28 June 2011

Katibu CCM atema cheche dawa za kulevya

Na Andrew Ignas

KIONGOZI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Saad Kusulawe, amewataka viongozi wa serikali kutekeleza kaulimbiu ya
kupiga vita dawa za kulevya kwa vitendo ikiwemo kuwachukulia hatua kali viongozi wote wa juu wanaojiusisha na biashara hiyo haramu.

Akizungumza na mwandishi wa haabri hizi jana Bw. Kusulawe ambaye ni Katibu CCM wa Wilaya ya Temeke alisema serikali inatakiwa kuadhimisha siku hiyo ya kupambana na dawa za kulevya kwa vitendo na siyo kwa kutamka tu maneno.

"Serikali haitaweza kutokomeza biashara ya dawa za kulevya nchini pasipokuwapo na ushirikiano wa kina, kuna baadhi ya polisi wanashiriki katika suala hilo,"alisema Kusulawe.

Alisema jitihada za pekee zinazofanywa na Rais wa Jakaya Kikwete, haziwezi kumaliza vita hivyo na kupambana na waingizaji na wauzaji wa dawa za kulevya nchini.

Hata hivyo alitoa rai kwa mamlaka ya usafiri wa majini kuhakikisha wanafanya misako ya mara kwa mara wa mizigo ya biashara za magari.

Alisema hivi karibuni serikali ya Kenya ilifanikiwa kuwatia mbaroni baadhi ya wafanya biashara hao wakijiusisha na biashara hiyo harama.

Wakati huo huo ameutaka uongozi wa Jeshi la Polisi kumchukulia hatua za kisheria polisi wa Mwembe Yanga kwa kile kinachodaiwa kuwalinda wahalifu wanaokaa katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment