*Ataka liwe la kwanza kunadiwa, kutolea mfano
*Amtaka Spika atenganishe fomu za posho, mahudhurio
*Bajeti yapita, Mkulo akubali kupunguza bei ya mafuta
Na Waandishi Wetu, Dodoma, Dar
KATIKA hatua inayoonesha Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutaka kupunguza matumizi ya serikali na kuongeza fedha kwenye maendeleo ya nchi, Kiongozi wa Kambi hiyo, Bw. Freeman Mbowe, amerejesha gari la serikali aina ya Toyota Land Cruiser 'shangigi' ili lipigwe mnada.
Mbali na hiyo pia kambi hiyo imemwandikia rasmi Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah, kumtaka atenganishe fomu kwa ajili ya mahudhurio na orodha ya kuchukua posho ili wanaozichukua wafahamike.
"Kuhusu magari, kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB) Mhe. Freeman Mbowe, ameamua kurejesha gari yake aina ya “Shangingi” alilopewa na Bunge ili liwe la kwanza kupigwa mnada. Tunawataka wabunge wengine waunge mkono hoja hizi kwa masilahi ya wananchi na taifa kwa ujumla," alisema Bw. Mbowe.
Bw. Mbowe ambaye alizungumza baada ya bajeti ya serikali kupitishwa huku hoja yao ya kupunguza posho vikao kutupwa, alieleza kuwa lengo kuu la hatua hiyo ni kusisitiza lengo la kambi yake kutaka serikali kuongeza fedha hizo katika bajeti ya maendeleo.
Lengo lingine kwa mujibu wa Bw. Mbowe ni kutaka kuipunguzia serikali mzigo, kisha fedha hizo kuongezwa katika bajeti ya maendeleo ili kumpunguzia ukali wa maisha Mtanzania wa kawaida kwa kuboresha miradi ya maendeleo yanayosuasua kwa sasa kwa maelezo kua 'sungura ni mdogo'.
Pia taarifa hizo ilitoa ufafanuzi kuhusu sababu ya kambi yake kukataa kuunga mkono bajeti ya serikali ya sh. trilioni 13.
"Pamoja na Bajeti ya Serikali kukubali na kuzingatia baadhi ya hoja zilizotolewa na wabunge wa Kambi ya Upinzani, tuliamua kupiga kura za HAPANA kwenye mapendekezo hayo ya serikali kutokana na sababu muhimu," alisema Mbowe katika taarifa yake.
Alitaja baadhi ya sababu hizo kuwa ni pamoja na kutokubaliana na hoja yao kuhakikisha magari yote aina ya “Mashangingi” yanayotumiwa na viongozi na watumishi wa umma yauzwe kwa mnada ndani ya miezi sita na viongozi hao wakopeshwe magari kwa ajili ya kufanya majukumu yao mbalimbali.
Serikali kutokubaliana na hoja ya kufuta/kupunguza misamaha mikubwa ya kodi ambayo Makampuni ya Madini yanapata ili kuhakikisha kuwa serikali inapata mapato kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.
"Serikali imekataa kuingiza pensheni kwa ajili ya wazee wote nchini ya sh. 20,000 kila mwezi kuwapunguzia ukali wa maisha wazee wetu," alisema Bw. Mbowe.
Bajeti yapita
Kabla ya tamko la Bw. Mbowe, Bunge lilipitisha bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2011/2012 ya sh. trilioni 13.5 huku ikubaliana na ushauri wa kupunguza kodi za mafuta ya dizeli na mafuta ya taa na kutolea ufafanuzi suala la posho ambalo limezua gumzo.
Katika kura zote zilizopigwa kupitisha bajeti hiyo, wabunge 81 walisema Hapana, huku 234 wakiunga mkono. Wabunge 34 hawakuwepo bungeni.
Hatua hiyo ilifikiwa jana mjini hapa baada ya mawaziri wa Wizara ya Fedha kujibu hoja zilizokuwa zimeibuliwa na wabunge kutokana na bajeti hiyo.
Katika majumuisho yake Waziri wa Fedha, Bw. Mustapha Mkulo, alisema kuwa katika suala la mafuta serikali imekubaliana na ushauri wa Kamati ya Fedha na Uchumi na kufanya marekebisho katika viwango vya ushuru kwenye mafuta ya taa na dizeli na
kupunguza tozo zinazotolewa na mamlaka mbalimbali katika mafuta.
