Na Mwandishi Wetu
WAKATI timu ya Simba, ikisaka ushindi katika mechi ya Kombe la Kagame Castle, Ocean View watakuwa wakitafuta pointi moja waweze kutinga hatua ya
nusu fainali ya michuano hiyo leo.
Lakini, mashabiki wa soka wanajiuliza kama Simba itaweza kuisimamisha Ocean View.
Timu hiyo, zitajitupa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, kuwania pointi tatu katika mechi ya Kombe la Kagame zilizoanza mwishoni mwa wiki jijini hapa.
Simba ambayo katika mechi ya kwanza ilitoka suluhu na Vital'O ya Burundi, ikiwa ya tatu katika msimamo wa Kundi A linaloongozwa na Zanzibar Ocean View, ikifuatiwa na Vital'O yenye pointi nne.
Katika kundi hilo timu za Etincelles na Red Sea hazina pointi, hivyo kuwa za mwisho.
Kutokana na kiwango cha soka kilichooneshwa na Ocean View kwenye michuano hiyo, kinaweza kuwaweka Simba katika nafasi ndogo ya kusonga mbele hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Simba itakuwa ikihitaji pointi tatu muhimu katika mchezo wake wa pili wa kundi hilo, lakini ikiteleza itakuwa imejiweka kwenye nafasi ngumu kwani itakuwa imebakiza mechi mbili, dhidi ya Etincelles na Red Sea.
Kwa upande wa Ocean View, wao wameshinda mechi zote mbili za mwanzo hivyo wanahitaji sare ya aina yoyote kutinga hatua ya robo fainali na kuziacha timu nyingi katika kundi lao zikitafuta nafasi ya pili na timu yenye matokeo bora itakayokuwa ya tatu.
Raha ya mchezo wa leo, itakuwa kwa timu ya Simba kusaka ushindi katika mchezo huo, huku Zanzibar Ocean View ikitafuta heshima na kuthibitisha ubora wao.
Ocean View, kabla ya kuanza kwa michuano hiyo waliweka wazi kuwa, wanakwenda kushindana na wamefurahi kupangwa kundi moja na Simba.
Kikosi hicho kilisema, lengo lao ni kuwahakikishia mashabiki wa soka kuwa, Zanzibar wako juu kisoka kuliko Tanzania Bara.
Lakini kwa upande wa Simba, wao baada ya kutoka suluhu dhidi ya Vital'O, Kocha Mkuu Moses Basena, alisema kuwa watajipanga vizuri kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mechi hiyo.
Basena alisema wana matumaini ya kuibuka na ushindi katika mechi hiyo kwao na tayari wachezaji wake wameahidi kujituma uwanjani.
Mechi hiyo itakuwa ya pili, ambayo itaanza saa 10 jioni, ikitanguliwa na mchezo kati ya Red Sea ya Eritrea na Etincelles ya Rwanda.
viva la Ocean View watoto wa kizenji muweni simba huyo leo
ReplyDelete