07 June 2011

Kauli ya JK yawashangaza viongozi wa dini, wanasiasa

Na Dunstan Bahai

BAADHI ya viongozi wa dini na wanasiasa nchini wameishangaa kauli ya Rais Jakaya Kikwete kwamba viongozi hao wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya bala
ya kuwakamata.

Viongozi hao kwa nyakati tofauti walisema kama kweli kauli hiyo ina ukweli, ni kwamba serikali inawajua wahusika hivyo kuhoji kwa nini isiwakamate na badala yake Rais anaishia kulalamika kwenye majukwaa.

Juzi wakati akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga kwenye ibada maalum ya kupewa daraja la Uaskofu na kusimikwa kwa Mhashamu Askofu John Ndimbo wa jimbo hilo, Rais Kikwete aliwataka viongozi wa dini kuacha kushiriki kwenye biashara ya kuuza dawa za kulevya na badala yake washirikiane na serikali katika kuidhibiti.

Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Bw. Ponda Issa Ponda alisema kauli ya Rais inaashiria kuwa yeye (Rais) na watendaji wake (serikali) wanawajui wafanyabiashara hiyo haramu.

"Mimi nashindwa kuelewa, kitendo hicho ni kosa, na sheria inapovunjwa haiangalii huyu ni kiongozi wa dini au la, inachukua mkondo wake dhidi ya watu hao," alisema.

Alisema kabla ya Rais kutoa kauli hiyo aliyoiita ni ya kulalamika kwa wananchi, alitakiwa kuwakamata kwanza hao viongozi wa dini kisha kuuambia umma wa Watanzania kuwa nao wanajihusisha na biashara hiyo.

Bw. Ponda alisema kuwa viongozi wa dini ni sehemu ya serikali, hivyo haipaswi kiongozi wa serikali kuwalaumu, bali kama wanafanya makosa, sheria ichukue mkondo wake.

Mmoja wa maaskofu wa Kanisa Anglikana Tanzania ambaye alikataa kutajwa jina lake gazeti kwa vile si msemaji wa kanisa hilo, alizungumza kwa masikitiko kwamba Rais amewadhalilisha na kuwakosea adabu.

"Kwa kweli Rais ametudhalilisha, hakututendea haki kabisa, ametukosea heshima kwani alichotakiwa ni kumtaja huyo anayedhani anajihusisha na biashara hiyo, lakini si kutaja kwa ujumla wetu," alisema.

Askofu huyo alisema wao ni watu wa heshima na wanaoheshimiwa na jamii na hasa ikizingatiwa pia kuwa wanaisadia serikali katika kuwaongoza wananchi katika njia iliyo nyofu, hivyo hawajui hatma yao mbele ya jamii hiyo inayowaamini.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba alisema kama rais anapata ujasiri wa kusema hayo, iweje asiwachukulie hatua za kisheria kwani hayo ni makosa ya jinai ambayo adhabu zake hazichagui kiongozi wa dini, serikali au mwananchi wa kawaida.

Alisema serikali haiko makini katika vita dhidi ya dawa za kulevya kwani aliyekuwa mbunge wa viti maalumu Marehemu Amina Chifupa, alijitoa mhanga katika kuisaidia serikali kuwafichua wafanyabiashara hao haramu, lakini serikali haikumtumia hadi akafariki dunia.

Bw. James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, alisema mfumo wa uendeshaji serikali ni wa kifisadi, kwani hata viongozi wamejawa na ubinafsi na ndiyo maana hata sheria hazisimamiwi ipasavyo.

"Rais ameendelea kuimba ngonjera kila siku, leo kawataja viongozi wa dini, kesho ni wewe mwandishi, siku nyingine waganga wa kienyeji. Kama anawajui anasita nini kuwachukulia hatua," alihoji Bw. Mbatia.

Alimshauri Rais kutumia madaraka yake kuwachukulia hatua badala ya kulalamika kama wananchi wa kawaida.

