28 June 2011

Sitambui muafaka Arusha-Lema

Na Queen Lema na Richard Konga, Arusha

MBUNGE wa Arusha Mjini, Bw. Goodbless Lema (CHADEMA), ameibuka na kudai kutotambua muafaka wa kumaliza mgogoro wa Meya wa Jiji hilo uliofikiwa kati ya
chama chake na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Amedai Madiwani wa CHADEMA walioshiriki maamuzi ya muafaka wamekiuka sheria na taratibu za uongozi wakati wa kumchagua Naibu  Meya wa Manispaa ya Jiji la Arusha kutoka chama hicho, Bw. Estomih Mala, hivyo hamtambui.

Bw. Lema aliyasema hayo mjini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa kile alichodai kuwa yeye hamtambui Naibu Meya wa Arusha ambaye alichaguliwa June 20 mwaka huu jijini hapa katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani.

Alisema kuchaguliwa kwa Bw. Mala hakuwezi kufuta masharti ya chama hicho kutaka uchaguzi wa meya wa Arusha kufanyika upya kwa madai kuwa uongozi wa chama hicho haukuwa na taarifa juu ya uchaguzi ndani ya halmashauri hiyo.

“Naomba ifahamike kuwa mnamo Januray 5 tuliandamana kumpinga Bw. Lyimo kwa kuwa ule uchaguzi wa kumtafuta Meya haukuwa wa halali, lakini leo madiwani wa CHADEMA wanachagua na kufurahia Naibu Meya kwa misingi gani?,“Alihoji Bw. Lema.

Aliongeza alichokifanya Bw. Mala si sahihi kwa kuwa taratibu za chama zilimpasa apeleke jina Makao Makuu kwa uteuzi lakini yeye hakufanya hivyo.

“Leo tunaambiwa kuwa Naibu Meya ni Mala kutoka CHADEMA wakati Makao Makuu ya chama hawajajua, kwa hali hii mimi sipo tayari kumtambua huyu Naibu Meya na pia sipo tayari hata kushirikiana na diwani yeyote  ambaye anaangalia maslahi yake," alidai Bw. Lema.

Akizungumzia hali hiyo Meya Lyimo alisema kuwa wamefanya hitimisho na kubaini kuwa kuna umuhimu wa kila kiongozi wa jiji kuungana na kuachana na tofauti za kisiasa kwa kuwa
Jimbo la Arusha linahitaji ushirikiano ili lifanikishe lengo la kuondokana na umaskini .

“Anachokisema Bw. Lema si sahihi, endapo tutaendelea kuangalia vyeo vya vyama vyetu, basi sisi hatutafikia lengo halisi ambalo limetuweka hapa, uchaguzi tumefanya kwa mujibu wa sheria," alisema Bw. Lyimo.

Bw. Lyimo alisema kuwa wao wanajua sheria na taratibu za uchaguzi na kwamba sheria za uchaguzi zilifuatwa na halmashauri ambayo ilitangaza uchaguzi na kuitisha majina ya wagombea.

Alisema kutokana na kufuatwa kwa taratibu madiwani walipokea uchaguzi huo kwa nia njema na nafasi ya Naibu meya ikawaniwa na diwani kutoka CHADEMA kwa mujibu wa sheria na taratibu.

Alisema hatua hiyo ya kumchagua Naibu Meya haikufanywa na CCM kwa kuwa ilikuwa ni maazimio ya pande zote chini ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Bw. Raymond Mushi.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Bw. Estomih Changaa, alisema madai ya mbunge huyo ni ya kuupzwa kwa kuwa walifanya uchaguzi kwa kufuata kanuni na sheria. 

Alisema wana barua ambazo zilitoka CHADEMA na kwamba kulingana na sheria na taratibu za halmshauri ziliwaruhusu kufanya uchaguzi wa Naibu Meya. 

Hivi karibuni madiwani wa Arusha waliafikiana kugawana madaraka ili kuondoa tofauti za kisiasa zilizojitokeza wakati wa uchaguzi wa meya mwaka jana na kusababisha maandamano.

