01 July 2011

Mchumba wa Dkt. Slaa akanusha matusi dhidi ya mbunge

 Na Flora Amon

MCHUMBA wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Willibrod Slaa, Bi. Josephine Mashumbusi, amekiri kumtumia ujumbe mfupi wa simu (SMS) Mbunge wa viti Maalumu Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Stella Manyanya, huku akikanusha kumtukana.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Bi.Mashumbusi alisema kabla ya mbunge huyo kumtuhumu kuwa ametumiwa ujumbe wa matusi angefafanua kwanza kwa kusoma ujumbe aliotumiwa.

Alisema hawezi kukataa kumtumia mbunge huyo sms lakini haukuwa wa matusi kama alivyodai.

"Ujumbe wangu niliandika kuwa "aache kuwa mshabiki bali aongelee uhalisia na nadharia kwa sababu wananchi walipo kijijini kwake ni masikini na wana maisha magumu,"hilo ni tusi? alihoji Bi.
Bi.Mashumbusi.

Alisema yeye alishaenda kijijini alikotokea Mwandisi Manyanya ambapo wananchi wake wana maisha magumu hali ambayo yeye ilimtia uchungu.

Alisema mbunge huyo akisimama kuchangia hoja achangii kama mtu mwenye wananchi walio na maisha magumu bali yeye ni mshabiki hali ambayo inamshgaza.

"Ninavyoelewa wanawake wasomi wanajadili mambo ya kisomi, lakini yeye akiwa katika kujadili hoja hajadili
kama mwenye uchungu na wananchi wake bali anajadili ushabiki kitu ambacho kwa sasa kimepitwa na hakileti maendeleo,"alisema.

Aliongeza kuwa jinsi anavyomjua mbunge huyo laiti kama angekuwa amemtukana basi angemfikisha katika vyombo vya sheria.

Akichangia bajeti ya waziri mkuu 2011/2012 Mwandisi Manyanya alisema alipokea ujumbe mfupi wa matusi kupitia simu yake ya mkononi kutoka kwa
Bi.Mashumbusi.

13 comments:

  1. Udakuudaku na upekupeku then unajiita enginia?? Hivi ulipita wapi hiyo degree ya uengeneer, huweza tafsiri, ukatafakari then ukajudge?? Hayo mambo yenu ya mipasho si ya kuleta bungeni, sisi tunakufa njaa, maisha magumu kila kukicha heri ya jana, leo unapata nafasi ya kuingia humu jengoni badala ya kufanya tulichokutuma unaanza kutueleza jinsi na ni mesegi ngapi unapata kutoka kwa mashoga zako?? Huna haya!!!!! Watu wa iana yako kule cuba hata simu hawashiki wanawapa masekretari zao kwani saa zote maengineer ni kazi kwa kwenda mbele. Ngoja tuone uchaguzi ujao kama utapata tena hii favour ya kuingia huku... Acheni fedheha fanyeni kazi kwanza haki sawa baadae!!!!

    ReplyDelete
  2. HAYO NI MASUALA YA KIKE YANGEMALIZWA BILA KUFIKA KWENYE MAGAZETI. KAMA KWELI MH. MANYANYA NI INJINIA TUTAKUWA NA WASIWASI NA HUO UINJINIA WAKE. ATUMIE ELIMU YAKE KUMALIZA VITATIZO VIDOGO VIDOGO SIO KUYAKUZA YAONEKANE NI MASUALA MAZITO ANAKUWA KAMA SI MSOMI!! SHUGHULIKIA MATATIZO YA WANANCHI WAKO YA SIO KUWA MDAKU MDAKU WA MTAANI NA KUMBE WEWE NI MH.MBUNGE

    ReplyDelete
  3. Mhe. Manyanya unatuboa uchaguzi ujao tunakutosa. Ukielezwa ukweli unasema umetukanwa. Degree yako ni ya chuo gani? Si ajabu na wewe ni mmja wa wale mafisadi wa elimu waliosoma katika vyuo visivyotambulika

    ReplyDelete
  4. Ingiza manyanya umeingizwa vitu vya hovyo; hata elimu uliyosoma haikusaidii. basi elimu yako umefoji kama ya Nape

    ReplyDelete
  5. unbelivable! engineer? how comes you use parliamentary microphone to speed nonses.
    Are they vital to your people in Songea? Engineer wa Nyanya pole sana kwa mipasho.