Alisema kuwa katika kurekebisha ushuru katika mafuta ya dizeli imepunguza kodi ya sh 100 na tozo kwa sh 224 kwa lita huku wakisubiri ushauri wa Ewura kuhusu punguzo kwenye mafuta ya taa.
Alisema tozo hizo zilikuwa zinachangia upandaji wa bei ya mafuta na kusababisha upandaji wa gharama za maisha.
Alisema hatua ya kupunguzwa kwa kodi na tozo hizo itasaidia kuondoa ushawishi wa kuchakachua ambapo ushuru wa mafuta ya taa utarekebishwa baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) kutoa ushauri kwa serikali baada ya kufanya hesabu na kuona ni namna gani itasaidia katika kumaliza tatizo la uchakachuaji na kuondoa kichocheo cha kukwepa kodi.
Kauli kuhusu posho
Bw. Mkulo alisema kuwa suala la posho ambalo limerindima katika vyombo vya habari takribani wiki nzima limekuzwa kutokana na
matumizi ya takwimu zisizo sahihi.
Alisema kuwa suala posho alilisoma kwenye hotuba yake katika ukurasa wa 50-54 ambayo inasema itapunza posho mbalimbali sizizo na tija, safari sizizo na tija, semina na warsha zisizo na tija.
Alisema kuwa jumla ya posho zote zinazotolewa kwa mwaka ni sh. bilioni 312 na sio sh. bilioni 980 kama ilivyodaiwa na upinzani.
Alisema kuwa posho za vikao kwa serikali nzima ni sh. bilioni 25.68 na kati ya hizo, wabunge wanatumia sh. bilioni 4.92 hivyo kama posho za vikao zitafutwa serikali itaokoa jumla ya sh. bilioni 4 tu ambazo zinatumiwa na wabunge.
Alisema kuwa kutokana na takwimu hizo wabunge wanaweza wakapima wenyewe.
Akizungumzia suala la matumizi mabaya ya fedha za serikali kama ilivyooneshwa katika taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Fedha za Serikali, alisema kuwa serikali itaendelea kuzingatia ushauri unaotolewa na CAG ili kuimarisha nidhamu ya utunzaji wa fedha za umma.
Alisema kuwa pamoja na yaliyooneshwa na CAG lakini utunzaji wa fedha umeimarika na akaahidi kuwa serikali itaendelea kuutumia ushauri huo ili matumizi ya serikali yazingatie taratibu.
Shukurani kwa Chadema mnafanya kazi tuliowatuma laiti uchaguzi ungefanyika leo tungewapa zawadi ya ushindi mnono. Asante, Mbowe unatusaidiana.
ReplyDeleteMbowe bado anasaini posho, aache uongo.
ReplyDeleteJamani watu waliolelewa na mfumo Kristo wana hatari, wanaiba huku na huku. Tungeongelea kuondoa misamaha ya kodi mashirika ya dini. Maaskofu wanafanya ufisadi wa hatari kwenye misamaha hiyo.
Watasema eti anatafuta Umaarufu wa Kisiasa.Ni bora kuutafuta kwa kuchangia maendeleo kuliko kutunyonya wananchi bila hata soni Kama wanavyofanya viongozi wa chama hiki kilicho madarakani.Hongera sana kamanda na kaza buti,WATABISHA LAKINI MWISHOWE UKWELI UTAJITENGA NA UONGO
ReplyDeleteAsitudanganye huyo, kwanza ametuibia kodi zetu sana kwa kutulipia biashara zake, hebu pitieni hesabu zake pamoja na ndesamburo muone madudu aliyokuwa anatufanyia. ninauhakika na hilo fanyeni kwa kipindi kifupi tu. kuanzia 1985-1995. sasa leo anataka kutughiribu eti anarudisha gari. asitake kutufanya wote mbumbumbu kama yeye, mwizi mkubwa. Bajeti imepita na kazi itafanyika tusubiriane tena mwakani.
ReplyDeletemwizi tu huyo misimkubali muongo na anataka nafasi azidi kuiba tu
ReplyDeleteWatu wengine badala ya kuchangia wao wanaleta wivu wa kijinga. Unamshutumu mtu kupata utajiri kihalali, wenzio wanafanya kazi. Swala la kodi ni system mbovu iliyopo serikalini, wanabana wauza vitumbua huku magabacholi ´wakishirikiana na haohao wakusanyaji katika kukwepa. Fanya kazi kijana na pigia kelele serikali ikuwekee mazingira mazuri ili juhudi zako zizae matunda. Hii nchi ina watu kibao wakulialia, mpaka JK mwenyewe badala ya kuwawajibisha watu naye anabaki kulialia tu. Mnaniuziii......
