyopangwa,” alisema Bw.Membe.

15 comments:

  1. Amma kweri mungu ametujaalia Ubinafsi. huyu jamaa kwa vile yeye amekuwa waziri basi anaweza kuzungumza hata mambo yasiyo na faida kwa taifa hili, kwani hiyo Rada ilinunuliwa kihalali? sasa serikali imekaa kimya haitaki kuwawajibisha waliofanya uhuni huo wa rada, ndio maana hawa wazungu wameamua kutulipa watanzania ambao ni masikini tunaonewa kila siku na wajinga wachache kama hataki pesa hizo basi ni yeye mimi kama mtanzania nazihitaji, labda zinaweza hata kufikikisha maji na barabara ya vumbi kijijini kwangu na hata hapa ninapoishi mjini maji hayajawahi kutoka mwaka wa saba sasa ETI TUPO TAYARI KUTEZA MABILIONI HAYA KULIKO KUZALILISHWA. KWANZA NAKTAKA MJUE KUWA MIMI KAMA MWANANCHI WA TANZANIA SIZALILIKI HATA KIDOGO KAZI KWENU MNAOONA KUWA ULAYA NDIO MALI KILA SIKU MWAENDA HUKO NA KUSOMESHA WATOTO WENU HUKO

    ReplyDelete
  2. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Bernard Membe, JEURI HIYO NI YAKO AU MMESHA WASILIANA NA MHESHIMIWA RAISI.
    ACHA UNAFIKI KWA WATANZANIA KUONYEHA UNAWAONEA HURUMA, ANZA KUWAWAJIBISHA ALIYEKUWA MWANASHERIA WA SERIKALI,WAZIRI WA MAMBO YA NJE,ALIYEPEWA TENDA KUNUNUA HIYO RADA WAKATI HUO.BAADA YA HAPO NDIO UJE KUOMBA TUWASHUGHURIKIE HAO BAE System.WEZI SI BAE SYSTEM TU, WALIANZA HAO WA NDANI BAADAYE WAKAWASHIRIKISHA WANJE.

    ReplyDelete
  3. Waingereza wanajua serikali yetu fisadi. Kurudisha hizo pesa serikalini ni kuziruhusu zikanunue vitu vingine vya anasa kwenye nchi nyingine kama vile Costa Rica ambako hamna atakaejua zilikoenda. Hivyo vyoo na miradi mingine ya elimu ije kusimamiwa na NGO za kiingereza ili wahisani wetu waamini kuwa juhudi zao za kuwahurumia watanzania zimezaa matunda

    ReplyDelete
  4. Membe hana akili timamu!

    ReplyDelete
  5. Watanzania tuache kulalamika tu bila kuchukua action. Kama kweli tunapinga Serikali yetu CORRUPT kutochukua tozo ya rada na badala yake zipelekwe kwenye NGOs za Kitanzania basi tutume emails kwa wingi kwenye address zifuatazo. I'm sure serikali za wenzetu ni SIKIVU na pesa hizo kamwe haitapewa serikali ya Tanzania. Tuma email KUPINGA kwenda address zifuatazo.

    Leonnie.foster@baesystems.com, info@ibe.org.uk, norman@normanlamb.org.uk

    ReplyDelete
  6. Wewe Membe tangia ukae serikali ya CCM haujaona kuwa ni fisadi mimi naunga watoe fedha kwa mashirika yasiyo ya Kiserikali zikiingia serikalini zitakwenda kwa mikono ya wachache na mafisadi. Serikali ya CCM imetufanyia nini labda kuiba kura ndilo imetufanyia. Msiwape serikali ngo

    ReplyDelete
  7. Waziri Membe wacha kulalamika,Nyie viongozi mmezidi kuingia mikataba mibovu na ndio maana hata hao wanaongia mikataba na serikali ya Tanzania wanawazarau kwa ajili ya madudu mnayoyafanya.Sasa mnalalamika kitu gani?Hata hao walioingia huo mkataba wa wizi wa fedha az walipa kodi hawajachukuliwa hatua yoyote ile.Na huyo aliyefungua akaunti ya mamilioni ya dola katika kisiwa cha Jersey hajaitwa na kuulizwa hizo fedha alizipata wapi na kwa biashara gani anayoifanya.Au anauza unga?.
    Anatakiwa aitwe na aeleze jinsi alivyo pata hizo fedha.Serikali imeshindwa kuchukuwa atua zozote mpaka leo mmebaki mnamtizima tu.Alafu mkiambiwa ukweli mnakasirika.Sasa mnazitelea macho hizo fedha.

