07 June 2011

England yamuumiza kichwa Capello

LONDON, England

KOCHA Fabio Capello amesema hadi sasa hafahamu jinsi gani aisuke timu ya taifa ya England, ili iweze kuwa fiti na iweze kuleta ushindani.Kocha huyo ambaye analipwa
pauni milioni 6 kwa mwaka, alikiri kuwa hawezi kutatua matatizo kama yaliyoikumba timu hiyo katika mchezo wa Jumamosi wa kufuzu fainali za Matifa ya Ulaya Euro 2012, ambao timu hiyo ilitoka sare ya mabao 2-2 na Uswis.

Hata hivyo Capello, mwaka jana alitoa kauli kama hiyo baada ya timu hiyo kutupwa nje ya michuano ya fainali za Kombe la Dunia.

Alipohojiwa kama timu hiyo itaelewena endapo itafuzu fainali hizo alisema: "Sifahamu. Tutajaribu kutafuta ufumbuzi. Nina matumani hayo. Unaweza kufahamu dawa yake?. Haiwezi kuwa ni kiwango kwa sababu tuna kiwango. Tatizo ni nguvu.

"Unapokuwa haupo fiti inakuwa ni vigumu, lakini unapokuwa upo fiti mpira unakwenda kwa haraka bila matatizo.

"Unapofanikiwa kupokea mpira unahitaji kukimbia na kutoa pasi na akasema kuwa unapopoteza mpira inakubidi uhitaji kuuchukua tena," aliongeza.

Capello alisema wamekuwa wakitumia muda mwingi kujaribu kuchukua mpira, lakini siku hiyo hakuwa safi kama walivyokuwa kwenye mechi walizopata ushindi nchini Uswis na Wales kutokana na kuwa walikuwa wakichukua mipira kwa haraka.

Alisema  wakati wa mazoezi walikuwa wakijifua kwa muda wa saa moja, lakini mechi hiyo ya juzi ilikuwa ni ya saa moja na nusu.

"Si mawazo yangu walikuwa wamechoka, uliweza kuwashuhudia uwanjani. Wilshere alimaliza dakika 10 akiwa amechoka mno," alisema Capello.

Hata hivyo Capello alijichanganya mwenyewe baada ya kusema tena kuwa England, ilizinduka baada ya kutoka mapumziko.

No comments:

Post a Comment