08 June 2011

Ole Millya kuvuliwa uanachama CCM

Na Said Njuki, Arusha

MGOGORO ndani ya CCM Mkoa wa Arusha umeshika kasi mpya baada ya Kamati ya Usalama na Maadili na Kamati ya Siasa za chama hicho mkoa kudaiwa kumvua
uanachama Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) Mkoa, Bw. James Ole Millya.

Pia vijana wengine watano wa umoja huo wanaodaiwa kuwa vinara wa mgogoro nao watakumbwa na rungu hilo baada ya kamati hizo kutoa mapendekezo ya kufukuzwa uanachama kwa kitendo chao cha kushadadia kuondoka kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Bi. Mary Chatanda.

Habari kutoka ndani ya vikao hivyo ambazo zimethibithswa na  baadhi ya viongozi wa chama hicho kwa sharti la kutotajwa majina, zimedai Kamati hiyo iliyoketi mwishoni mwa
wiki ilitoa mapendekezo yake kuwa Mwenyekiti huyo anayedaiwa kuwa kinara wa mgogoro huo pamoja na vijana hao avuliwe madaraka.

Vyanzo hivyo vilidai kuwa kikao cha kamati hiyo pia kilihudhuriwa pia na wajumbe kutoka Kamati ya Maadili ya Taifa ikiongozwa na Kanali Mhando na wajumbe wawili kutoka UVCCM Taifa ambao ni Bw. Seif Malinda na Mzee Mipoko kilichokaa kuanzia asubuhi hadi usiku wa manane.

Mapendekezo hayo baada ya kuridhiwa na wajumbe hao yalifikishwa  katika Kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa, kilichofanyika siku moja baadaye na kuridhia mapendekezo hayo, hivyo kusubiri kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa kinachotarajiwa kukutana Jumamosi wiki hii kwa ajili ya maamuzi zaidi.

Vyanzo hivyo vimewataja majina ya vijana watano kati ya 11 waliohojiwa siku hiyo,  kufuatina mgogoro unaotokana na falsafa mpya ya CCM ya kujivua gamba ambapo makada waandamizi wa chama hicho, aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, Mbunge wa Igunga, Bw. Rostam Aziz na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Bw. Andrew Chenge wanashinikizwa kuachia ngazi zao.

Baadhi ya sababu zilizoelezwa za kuwajibika kwa Bw. Milly
Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Bi. Mary Chatanda.

Wadadisi wa mambo ya siasa mkoani hapa wameeleza ya kuwa iwapo hatua hiyo ya kuwavua uwanachama vijana hao itatekelezwa itazidi kuchochea na kupanua mgogoro huo ambao ungeweza kutatuliwa kwa njia za kidiplomasia na kupunguza ufa ndani ya chama hicho.

Lakini kundi lingine linatoa matamshi mazito dhidi ya makada hao na kueleza kuwa wanapaswa kuwajibika kwa tuhuma zinazowakabili na kwenda mbali zaidi na kumtaja Bi. Chatanda ni lulu ya chama mkoani hapa na hapaswi kuondoka.

5 comments:

  1. Mbona ukweli unapotoshwa jamani? Chanzo cha mgogoro huu kilianza tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu 2010 na mgombea wa CCM Dr. Batilda kushindwa na mgombea wa Chadema.
    Ule ukweli Mary Chatanda alihusika 100% na kushindwa kwa CCM Arusha. Hawa wamama wawili Batilda na Chatanda ni paka na mbwa. Kwa hiyo Chatanda alifanya juu chini kulipiza kisasi na akafanikiwa. Chatanda huyo huyo alichota mabilioni akaenda Jimbo la Karatu badala ya kujenga akazidi kubomoa Jimbo la Karatu nalo hilooooo likachukuliwa na Mgombea wa Chadema. Kama ni kuwajibishwa ule ukweli wa Mwenyenzi Mungu hata Chatanda anastahili kuwajibishwa. Kauli zake tu zinatosha kuigawa CCM kwani ni za kibabe sana.

    ReplyDelete
  2. Ndugu yangu Anonymous, asante kwa kuusema ukweli. Ila ndugu yangu si unajua mama huyo ni wa wenyewe? Unakumbuka aliposababisha mauaji Makamba akawasifu Polisi akisema wamefanya kazi yao? Unakumbuka mama huyo aliwakashfu Maaskofu na bado akaonekana kutenda mema hadi pale Malekela alipowaomba radhi Maaskofu? Unakumbuka alihamasisha dhehebu fulani la dini kujibu Maaskofu?

    Yote hayo ukiyakumbuka, basi, elewa Ole Millya na wenzake wako matatani/

    ReplyDelete
  3. ukweli ni kwamba huyo mama hatufai kabisa Arusha, kwanza ni mropokaji, ni mtu ambaye hana point ni kama mzigo tu. pia ni mchochezi vibaya mno. mauaji ya Arusha yeye anastahili kuwa wa kwanza kwenda jela. kweli mimi nikisikia jina la Mary Chatanda nasikia kichechefu.

    ReplyDelete
  4. ndio mambo ya SIASA za unafiki

    ReplyDelete
  5. hicho ni chakula cha watu hivyo lazima kiharibu vyakula vingine vionekani havifai ili chakula chake kiwe kizuri; ila yana mwisho tuuuuuuuu.

    ReplyDelete