ReplyDeleteHuko nyuma nimewahi kumsikia Kikwete akisema kwamba zamani mtu akikaguliwa na kukutwa na utata katika fedha za serikali kulikuwa hakuna mjadala. Polisi waliitwa na hatua kuchukuliwa. MBONA HAIKO HIVYO SASA? KULIKONI?
ReplyDeleteHONGERA SN MHESHIMIWA,INAHITAJI MOYO HAKIKA MNATUJALI CHADEMA,NA WENGINE WA KAMBI YA UPINZANI IGENI MFANO TWATAKA KUSIKIA UPINZANI WOTE MWAFANYA HIVYO KAMA KWELI MNAONA NA MNAUCHUNGU NA MAISHA WANAYOISHI WANANCHI WENU,KUNA MTU ANAISHI KWA CHINI YA DOLA MOJA KWA SIKU LAKINI VIONGOZI WAO KWA SIKU WANAPATA LAKI NA NUSU POSHO TU,KWELI VIONGOZI WETU WAKO KIMASLAHI ZAIDI,HONGERA MBUNGE WETU KWA KUONYESHA KUWA UNATUJALI,MUNGU AKUJALIE MOYO HUO HUO NA PIA AMJALIE RAIS WETU MTARAJIWA DR WILBROD SLAA MOYO KAMA WAKO.KAZI NJEMA MHESHIMIWA
ReplyDeleteHilo shangingi umerudisha baada y kuwa nayo zaidi ya moja siyo,,,acha kutufanya watoto siye kama vipi kama milivyogoma bungeni kwa pamoja basi wote myaweke pale hayo mashangingi basi mbona wewe tu mheshimiwa....ama kweli umaarufu kazi kwelikweli....
ReplyDeleteHospitali ya Muhimbili hupata takribani shs billion moja tu kwa mwaka kwa matumizi yake ya kawaida. Hebu wape hizo billion 4 za posho ya vikao ya wabunge huduma itakavyokuwa muruwa hapo Muhimbili na idadi ya vifo vya Watanzania wanaokufa pale Muhimbili itakavyopungua!
ReplyDeleteMafuta ya taa yanatakiwa yapungue bei. Ni aibu serikali kukiri wachakachuaji imewashindwa. Inatakiwa kuwatungia sheria kali -- akishathibitishwa mahakamani ni kifungo miaka 2 jela na viboko 12 sita anapoingia gerezani na sita anapotoka akamuonyeahe mkewe. Wataacha.
Naamini wamilki wa gazeti hili kama wangejua kuwa watu baada ya kutoa maoni, wangegeuza fursa hii kuwa ya kutoa matusi, kujenga uchochezi na lugha zisizo na ustaarabu, wasingetoa fursa hii.
ReplyDeleteWasomaji wenzangu, kama huna maoni hulazimishwi useme chochote. Nayasema haya kwasababu bila kujali itikadi, ukweli ikifuatilia taarifa iliyoandikwa na gazeti hili pamoja na kitendo chake cha kuachia hilo V8(KUB) alipaswa kupongezwa, lakini matokeo yake anatukanwa, wengine wanaleta ikadi, n.k.
Kwa upande mwingine, Mkulo alipaswa kuonyesha ukomavu wa kisiasa. Katika matamshi yake, hakuna mahali anaonyesha kwamba kuna jambo japo moja la kuwaunga mkono upinzani kwa maoni na mapendekezo waliyotoa, hii si sawa hata kidogo. Anasema wamekubaliana na ushauri wa kamati ya kigoda, asijue kuwa katika kamati hiyo yumo Mbowe pia, sasa kama anaweza kumuunga mkono akiwa chini ya uenyekiti wa Kigonda, leo hii inakuwaje ambeze kwa kila jambo kwa kuwa upinzani?