14 comments:

  1. ASAMEHEWE BURE!! NAFIKIRI ANATATIZO

    KWENYE MAAFA YA GONGOLAMBOTO ALITOA TABASAMU LAKUFA MTU WAKATI ANAPEWA MUHUTASARI WA YALIYOWAFIKA WAKAZI WA GONGO LA MBOTO.

    TANZANIA TUNAHITAJI KIONGOZI ATAKAYE TUONESHA NJIA YA KUJIKWAMUA NA UMASKINI,UJINGA NA MARADHI.

    CHUKI INAYOENDELEA KUJIJENGA NI KWA SABABU YA UJINGA NA KUJIPENDEKEZA KWA MAOFISA KADAHAA WAKIDAI WANALINDA MPUNGA WAO.

    KAMA KIONGOZI NI AIBU KWENU, MNANUKA RUSHWA,NA KUTOWAJIBIKA IPASAVYO, UMBEA NA KUONGOPA KWA WANANCHI NDIO DIRA NA MAFANIKIO KWENU.

    &^%$$## ZENU.

    ReplyDelete
  2. Tulisha sema jamani nchi hii nzuri sana yenye maliasili nyingi, watu wema sana na wapenda amani lakini kwa uhakika Tanzania inapoteza mwelekeo! nionanvyo mie ni kwamba yaletuliokuwa tunayasikia, kuyaona kwa majirani na tulikuwa wasuluhishi wao sasa tunaelekea huko walikotoka wao. hakika ikiwa Kikwete ataendelea kuwa Rais wa kuchekacheka matokeo yake ndio anaongea tena mbele ya hadhara kana kwamba yeye siyo rais mwenye mamlaka! huyu mtu anatupeleka wapi?! ameingiza nchi ktk mgogoro wa kidini, umaskinina ukabila maana yeye hajawahi kukemea kwa sababu anajua jinsi anavyowatumia viongozi wa kidini

    ReplyDelete
  3. Mafisadi wa EPA unawabembeleza kurudisha pesa.Mafisadi wa DOWANS,RICHMOND na RADA unawaapa siku wajiue magamba.WAUZA UNGA tangu umeingia madarakani ulisema unawajua kwa majina na hata sasa viongozi wa kiroho pia unawajua.Wape siku waache hiyo bishara na SISI WATANZANIA TUNAPENDA AMANI NA UMASKINI NA HUKU TUKICHUKIA MAENDELEO.Kufika 2015 tutakuwa tumeona na kusikia mengi ya utawala wa kulalamika na kulinda mafisadi lakini wenye kukandamiza wanaopaza sauti kutetea wanyonge.POLEPOLE TUTAFIKA TU

    ReplyDelete
  4. Ni kauli iliyoshangaza wengi. Hakuna mtu anayefanya biashara hiyo kwa kutumwa na madhehebu yoyote, wala kuruhusiwa na madhehebu yoyote. Ila wapo wanaofanya biashara hiyo kwa kutumia majina ya madhehebu za dini bila idhini. Inawezekana wakawa Wachungaji, au Masheikh, lakini si kweli kwamba hawa wanatumwa au wameruhusiwa na madhehebu hizi, hii ni biashara haramu na inafanywa na mtu binafsi kwa faida yake yeye mwenyewe! Mbona hata Mawaziri wengine na wakubwa wengi wamekwisha fanya sana biashara hii, tena kwa kutumia diplomatic bags za serikali? Je, tutasema serikali inajihusisha na madawa ya kulevya? Sidhani kama Rais alikuwa hajui hili, ni kauli ambayo hakupaswa kuitoa kwa kinywa chake kabisa! Kwa hili, kwa uungwana tu, ni vyema aka-apologise ili umma uweze kumsamehe.

    ReplyDelete
  5. Kwa nini Chifupa alikufa!!!!! Kwa sababu ya kufuatilia KIKWETE NA MAWAZIRI WAKE kwa biashara hii ya kuuza unga!!!

