Na Grace Michael, Dodoma
SERIKALI imetakiwa kuwa makini na kukanusha taarifa za upotoshaji wa taarifa zinazotolewa na nchi jirani ya Kenya kuhusiana na Mchungaji Ambilikile Masapila maarufu
kama ‘Babu’ kuwa anapatikana kusini mwa nchi hiyo kwa lengo la kujitangaza.
Mchungaji Masapila ambaye hivi karibuni alipata umaarufu mkubwa kwa kudaiwa kutibu magonjwa sugu ya kisukari, Ukimwi, kansa na mengine mengi.
Hayo yalisemwa na Mbunge wa Ngorongoro, Bw. Kaika Terere (CCM) wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Waziri Mkuu, ambapo alitumia mwanya huo kuelezea umaarufu wa mchungaji huyo na namna alivyozawadiwa gari na mmoja wa wagonjwa kutoka Malawi aliyenufaika na matibabu hayo.
Bw. Terere alisema kuwa umaarufu wa Mchungaji huyo umeisaidia Loliondo kujulikana dunia nzima, hatua inayoifanya Kenya kutumia jina lake kwa lengo kujiingizia
mapato, kuwa anapatikana kijiji cha Samunge kilichopo Kusini mwa Jamhuri ya Kenya.
Alisema upotoshaji huo ambao umekuwa ukifanywa makusudi umewafanya wagonjwa wengi wanaotoka katika mataifa mbalimbali duniani kusafiri hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa vya Jomo Kenyatta, Nairobi au Kiwanja cha Ndege cha Williason badala ya kushukia Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA).
“Imefika mahali wanadanganya wagonjwa kuwa wakishuka KIA hadi Samunge ni kilometa 800, lakini wakishuka Nairobi au Williamson wakapita mji wa Narok hadi Samunge ni kilometa 45 tu wakati ni uongo, kwani kuna zaidi ya kilometa 300 kufika Samunge.
"Hivyo kunapotokea taarifa kama hizi, serikali ichukue hatua na kuzikanusha mara moja,” alisema Bw. Terere.
Alisema endapo Samunge ingekuwa nchini Kenya, magari ya kutoka Tanzania yasingeruhusiwa kuingia lakini kwa kuwa kijiji hicho kiko Tanzania wananchi wa nchi hiyo jirani wanaingia na magari yao bila tatizo lolote.
“Hivi kweli hiki kijiji kingekuwa kwa hawa wenzetu sidhani kama tungeweza kuingiza hata magari yetu, tungekuta magari yao yako mpakani kwa lengo la kuwavusha, hivyo ni lazima tuwe wakali katika mambo yanayoleta sifa kwa taifa
hili,” alisema.
Akielezea zawadi ya gari, alisema kuwa Mchungaji Masapila alikabidhiwa gari hilo aina ya Toyota Hilux Pick Up lenye usajili wa namba BL 9238 lililotolewa na mgonjwa huyo ambaye hakumtaja jina, lakini akaeleza ni raia wa Malawi anayeishi Blantyre.
Alisema kuwa gari hilo kwa sasa linatumika kwa ajili kufuata dawa ambayo sasa inapatikana eneo la mbali kidogo kutokana na kumalizika katika maeneo ya karibu kutokana na
wingi wa wagonjwa.
Mbunge huyo alisema ingawa suala la dawa hiyo kuponya au kutokuponya ni la mgonjwa mwenyewe kutoa ushuhuda, lakini dawa hiyo imeleta sifa kubwa wilaya ya Ngorongoro na kuifanya kujulikana ndani na nje ya nchi.
“Mimi nawaomba wale wote waliokunywa dawa ya Babu waendelee kupima afya zao mara kwa mara kama ambavyo serikali imekuwa inasisitiza na napenda kuwapongeza sana
wabunge wenzangu waliopo humu ambao walifika Samunge kupata kikombe cha Babu,” alisema Terere.
your right Terere bigup kwa maendeleo ya TZ
ReplyDeleteChochote chenye mwanzo kina mwisho. huyo babu , hatujaona chochote cha ajabu kutoka kwake, isipokuwa ikiwa mbunge anasema basi tumuamini.lakini elimu ni muhimu kuliko kila kitu.
ReplyDeleteMimi binafsi nawajuwa wagonjwa wawili kutoka arabuni waliokwenda kwa Babu kwa matibabu na hapana hata mmoja aliyepata ahweni baada ya miezi miwili ya matibabu
ReplyDeletehayo na hali zao zimekuwa zikizidi kwenda chini.