*Atoa tuhuma nzito kwa Baraza la Mawaziri
*Spika Makinda ampa siku saba kuthibitisha
Na Grace Michael, Dodoma
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini Bw. Zitto Kabwe, (CHADEMA), ameingia katika mgogoro mwingine bungeni, baada ya kutoa tuhuma nzito dhidi ya
Baraza la Mawaziri kuwa maamuzi yake yanatokana na ushawishi wa watu wenye nia ya kuua mashirika ya umma.
Kutokana na kauli hiyo Spika wa Bunge Bi. Anne Makinda, alilazimika kumpa mbunge huyo siku saba kuanzia jana kuthibitisha kauli yake.
Bw. Zitto alitoa tuhuma hizo bungeni jana, wakati akichangia azimio la kuongeza muda wa uhai wa Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC).
Mbunge huyo alipinga azimio hilo lilitaka kuongezwa kwa muda wa miaka mitatu kwa CHC moja kwa moja kwa kutoa sababu mbalimbali.
“Jamani tulikubaliana vingine kabisa katika Kamati,leo kilicholetwa hapa ni kitu kingine. Kamati ya Fedha na Uchumi ilijadili na kutaka shirika hili lipewe muda zaidi kutokana na majukumu yaliyo mbele yake lakini hiki kilicholetwa hapa ni kitu kingine,”
“Wabunge kataeni haya maamuzi ya Baraza la Mawaziri, yametokana na kurubuniwa na watu wenye lengo la kuua CHC kwa ajili ya maslahi yao,"alisema Bw.Zitto na kuongeza
"Ikumbukwe kuwa chombo hiki kinaangalia mali za umma na mashirika lakini pia kuna kesi mbalimbali za watu ambao wanadaiwa na mashirika hivyo kwa kuja na hoja hii ni sawa na maandalizi ya wizi,” alisema.
Baada ya maneno hayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. George Mkuchika, aliomba mwongozo wa spika kutaka Bw. Zitto athibitishe kauli yake.
Katika maelezo yake kwa Spika Waziri huyo alisema kauli ya Bw. Zitto imewadhalilisha mawaziri ambao wanafanya kazi kwa maadili na kwa kuzingatia maslahi ya nchi.
Alisema kauli ya maamuzi ya Baraza la Mawaziri kutokana na kurubuniwa yanaleta picha mbaya kwa watanzania ambao wao wamewaamini watendaji hao wakuu wa serikali.
Pamoja na maombi ya Bw. Mkuchika, Spika Makinda aliingilia kati na kumtaka Bw.
Zitto ajikite kwenye hoja na kutahadharisha kuwa kinachotakiwa ni wabunge kupitisha muda huo kisha utaratibu mwingine ufuatwe kujadili suala hilo kwa kuwa amebaini kuna hoja za msingi.
“Jamani tunachotakiwa kufanya hapa ni kuipa uhai kwanza CHC na baada ya hapo tutaangalia utaratibu mwingine kwa kuwa tukianza kubishana uhai wake utakufa...ni kweli hoja mnazozitoa ni nzito na za msingi,” alisema Bi. Makinda.
Hata hivyo Bw. Zitto aliporuhusiwa kuendelea, aliendelea kusisitiza kauli yake kuwa maamuzi ya baraza hilo yanatokana na ushawishi wa watu wasio na malengo mema na mashirika pamoja na mali za umma.
“Siwezi nikafinyanga maneno hapa, nina uhakika na ninachokisema, maamuzi ya Baraza la Mawaziri ni matokeo ya malobbiest, kama serikali mnabisha leteni hapa mapendekezo ambayo yaliwasilishwa katika Kamati ya Makatibu wakuu na baraza la mawaziri...nasema tusiruhusu haya maamuzi ya mawaziri ambayo yametaliwa na mawazo ya malobbyist,” alisisitiza Bw. Zitto.
Kutokana na msimamo huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Bw. Willium Lukuvi, alisimama na kuomba mwongozo wa spika kutaka kauli hiyo ithibitishwe kwa kutajwa mawaziri waliopitiwa na kurubuniwa.
