23 June 2011

Tume ya Maadili yakwama kumhoji Cisco Mtiro

Na Salim Nyomolelo

BALOZI wa Tanzania nchini Maleysia, Bw. Abdul Cisco Mtiro, ambaye alitakiwa kuhojiwa na Tume ya Maadili kwa kushindwa kujaza fomu za tamko juu rasilimali
na madeni,  hakuhojiwa baada ya kutoa udhuru.

Katika taarifa ya udhuru wake, Bw. Mtiro alisema hakuweza kufika kwa ajili ya kuhojiwa kutokana na  Rais wa nchi hiyo kuwa na ziara katika eneo lake la kazi.

Aliomba kupangiwa tarehe nyingine ya kufika ofisi za tume kwa ajili ya kuhojiwa.

Taarifa hiyo udhuru wa Balozi Mtiro ilikubaliwa na ofisa wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ingawa tarehe rasmi haikutangazwa.

Tume hiyo iliendelea kuwahoji viongozi wengine, akiwemo  Diwani wa Kata ya Mwamanga wilayani Magu Mkoa wa Mwanza, Bw. Elikina Makoja na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Wilayani Magu, Bw.Sabato Bwire.

Akijijitetea mbele ya baraza hilo ambalo lilikuwa linaongozwa na Mwenyekiti, Jaji Damian Lubuva,  diwani huyo alidai alijaza fomu hizo, tofauti na inavyodaiwa kwamba hajafanya hivyo kwa mwaka 2007,2008 na 2009.

Kwa upande wake wa Bw. Bwire, alisema mwaka  2008 hakupata fomu hizo, mwaka   2009 alipata fomu hizo Januari mwaka jana na alizijaza na kuzituma kwa njia ya posta, hivyo kama hazikufika hajui zilipokwamia.

No comments:

Post a Comment