BEIRUT, Lebanon
ALBAMU mpya ya mwanamuziki, Lady GaGa iitwayo 'Born This Way' imeruhusiwa kuingia nchini Lebanon baada ya nchi nyingi za Mashariki ya Kati kuipiga
marufuku.
Ilielezwa kuwa kumekuwepo na kilio kutoka kwa mashabiki wa mwanamuziki huyo, baada ya gazeti la The Sun Jumamosi iliyopita kueleza kuwa mwimbaji huyo wa Marekani amewekewa ngumu na Serikali ya Lebanon.
Hatua hiyo ilikuja baada ya makachero wa nchi hiyo kukamata meli iliyokuwa na shehena ya CD za albamu hiyo, ambayo ina kibao kitwaacho Judas was 'offensive to Christians' ambacho kinadaiwa kukashifu dini ya Kikristo.
Albamu hiyo pia ilizuiwa kupigwa hata kwenye vituo vya redio, lakini baadaye Serikali ikamua kuiruhusu albamu hiyo baada ya mashabiki nchini humo kuandamana wakidai kuwa hatua hiyo haina maana kutokana na kuwa tayari albamu hiyo imeshasambazwa kwenye mitandao ya internet.
Taarifa iliyotolewa juzi ilieleza kuwa "CD zimehidhinishwa kuingizwa na kusambazwa nchini Lebanon."
Na taarifa hizo kisha zikadhibitishwa na msemaji wa Lady GaGa (25).
Albamu hiyo ya Born This Way, imekuwa ikishika nafasi ya kwanza katika mataifa 28 tangu ilipoipuliwa wiki mbili zilizopita.
No comments:
Post a Comment