*Afichua yaliyomo katika bajeti yake
*Bodi ya mikopo kuongezewa fedha zaidi
Na Charles Mwakipesile, Mbeya
WAZIRI wa Elimu na Mafunzoya Ufundi, Dkt.Shukuru Kawambwa, ametangaza mkakati wa kumaliza migomo na vurugu katika vyuo vikuu
baada ya wizara yake kuongezwa bajeti katika mwaka huu wa fedha 2011/2012.
Akitoa salamu zake kabla ya kusoma hotuba kwa niaba ya Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, ambaye alimwakilisha kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa Chuo Kikuu cha Teofili
Kisanji (TEKU), Bw. Kawambwa alisema kuongezwa kwa bajeti ya wizara yake kutasaidia kumaliza matatizo kwenye vyuo vikuu.
Huku akishangiliwa na wanafunzi wa chuo hicho, Dkt. Kawambwa, alisema wizara yake imeamua kuongeza bajeti hiyo, ili zipatikane fedha za kutosha kwa ajili ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu na kisha kuongeza posho ya chakula ambayo nayo imekuwa ikilalamikiwa kila siku na kusababisha migomo.
Hata hivyo waziri huyo hakutaja ongezeko hilo kwa kuwa lilikuwa halijapitishwa na bunge. Alisema ana imani kuwa bajeti hiyo itamaliza matatizo ya wanafunzi wa vyuo vikuu. Alisema wanafunzi wengine wamekuwa wakiofanya
vurugu kwa kufuata kasumba.
Alitoa mfano akisema wanachojua ni kuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) walifanya mgomo usiowa wa lazima,
kwa kuwa madai yao yalikuwa yakishughulikiwa.
"Angalia ndugu zangu wale wa UDOM kwa kweli walifanya mgomo wakati madai yao yanashughulikiwa," alisema.
Alisema serikali inatoa kipaumbele kwa elimu kwa kutambua
umuhimu wake,hivyo kupitia bajeti ya mwaka huu itakapokuwa kutakuwa na mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu.
Alipongeza amani na utulivu uliopo katika chuo cha kikuu cha TEKU na kushauri kiwe mfano wa kuigwa na vyuo viongine.
Mkuu wa chuo cha TEKU Mhashamu Askofu Alinikisa Cheyo alisema chuo hicho kimekuwa na nidhamu hivyo kuwa na uhakika wa kutoa wasomi wanaotegemewa. Chuo hicho kinamilikiwa na Kanisa la Moravian Tanzania.
sio kweli kuwa matatizo ya wanaudom yalikuwa yanashughulikiwa hizo ni siasa tu
ReplyDeleteWATANZANIA HAPA NDIO TUMEFIKA MWISHO WA MAENDELEO NA KUFIKIRI,HUYU WAZIRI KICHWA CHAKE NADHANI SIYO KIZURI KWA SABABU KUANDAMANA NI HAKI YA WANAFUNZI KUELEZEA SHIDA WANAZOPATA! SASA KAMA HATA WASOMI NAO WANAZUIWA KUFIKIRI AMA KUELEZEA SHIDA ZAO KWA MAANDAMANO HII NDIO SERIKALI TULIYONAYO
ReplyDeleteSERIKALI INALAUMIWA KWA UZEMBE KUTOWAWAJIBISHA BODI ZA VYUO, MAANA VYUO VINAFUNGULIWA BADO MIKOPO HAIJATOKA HIVI HAWA WATAJIKIMU VIPI? WANAZEMBEA INAFIKA MUDA UVUMILIVU HAKUNA NA HASA UKIZINGATIA SIKU HIZI NIDHAMU NA USTAHAMILIVU UMEPUNGUWA,NA BAADHI YA WANAFUNZI WAMEKUWA JEURI MNO,SIO WOTE WAPO WANAOTAKA KUSUBIRI
ReplyDeleteLAKINI WANASHINIKIZWA NA HATA KUPIGWA NA WENZAO WAWAUNGE MKONO KTK MADAI YAO ETI UKIINGIA DARASANI UNAWASALITI, TUBADILIKE
NA SASA KUWE NA KITENGO MAALUMU NDANI YA TAKUKURU KISHUGHULIKE NA WALE WOTE WALIOPEWA MIKOPO AMBAO SASA WENGINE NI WABUNGE,MAWAZIRI,WAKURUGENZI NK, WAWAKABE WARUDISHE MAANA WANAJULIKANA MIKOPO HAIREJESHWI IWEJE WAO WAWE WANAPEWA ZINAPOTEA KILA MWAKA? BASI KAMA HAKUNA KUREJESHWA VIJANA WALIO VIJIJINI WAPEWE NAO
HIYO MIKOPO ISIYORUDISHWA!!