    ReplyDelete
  8. Wewe membe na serikali mnayoiongoza ni mabwege kabisa! BAE wanawajua watu walotengeneza nao dili na serikali bado inawakumbatia na wengine bado wamo serikalini, lakini hamjawachukulia hatua yoyote so kwanini wasiwe na shaka km zitakuwa salama zikirudi! Serikali ya TZ ni too corrupt! kinyaaa, kichaaa, fidodidooo, serikali mwitu! Sasa Membe au Mende kama siyo Wembe unatakakutudanganya kwamba unauchungu, unalalamika eti nchi imedharauliwa na BAE, mimi nasema BAE hawajadharau nchi ila wameidharau serikali ya CCM, na haipo sababu kwa BAE kuheshimu serikali corrupt! Ivi wewe membe au raisi wako JK kama msingekuwa madarakani mngekuwa tayari kuheshimu serikali corrupt?. Unless mwenda wazimu, huwezi heshimu serikali corrupt! Hafu nawashangaa kweli serikali pamoja na mahakama ya uingereza kusema kulikuwa na wizi bado tu mko kimya kwa maafisa wa TZ waloshiriki, huu si uchizi! Ndiyo ni uchuzi na wala Membe usinitafsri ninadharau ila nasema ni uchizi tupu, serikali ya kijiwe tena cha wahuni!

    ReplyDelete
  9. Hawajawadharau mmejidharaurisha wenyewe. MMMMMMHHHH MNANUKA RUSHWA

    ReplyDelete
  10. KWANZA MEMBE MAFISADI WANAKUTUMIA SANA, HIYO WIZARA YAKO NJIA YA KUFANYIA UFISADI, TUNAWAAMBIA KUWA MWISHO WENU UNAKUJA!

    ReplyDelete
  11. Wee Maembe kweli umeoza kabla hujafika sokoni! yaani wezi bado wako ndani ya nyumba unataka kuwaletea TV waliyoiba ikakamatwa kwa jirani mwema? bora tv ikae hukohuko mpaka tuwatimue wezi wetu ndani ya nyumba! Hao BAE wakomae kama ni kudhalilika mmejidhalilisha wenyewe kwa wizi na kulea wezi. Yaani utembee kaptula umening'iniza makalio nje nje halafu watu wakicheka unalalama ooo wananidhalilisha! kumbe uko hivi na uraisi usithubutu kugombea!

    ReplyDelete
  12. You need to be just a little intelligent bwana Membe! Hizo fedha zilifikaje huko?you don't deserve to be trusted my aspiring president!
    Infact trust huwa inajengwa is not just there.
    You and your fellows are not trustwothy. Kwani nuke Ndio milgundua huo Wizi na kui task serikali ya uingereza AMA ni wao wenyewe?
    Si serikali yenu hiyo hiyo imesema chenge Hana hatia?
    Shame on you....

    ReplyDelete
  13. Hey Membe ukali unaojaribu kuuonyesha hautusaidii chochote.Hii serikali ya JK imejaa viongozi wasio na busara,walioja ubinafsi na uwezo mdogo wa kufikiri na kutenda.Ndiyo maana mnakimbilia hoja dhaifu zisizo na tija kwa TAIFA.Eti bora tuzikose hela zetu.CCM is totaly exhousted,mmechoka pisheni watu wenye bongo zinazochemka wenyeuchungu na nchi hii watuongoze.

    ReplyDelete
  14. Huwa naishangaa sana serkali yetu, tunapenda kutafuniwa. BAE imekiri kwamba rushwa ilitolewa na ushahidi ukapatikana na adhabu imetolewa kwa BAE. Kama kweli tuna uchungu wa hizo hela kwa nini tunawahifadhi mafisadi waliokula fedha hizo. Tunapenda tupewe fedha tu. Viongozi wetu hamna uchungu na nchi hii.

    ReplyDelete
  15. tunataka fedha jetu, fedha za watanzania, nataka mimi, ah tunataka aki ..ya mongo..mi silali uchingiji navowafikiria watanzania wanavo zaraurika, mi sikubali, taka fedha zetu uko, mh za watanzania...mi nataka nijenge chule.dodo, nataka jenge choo na mdawati dodo..mi chikubali ili walimu wapate raha, mi nauchungu nao..wanichi kwa tabu...feja tulizonazo hazitoshi..ila zilizoibiwa zinatosha kuanzia.

    wameiba wao..huku hakuna fichadi wao wameiba..huku kuna fichadi...mizi ni pande moja ,kwetu hakuna chi watu safi..taka feza zetu.
    chikubali.

    ReplyDelete