Baada ya Bw. Lukuvi kuomba mwongozo huo Bi. Makinda alimpa Bw. Zitto muda wa siku saba kuthibitisha kauli hiyo.
“Mpaka tarehe 29, mwezi huu uwe umethibitisha hayo uliyoyasema,” alisema Bi. Makinda.
Pamoja na hatua hiyo ya Bw. Zitto, mjadala huo ulionekana kuwagusa wabunge wengi wakiwemo wa Chama tawala ambao walipingana na azimio hilo.
Katika michango yao wabunge hao walipinga kipengele cha muda na pendekezo la majukumu ya CHC kupelekwa kwa Msajili wa Hazina.
Mbunge wa Mwibara Bw. Alphaxard Lugola (CCM) alisema kitendo cha kuweka muda huo ni kutoa mwanya wa maandalizi ya wizi wa mali za
mashirika ya umma ambayo yamekuwa yakitumiwa na wachache kujitajirisha.
“Mimi ni mbunge wa CCM lakini katika hili napingana kabisa, napata fursa ya kuchungulia na kuwahoji walioko kwenye mashirika ndio maana nina uchungu, fedha zinaliwa bila sababu ya msingi...hicho kipengele cha majukumu ya CHC kuwa chini ya Msajili wa hazina ambaye hata ukimuuliza ana mashirika mangapi hajui itakuwa ni kuwafikisha watanzania mahala pabaya,” alisema alisema.
Alisema utaratibu wa kuhamisha madaraka ni njia au mwanya wa wizi na kwamba imefikia wakati maamuzi yanayotolewa na bunge yasipuuzwe na serikali kwa kuwa kufanya hivyo ni kutowatendea haki watanzania.
Waziri alilazimika kuondoa kipengele cha majukumu ya CHC kuhamishiwa kwa Msajili wa Hazina na kueleza kuwa muda wa miaka
mitatu itafanya tathmini ya kiutendaji inayofanywa na CHC ili kuona namna nyingine ya kufanya.
tunakushukulu zito kabwe ao mawaziri wanaonekana wote ni mafisadi na akuna wanachoweza kuwasaidia wa tanzania ,wapo kusaidia familia zao na matumbo yao,kwa hoja iyo ata kipofu atajua upeo finyu walionao mawaziri wetu.
ReplyDeleteJamani nchi yetu haina uongozi wa kizalendo hata kidogo. Wako kujaza matumbo yao na kujilimbikia mali na utajiri bila kujali umaskini wa wengi. Wengi wa wale tuliowachaguo ambao sasa ndio viongozi ni mafisi watupu na wapatapo mwanya wanaweza hata kufilisi nchi. Wabungu hawana budi kuwa macho bila kujali itikadi ya vyama vyao. Hakuna itikadi ya wizi, ingawa Serikali ya ccm imeonyesha ubingwa katika ufisadi, rushwa na kupora mali za nchi waziwaz. Kuweni sana macho wabunge, la sivyo tutawahesabu kama mnaoshiriki kikamilifu katika kuendeleza ufisadi na wizi unaoendelea kuifanya nchi yetu kuwa fukara wa kutupwa. Ukimkingia jambazi kifua basi nawe unahesabiwa kama jambazi. Singependa kuamini wabunge wetu ni majambazi lakini mkiwa wadhaifu na kuunga mkono vitendo wa ufisadi wa viongozi wetu hatuna budi kuwachukulio nyie kama wao. Chungeni sana hilo.
