24 June 2011

Jaji amwaga chozi mbele ya Tume

Na Salim Nyomolelo

SAKATA la baadhi ya viongozi wa umma kueleza sababu za kushindwa kujaza na kuwasilisha fomu za mali na madeni kwa mwaka 2010 imezidi kuibua mapya baada ya
Jaji wa Mahakama Kuu, Kitengo Cha Ardhi Atuganile Ngwala, kuangua kilio mbele ya Baraza la Maadili ya Tume hiyo.

Tukio hilo lilitokea jana wakati Jaji Ngwala akijieleza mbele ya Baraza hilo chini ya Mwenyekiti wake Jaji Damian Lubuva,
kuhusu sababu zilizomfanya ashindwe kutekeleza wajibu wake na kuwasilisha fomu hizo kwa wakati.

Katika lalamiko hilo namba 49/2011 Jaji Ngwala alitakiwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo aieleze tume sababu za kushindwa kujaza fomu hizo na kwa nini asichukuliwe hatua za kisheria jambo lililomfanya aangue kilio.

Huku akiwa analia Jaji Ngwala hakutafuna maneno wala kutumia maneno ya kisiasa badala yake alikiri kufanya kosa hilo na kuliomba balaza kumuonea huruma kutomfukuza kazi.

Alitaja sababu za kuomba huruma ya Baraza hilo kuwa ni pamoja na kutunza familia na maisha yake yote kutegemea kazi hiyo.

Kukiri kosa hilo moja kwa moja kulifanya balaza hilo kutoendelea kumuuliza maswali yoyote kama ilivyokuwa kwa waliomtangulia amboa walikuwa wakitoa sababu mbalimbali.

Mwenyekiti wa baraza hilo alimweleza Jaji Ngwala kuwa watazingatia maombi yake pindi watakapofanya uamuzi wa adhabu.

Hata hivyo kitendo cha Jaji huyo kukiri kosa hilo bila kuzunguka na kuangua kilio mbele ya baraza kuliwafanya watu waliohudhulia baraza hilo kutoa maoni tofauti.

Baadhi yao walifurahishwa na kitendo hicho na kuwataka viongozi wengine kuiga mfano wake ili kuokoa muda wa kufanya shughuli zingine za kujenga taifa huku wengine wakidai alifanya kosa kwa kukusudia.

Kwa mujibu wa sheria namba 13 ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba ya mwaka 1995, ukiukwaji wa maadili utashababisha mhusika kuchukuliwa hatua ikiwemo kufukuzwa kazi.

Adhabu nyingine kwa mujibu wa sheria hiyo ni kuonywa na kupewatahadhari,kushushwa cheo, kusimamishwa kazi pamoja na kumshauri kiongozi kujiuzulu wadhifa unaohusu ukiukwaji huo.

Lengo la sheria hiyo ni kuhakikisha viongozi wa umma wanafuata maadili kwa lengo la kuweka msingi wa kuongeza imani ya wananchi kuhusu uadilifu wa viongozi wa umma.

Baadhi vibwagizo vilivyowai kujitokeza katika sakata hilo ni pamoja na viongozi kutaja msongo wa mawazo, mgogoro wa maeneo wanakotoka na shetani kuwa chanzo cha kuwafanya washindwe kujaza na kuwasilisha fomu hizo kwa wakati.

5 comments:

  1. shelia irekebishwe ili wananchi wapewe uwazi wa kutaja malili za viongozi wao wanapoona wamedanganya kwani wananchi wanawajua zaidi lakini kwa shelia ya sasa ni vgumu mwananchi anapoona viongozi wanadanganya kuusu mali wanazomiliki.

    ReplyDelete
  2. Na wale waliojilimbbiki mali nyingi bila kueleza wamezipataje wanyanganywe mali hizo na hela zikanunua madawati, dawa na kuongeza mishahara ya waalimu na madaktari. Nyingi zitakuwa ni fedha za ufisadi, uuzaji wa unga na uuzaji wa nchi

    ReplyDelete
  3. Machozi siyo kinga! Nchi hii ifikie mahali ambapo machozi yatumike kwenye vilio na siyo sehemu ya kuomba msamaha. Kukomesha hilo ni kufanya maamuzi tu la sivyo baraza la maadili litatawaliwa na vilio. Jaji mzima unasimamia sheria na taratibu mbalimbali za nchi halafu unatuzuga hapa na machozi ya samaki! Mi sijawahi kuona machozi ya samaki!

    ReplyDelete
  4. Safi sana kila baraza na tume likifanya kazi hivyo tutafika mbali kwani Tanzania bila uzembe inawezekana.

    ReplyDelete
  5. huo ndio usanii wa hawa jamaa wanapo ona tonge linataka kudondoka.

    lile ni chozi la kisanii..we acha tu!!

    ReplyDelete