CCM Inatumia wingi wa kura zao kimabavu kupitisha hata mambo yenye kumdidimiza Mwananchi na kudumaza maendeleo ya Nchi ili mradi wao binafsi wanafaidika lakini hii ni changamoto kwa watanzania itakapo fika wakati wa kupiga kura 2015 ya kumchagua RAIS inabidi wawe makini zile zama za kuuza kura yenye thamani ya kipindi cha miaka mitano ya maisha yako kwa Chupa 1 tu ya Gongo, Pilau, Kangara, Mapuya, Kanga na T-Shirt za CCM umepitwa na wakati hata vijijini wanatambua haki zao sasa zidumu fikra na misimamo ya watanzania wa kisasa.
ReplyDeleteMTU MWENYE BUSARA ANABIDI AKAE AFIKIRIE MARAMBILIMBILI, KWANZA HILO LINABIDI LIPITISHWE NA BUNGE KUFUTA POSHO, NA HAYO MASHANGINGI, KUJIAMULIA TUU SIO KWELI!! YEYE ANGETAKA KUWA MKWELI ANGELIKATAA SIKU ALIYOPEWA,PIA AKATAE NA POSHO ANAYOPEWA KIONGOZI WA UPINZANI MILLION 200 KILA MWEZI AZIPELEKE ZIKALIPIWE WANAFUNZI VYUO VIKUU, HUWEZI KATAA KIMOJA CHA PILI UNAKUBALI IWEJE? TUNAJIKAANGA KWA MAFUTA YETU NA KUSHABIKIA MAMBO BILA KUFIKIRI!!
ReplyDeleteKIUKWELI UKIWA MWANA CCM HAUWEZI KUELEWA ANACHO FANYA MH:MBOWE ,HUU NDIO UZALENDO NA UCHUNGU WA NCHI HII .MTU ANASEMA KWANINI HAKURUDISHA SHANGINGI MWANZO? HILI SWALI HALINA MSINGI KWANI AMEAMUA KURUDISHA SASA
ReplyDeleteHAO AMBAO HATA AWAFIKIRII KUYARUDISHA MBONA HAWAZUNGUMZII.
KWA UJUMLA WABUNGE WA CHADEMA WANAFANYA KAZI NZURI SANA BUNGENI NA NDIO FAIDA YA VYAMA VINGI: NAAMINI WANAOPINGA SWALA LA MH:MBOWE HAWANA UCHUNGU WA NCHI HII
akuna matusi huo ni ukweli
ReplyDeletewatu hapa wanashindwa kuelewa na kuongea tu ila watanzania wenzangu mnachotakiwa kufahamu ni kwamba TZ ni nchi masikini hasa kwa wale wa kipato cha chini ambao ndio wengi, sasa Mheshimiwa Mbowe anachojatibu kufanya ni kwamba ni kupunguza mapato makubwa ya matajiri wachache na kuongeza angalao hata huduma za kijamii za mtanzania wa kawaida,lakini njia sahihi ya kuweza kufanikisha hili ni kwa kupunguza posho za hao matajiri ambao wengi ni viongozi wetu hivyo kama kiongozi wa upinzani mbeba hoja ni lazima aoneshe mfano.Nasikitika sana kutoangalia hili swala kwa umakini,sisi watanzania embu tufikirie hivi kweli mama mjamzito anazalia njiani kwa kukosa usafiri huku Mbunge akiwa anaingiza sh;laki unusu kwa siku,ni jinsi gani wabunge tuliowachagua walivyokuwa hawana huruma na sisi.Hata kama wewe unapenda ccm ni lazima ufike sehemu ukubali ufisadi wao.Na wewe raia wa maisha ya chini kama mimi unaeshabikia mafisadi,,embu jiulize wewe ni nani? na unakwenda wapi?Je watanzania watakubali kuibiwa hivi mpaka mwisho?amini ipo siku ccm itaondoka madarakani na nyota ya maendeleo Tanzania itang'aa.
ReplyDeletembowe endelea na mikakati yako kwa kuwa serikali siyo ccm inasikia na wabunge kama kweli wana uchungu na nchi yao naamini watabadilisha hizo tabia mbovu za kutetea mambo yasiyo ya msingi ilhali nchi yetu inaangamia.
ReplyDeleteMWIZI HUYO,MAPESA MENGI KAIBIA CHADEMA,KAUZA MADAWA YA KULEVYA SANA NA SASA ANATAKA NAFASI YA JUU KATIKA SERIKALI APATE KUTUMALIZA,MSIMKUBALI NI JAMBAZI HILO. WACHAGA WENZIE KATIKA GAZETI HILI WANAMLINDA
ReplyDelete