01 July 2011

Kocha wa ngumi amtaboria ushindi Klitschko

HAMBARG,Ujerumani

MANNY Steward anaamini kuwa, robot (Wladimir Klitschko), itammaliza David Haye katika pambano lao la kuunganisha mataji litakalofanyika kesho.Mwalimu huyo
maarufu wa ngumi ambaye alimwibua Lennox Lewis, ameitwa na Klitschko ili kumsaidia mbinu za kiufundi katika maandalizi yake ya mwisho.

Steward amekuwa amekuwa na kawaida ya kutopenda kuzungumza kabla ya pambano, lakini juzi alisema: "Haye anasema anapigana na robot kwa Wladimir.

"Tutakuwa na lengo la kuangamiza, kuua na kumtoa Haye Jumamosi.

"Hiki ni kitu ambacho robot itafanya. Huyu  mtu mjanja ataniambia mimi baada ya raundi kadhaa: Mpango umekamilika".

Wakati huohuo, Haye amesema kuwa, hawezi kuondoa Uingereza hata kama itamgharimu kwa kulipa kodi nyingi.

Bingwa huyo wa uzito wa juu wa WBA amesisitiza kuwa,  hana mpango wa kufuata nyayo za nyota wa mashindano ya mbio za magari za Formula One, Lewis Hamilton, alivyohamia Uswisi.

Haye mwenye miaka 30, atapata mapato ya pauni milioni 100 na hivyo kukatwa kodi kwa mujibu wa promota wake, Frank Maloney.

Lakini, bingwa wa WBA, kesho anapambana na  Wladimir Klitschko ambaye ni bingwa wa  mikanda ya WBO na IBF mjini Hamburg, amesema anafurahi kutoa kodi  Uingereza.

Alisema kwa kila pesa anayotengeneza, sehemu yake inabakia kwa rafiki zake na familia.

Utozaji wa kodi Uingereza ni asilimia 50.

Mbali na mapato kutokana na kupanda ulingoni, bondia huyo anapata mapato kwa mikataba ya matangazo ya watengenezaji sare za michezo, nguo, mikataba ya kampuni za televisheni na anachapisha gazeti lake.

No comments:

Post a Comment