06 June 2011

Kukamatwa M/Kiti CHADEMA.

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Willibrod Slaa akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu kukamatwa kwa Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Freeman Mbowe. Katikati ni Katibu mwenezi na habari Bw.Erasto Tumbo kushoto ni Mbunge wa Moshi Mjini Bw. Philemon Ndesamburo.

10 comments:

  1. Kwa hali hii sijui kama tutapata bajeti yenye mchakato mzuri kwani inahitaji mawazo ya vyama vyote na hasa upinzani ili kuibana serikali.Nadhani serikali inatakiwa kuwa makini na maamuzi otherwise patachimbika sasa

    ReplyDelete
  2. hamna jeuri ya kutishia amani ya nchi hii

    ReplyDelete
  3. Lakini Mbowe hayuko above the law,ili pia tuliangalie,inabidi CHADEMA wawe wajanja sana katika approach zao vinginevyo CHAMA CHA MAGAMBA kitawaumiza.

    ReplyDelete
  4. Hebu mkomae kifikra unapoleta jeuri kwa mahakama unatarajia kupata nini? hakuna aliye juu ya sheria mbona wenzie walitii nawakajisalimisha mapema yeye ni nani mpaka aabudiwe. amekipata alichokitaka na hakuna lolote litakalofanyika kuchafua amani tuliyo nayo, kama kweli wanaume anzisheni vurugu kwa ujinga weno ndo mtajua bangi siyo mboga

    ReplyDelete
  5. Muhimu kufata sheria za Nchi zinasemaje, isiwe kuwa upinzani ukapata jeuri ya kudharau kazi za taasisi zingine.Wengi wanajiingiza upinzani nia ni kudharau au kutowajibika kwa kigezo cha upinzani, na pia Slaa anapomfananisha Mbowe sawa na Pinda kwa cheo si kweli yule ni kivuli inakuwaje kivuli kiwe sawa na uhalisia? tuwe makini nia hapa ni kuchafua hali ya hewa inatafutwa kila mbinu ili kupata pa kuanzia,Mara Raisi hatumtambui mara Katiba mara polisi wanaua na sasa mbowe aachiwe kwa dharau au la sivyo patachimbika haya yetu macho.Na ndugu yangu Lipumba hata ukajipendekeza kwa hao hupendezi tuu wao washakuona uko ktk ndoa na Chama kubwa!! unapoteza muda wako bure.

    ReplyDelete
  6. WATANZANIA TUTAINGIZWA KATI VITA BILA SABABU ZA MSINGI, NAWAASA NINYI MNAOSHABIKIA UPUUZI UNAOFANYWA NA VIONGOZI WA CHADEMA, HIVI ANGELIKUWA NI MLALAHOI AMEKAIDI AMRI YA MAHAKAMA MNGELIPIGA KELELE KAMA MNAZOFANYA SASA, NA JE HUYO MBOWE ANAJIBU JEURI KAMA VILE YUKO ABOVE THE LAW!!!? AMEYATAKA ACHA AYAPATE. MTAKAOANDAMANA KUSHABIKIA UPUUZI HUO NANYI DOLA INAWASUBIRI MPATE MNACHOKITAFUTA WEWE MWENZANGU NA MIMI UNAKWENDA KWA MKUMBO BILA KUJUA MADHARA YATAKAYOKUPATA, WENZIO WANAWAKUWASEMEA HUKO UGHAIBUNI WEWE JE?? JEURI YA HAWA NDUGU INARAISHIA UVUNJIFU WA AMANI. TANZANIA YENYE AMANI INAWEZEKANA, POLISI,MAHAKAMA,KAZA BOOT KOMESHA WANAOJIFANYA KUTOZINGATIA SHERIA NAKUJIONA WAKO JUU YA SHERIA, HAYO NDIYO MATUNDA YA KIBURI

    ReplyDelete
  7. Naunga mkono kwa yaliyo mpata Mbowe, ili kukomboa wanyonge hunabudi kupatashida. Watawala wadhalimu siku zote hutumia mabavu katika \kivuli cha sheria. Mandela alikaa gerezani miaka mingapi akiwa kupigania Haki, iliyomfunga haikuwa sheria? Kwa wale wakristu Yesu alisulubiwa msalabani sheria haikutumika?

    Watu wangapi walinyongwa na kufungwa katika kudai uhuru wao sheria zilisemaje?

    Mzuzuri aliua dereva kwa pisto sheria ikasemaje?

    Wote mnahaki ya kumponda Mbowe na kujifanya mnajua sheria, kwani mnanufaika na utawala wa Kidharimu wa kikwete, hamjui mateso wanayopata maskini. Hata hiyo amani mnayotetea inawahusu ninyi mnaotembea kwenye magari ya kifahari, sisi maskini hatuna amani.
    Kwa taarifa yetu nyote hamjui sheria ila tu ni ushabiki unaotokana na manufaa mnayopata toka CCM.
    Kwa sasa Tanzania huwezi kutenganisha siasa za CCM, Mahakama, Police na Bunge.

    Mbowe kukaa Gerezani ni sehemu ndogo sana ya mateso makubwa yanakuja. Kuokoa wanyonge kunahitaji uvumilivu.

    Bagbo, Kaunda, Mbaraka, na wengineo waliona nchi kama za kwao, yote haya yana Mwisho.

    ReplyDelete
  8. sasa kwa taarifa Mbowe amekuwa kuwa nje kwa dhamana yake ilie ile ya kwanza, watu wanadhani haki inakuja kinalenale tu,hizi ni enzi zingine watu wanalinganisha na enzi za kudai uhuru kwa maneno tu, ile ilikuwa huruma ya watawala wa tanganyika,sasa hivi hata wadhalimu wamesoma hawatoi haki kirahisirahisi hivyo ni lazima kukomaa, na msidhani kuwa yuko peke yake daima watu tuko pamoja nae, hao wasioelewa wabakie kutoelewa maana ni vipofu hawaoni nchi inavyotaabika wakiwemo mapolisi.

    ReplyDelete
  9. CHADEMA MSIOGOPE KUPIGANIA NCHI KWAAJILI YA WAUWAJI WA CCM WANAO UWA WATANZANIA BILA HURUMA, POLE MBOWE UNAONYESHA JINSI ULIVYO NA HURUMA KWA WANYONGE WATANZANIA, CCM NI BALA NA VIONGOZI WAKE NI WAUWAJI WAKUBWA,WANAFURAHIA VIFO VYA WATANZANIA NA KUFANYA SHEREHE KILA POLISI ANAPO UWA WATANZANIA. BASI TU ATAAKAAYE KUJA KUITOWA CCM MAARAKANI SIJUWI TUTAKAAJA KUMPA ZAWADI GANI

    ReplyDelete
  10. Muwe makini na mawazo yenu huwezi kufananisha habari za Yesu kusulubiwa au mambo yaliyojiri huko Misri,Ivory coast au
    kulinganisha na mzee Mandela!! yashangaza kwani tuna gombea uhuru hapa?nk, na huu utumbo wa viongozi wenu nanyi kutumia kivuli cha upinzani kutoa matusi na kashfa kwa viongozi walio madarakani mujuwe huu ni umbumbumbu na kutojuwa sheria,pamoja na viongozi wenu, huyo mbowe anajiona kuwa Kiongozi KIVULI wa bunge basi sheria ziko chini yake someni nyakati na Katiba pia

    ReplyDelete