5 comments:

  1. IKIWA HUYO MBUNGE HAKUBALIANI NA UAMUZI HUO NA PIA HAO MADIWANI WA CDM WALIOBARIKI KINYUME NA MABOSI WAO BASI WAFUKUZWE UANACHAMA KWA MAANA HIYO UDIWANI NAO UTAKUWA WAZI HAWANA RIDHAA NA MABOSI WAO WA JUU WACHAGULIWE WENGINE,!!HAPA UNAONA WAZI WANANCHI WAMEONA MVUTANO HAUNA TIJA WANACHOTAKA WAO NI MAENDELEO HAO VIONGOZI WAMEKALIA UKAIDI NA KUTAKA FUJO,AKILI KICHWANI MWENU KUNYOA AU KUSUKA ACHIENI NGAZI TUFANYE UCHAGUZI UPYA WA MADIWANI

    ReplyDelete
  2. Mbunge Lema yuko pamoja na Mwenyekiti wake Mbowe kukataa muafaka, maana wanakesi haijaisha pale Arusha na chanzo ni huohuo umeya, pili haki za waliofiwa hawajalipwa tatu CDM kutokana na kesi na mvutano huo kuna fungu kubwa la kufadhili hayo haujakamilika sasa kukubali yaishe hivix2 ni kuzuia kupatikana kwa hiyo RUZUKU!!! baadhi ya watu hawako kwa maslahi zaidi kwa watu ni kwa minaajili ya kujinufaisha wao wenyewe kwa njia za kupingapinga mambo wana Arusha muwe makini.

    ReplyDelete
  3. CCM lazima wajue kwamba hawataweza kufanya uhuni wa kulazimisha matokeo halafu waje kurubuni watu mezani kwamba wawagawie baadhi ya madaraka huku wao wakiendelea kung'ang'ania vyeo ambavyo wamevipata kiufisadi. Hiki kitu kisivumiliwe kabisa Tanzania. Ama sivyo tutaruhusu CCM kuendeleza uvunjaji huu wa demokrasia na siasa za kuheshimu utaratibu na maoni wa wananchi. Viongozi wa CHADEMA wanachokisema wako sawa kabisa. Suala siyo bora liende, bali sheria na taratibu zilizowekwa zifuatwe, kitu ambacho CCM hawakitaki maana wao wamezoea kuhujumu kitu chochote kinacholeta utawala wa sheria kama kinawawekea kizuizi kufanya ufisadi wao. Haya haya ndiyo yaliyomtosa mheshimiwa Lowassa, kulazimisha tenda ya umeme kinyume cha sheria na ushauri wa wataalamu. Mpaka leo nchi iko gizani kwa ajili ya kuzunguka mibuyu na kupitisha uozo wao. Wamezoea hawa CCM, wasiruhusiwe kabisa kuendeleza tabia hii, lazima wakomeshwe.

    ReplyDelete
  4. Wajinga ndio mliwao. mtakufa kila siku kwa ujinga wenu,hicho chama cha wachaga na wachaga ndio wenye maamuzi na huyo Lema ataangamiza Arusha wapeleke maendeleo Moshi kulipo lala baada ya wawekezaji wa ndani na wa nje kupaogopa kutokana na asili ya mchaga ya wizi na ujambazi. Huyo Lymo akifa leo maiti inapelekwa kwao Moshi,na maendeleo ya mji wa Arusha wakae sawa

    ReplyDelete
  5. MADIWANI WA CHADEMA ARUSHA WAFUKUZWE KATIKA CHAMA HATUKOTAYARI KURUBUNIWA NA CHAMA CHA MAPINDUZI NI BORA TUWAKOSE HAO MADIWANI KULIKO KURUHUSU UFISADI WA WAZI KATIKA JIJI LETU LA ARUSHA.MBUNGE ANA AKILI NA ANA MUOGOPA MUNGU NDIYO MAANA ANALILIA HAKI ITENDEKE.MADIWANI KAMA HAO HAWATUFAI SISI KAMA CHADEMA LABDA WAENDE CCM

    ReplyDelete