ReplyDeleteserikali yetu viongozi wake wamelewa madaraka bado wanafikili wanawaongoza watanzania wa miaka ya 61, wajue kuwa elimu hii hii wanaotupatia kwenye shule zisizo na ubora za kata zinatupa upeo uo mdogo wakujua yupi amewekwa wapi na kwa maslahi ya nani,
ReplyDeleteonngera muheshimiwa zito kabwe m/mungu akupe uhai mrefu
big up mheshimiwa zitto,
ReplyDeletewao wanakaa mudamwingi wanafikilia wawarubuni vipi watanzania masikini kwa kaumbio zao zisizokuwa na tija kwa taifa,na wakati mwingine wanajidai eti wanamuenzi baba wa taifa ili,wanafanya ivo kwa kinafiki,kama kweli wanataka kumuenzi basi wamuenzi kwa vitendo, na laiti angekuwepo akuna wazili angeweza kuleta hoja kama iyo bungeni na akapata ujasili wa kusimama na kuitetea, ufisadi unakuwa kwa kasi ya kutisha tanzania imefikia hadi wsaomi na walimu tunaowategemea kwenye vyuo vyeto wanaacha kufundisha wanaingia kwenye siasa
Hongera mheshimiwa Zitto, nchi yetu imefikia pabaya sasa mpaka mawaziri kutokuwa na upeo wa kufikiri sababu ya ufisadi,hawana uzarendo. Mwalimu Nyerere alituambia kuwa ili nchi iweze kuendelea lazima iwe na vitu vitatu, watu,aridhi na uongozi bora, lakini sisi tumekosa kimoja ambacho ni uongozi bora ndiyo unatufanya tushindwe kuendelea, hihyo ni kutokana na viongozi wetu kutokuwajibika na kutokuwa wazarendo wa nchi yao, mawazo yao ni ufisadi tu.
ReplyDeleteSafi sana Chadema kwa kuwa na wabunge makini. Waziri mkuu chati yake imeshuka mno, hata sijui yuko wapi. Tunaibiwa!
ReplyDeletehongeraaa mh. zitoo hayo ndio mambo tunataka
ReplyDeleteNASHUKURU MUNGU KULA YANGU NILIPOIPIGIA CHAMA MBADALA (CHAUSHINDANI)CHADEMA SIJAPOTEZA SASA NAYAONA MATUNDA YAKE TULIIBIWA SANA LASILIMALI ZETU WATANZANIA SASA TUNASEMA KUIBIWA BASI.HONGERA CHADEMA,HONGERA ZITO KABWE JITIHADA ZENU TUNAZIONA MUNGU AWALINDE,TUNAAMINI KUWA SIKU MOJA TUTAFIKA TU.
ReplyDeleteukweli ni kwamba watu wa maisha ya chini na vijana wengi tunajivunia kuwa na kiongozi mzalendo kama zitto lakini mimi nasikitika sana waziri mkubwa na mwenye elimu aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa kama Mh:Lukuvi anaweza kuuliza swali la kulumbana na majungu badala ya kufikiria maendeleo lakini kwani hajui matatizo ya wananchi wala hajawai kutuomba kura kwa sababu alishazoea kuteuliwa.
ReplyDeleteHongera Zitto,u gat BRRRRRRRRRAINS!
ReplyDeletebig up zito
ReplyDeletetatizo la viongozi wetu hawapendi kuambiwa ukweli wanataka kuficha mambo chini ya kapeti.
ReplyDeletetime will tell,
ReplyDeletetrue hata mwana filosofia bob marley alisema " time will tell"
ReplyDeletezitto usiogope
ReplyDeleteZITTO KAZAMWENDO BABA TUKONYUMA YAKO TUNAKUPA SAPOTI NGUVU YA UMMA IPO TUNAJIPANGA CHOKOZA ALAFU WAKUZINGUE WATAJUA VIJANA NI WAKATI WETU WA MABADILIKO NA TAIFA ILI NI LA KWETU LA SASA NA LA BAADAYE TUNA MAMLAKA YAKUTENGENEZE
ReplyDelete"you can not cheat all the people all the time"ninyi watu wa ccm jueni kwamba mwisho wenu umekaribia,mmeichezea sana nchi hii na mumewaonea sana watu wa nchi hii.sasa mwisho wenu umefika tumechoshwa na falsafa zenu zilizopitwa na wakati mnatapatapa lakini haitawasaidia nadhani hata baba wa TAIFA angekuwa hai leo angekiunga mkono CHADEMA.
ReplyDeletehongera sana Zitto big up zikufikie, usiogope endelea kukaza buti, vijana tuko na nyie bega kwa bega, big up CHADEMA pamoja na uongozi wake.
ReplyDeletechadema oyee....
ReplyDelete