    ReplyDelete
  6. Ndio shida ya kua na kiongozi msanii.Anadhani mambo hujipa tu na nchi ikaenda.Kumbukeni majuzi wakati anawaasa mawaziri wake alijaribu kukemea ubabe wa mawaziri.Wakati nchi inahangaika kuwapata wala rushwa,yeye anasifia kitendo chake cha kususia kiwanja alichopewa B'moyo.Badala ya kusimama kidete ajulikane aliefanya 'double allocation'yeye akasusia kiwanja eti wasimtafsiri kafanya ubabe kwavile yeye ni waziri.Hivi siku akilikuta jibaba chumbani kwake atasusa pia?Haya twendeni tu. . .tutafika

    ReplyDelete
  7. SHIDA VIONGOZI WA DINI MNAJUA FIKA KUWA ADUWI YENU KUBWA NI JAKAYA SASA IWEJE BADO MNAMNG'NGANIA UMWALIKA KWENYE SHEREHE ZENU, KWANI JAKAYA ASIPOKUWEPO HAKUNA UASKOFSHO MBONAMAASKOFU WA MAEDHEBU MBALIMBALI NIWENGI KAMA MNATAKAKUJAZA UKUMBI CHUKUENI WATU WOTE ACHENI KUJIPENDEKEZA KWA ASIYE WAPENDA MNAJIDHRIRISHA WENYEWE. KAMA ANAJUA BIASHARA HIYOIPO ANASUBRI KUITANGAZIAJUKWAANI. PENGO ACHA KUMWALIKA HUYU

    ReplyDelete
  8. Si lazima kumwalika Rais kwenye sherehe ya kumsimika askofu ingawa tangu nyuma imekuwa jadi, rais anaalikwa. Si unajua inaweka uzito! Sherehe aliyohudhuria rais si ya kawaida.
    Kutomwalika rais kwa kuhisi hawapendi maaskofu si suluhu. Aalikwe. Unajua Kikwete amekuwa akipashwa kwenye sherehe kama hizo. Mwanza alipashwa.Naye zamu hii akatafuta la kuwapasha hata kama halina udhibitisho. Kupashana kunaweza kuwa uwanja wa vita vya maneno. Lakini kama kuna ukweli wahusika wajirudi.

    ReplyDelete
  9. Hayo ndiyo matokeo ya kumwalika chizi harusini! Haya sasa kavua nguo mbele ya bibi harusi! Sasa sijui anamtaka bibi harusi? Joto limezidi? Au ni uchizi tu nyaya zimegusana harusini? Mtajaza wenyewe! Hivi niambie umewahi kusikia George Kichaka (Bush) anaalikwa popote toka atoke White House? Chizi hapewi kadi ya mwaliko!

    ReplyDelete
  10. Kikwete mdini sana. Udini umeanza hapa nchini katika awamu yake. Anatuchukia wakristo yeye anatamani atuweke chini lakini Mungu yuko upande wetu.

    Hata afanye nini yeye ni atabakia muisilamu tu.

    ReplyDelete
  11. Na wewe acha udini! Huyo ni yeye Kikwete binafsi na sio suala la dini? Mbona waislamu tupo wengi tu hatukubaliani na mambo yake? Mbona wakristo wapo (Kwani Lowassa Mwislamu?) na wanakubaliana na upuuzi wake? Acha udini, tumlaumu kama yeye sio uislamu wake. Hata Lowassa na Chenge hatuwalaumu kwa ukristo wao bali matendo yao machafu

    ReplyDelete
  12. Acha nao viongozi wa dini wakaripiwe kwani wao sio miungu. Ni kweli baadhi yao wanaendesha biashara chafu na sio dawa za kulevya tu bali mambo mengine. Sijasahau tulivhoibiwa na viongozi wa dini wakitumia chombo cha DECI.

    ReplyDelete
  13. Kweli shukurani ya Punda mateke. Kikombe cha babu wamekunywa sasa matusi.

    ReplyDelete
  14. Mnawakandia tu viongozi wa dini mnasahau kuwa hata viongozi wa serikali wanaweza kuwemo. jamani kauli zitolewe kulingana na mazingira manake naona tunajisahau.migogoro ya kidini huanza hivihivi.

    ReplyDelete