    ReplyDelete
  6. Muheshimiwa mzima halafu injinia unaongea pumba mjengoni? Shame upon you, kama umetumiwa sms ya matusi; fuck it off, sisi inatuhusu nini

    ReplyDelete
  7. Sasa huyu mchumba wa Slaa ataolewa lini? Maana ni miaka miwili sasa kila siku tunaambiwa ni mchumba!

    ReplyDelete
  8. inginia matomato ama kweli umefulia yaani unakwenda mjengoni na kuanza kujibu utumbo badala ya kuongea sera zinazoleta tija nami pia na wasiswasi huo uinginia wako km ni wa halali au wa kichinachina?

    Ongea vya maana and don't ever speak shit again.

    ReplyDelete
  9. YAANI HUYO SLAA NA UMRI WOTE HUO ALIKUA HAJAOA[ANA DO TU HOVYO] NDIO KWANZA ANA MCHUMBA,YAANI WATANZANIA TUKUBALI KUONGOZWA NA 'BACHELOR',HATUTAKI HATA KUSIKIA MAWAZO YAKE TENA! AOE!YAANI HUYO SLAA NA UMRI WOTE HUO ALIKUA HAJAOA[ANA DO TU HOVYO] NDIO KWANZA ANA MCHUMBA,YAANI WATANZANIA TUKUBALI KUONGOZWA NA 'BACHELOR',HATUTAKI HATA KUSIKIA MAWAZO YAKE TENA! AOE!

    ReplyDelete
  10. Dr. Slaa alikuwa Padre wa Katoliki ndio maana alichelewa kuoa, ingawa tunasikia alikuwa anaishi na suria mbunge wa viti maalum Hanang

    ReplyDelete
  11. KWA HIYO PADRE NDIO HANA MATAMANIO YA KIMWILI? HALI CHAKULA? HANYWI MAJI? AU TUNAZIBANA MACHO NA MASIKIO TU.KWANZA UMESHASEMA ALIKUA ANAISHI NA HUYO MBUNGE,KWA NINI ASIOE KABISA KULIKO KUENDELEA KUFANYA MAASI?
    *TUJIULIZE JAMANI TUSIFUATE MKUMBO TUA? HANYWI MAJI? AU TUNAZIBANA MACHO NA MASIKIO TU.KWANZA UMESHASEMA ALIKUA ANAISHI NA HUYO MBUNGE,KWA NINI ASIOE KABISA KULIKO KUENDELEA KUFANYA MAASI?
    *TUJIULIZE JAMANI TUSIFUATE MKUMBO TU

    ReplyDelete
  12. NI AIBU KUJADILI MAMBO YA WATU, NYIE MWAISHIJE MPO SAWA..NAWAULIZA MPO SAWA, NINYI NA NYUMBA ZENU.TWASIKIA KIONGOZI NUMBA MOJA ANA TOTOZI KIBAO..DATA ZIPO.

    DALILI YAKUKOSA ELIMU NI KUJADILI UMBEA.

    ReplyDelete
  13. WEWE MWAANDISHI WA HABARI HIZI WACHA KUMUITA HUYO MALAYA MCHUMBA. HIVI MNAELEWA MAANA YA UCHUMBA? HIVI DINI YENU YA KIKIRISTO INARUHUSU HAYO YA MTU KUKAA NA MALAYA MPAKA AKASHIKA MIMBA? MNAMUITA MCHUMBA KUHALALISHA UZINIFU WA SLAA NA HATA MAPADRI NA MAASKOFU WANAITA HIVYO. ACHENI UJINGA HUO.MCHUMBA INA MAANA NA THAMANI KUBWA? ZEE KAMA HILO SIJUI LINA TATIZO GANI? NI MAPESA YETU HAYO YANAWAFANYA HATA HAWA MALAYA WAKAKIMBIA WAUME ZAO. NA HUYO MJINGA WA HAPO JUU ANAYESEMA KIONGOZI NAMBA MOJA ANA TOTOZ KIBAO HAKUNA KIONGOZI WETU WA DINI YA KIISLAMU ANAYEWEZA KUSEMA HADHARANI HAYO NI MASUALA YAKE BINAFSI ATAAMBIWA TU ANATENDA DHAMBI. HUYO KABEBA MKE WA MTU NA ANAKAA NAE KINYUMBA NDIO AWE RAIS WETU AMA KWELI WATZ HAMNAZO

    ReplyDelete