Na Tumaini Makene, Dodoma
KAULI ya Waziri Mkuu aliyoitoa bungeni akionekana kutetea mfumo unaoruhusu posho za vikao, imeanza kumrudi, ambapo sasa imetakiwa kuifuta kwa
madai inakwenda kinyume na Katiba ya Tanzania, kwa kupotosha majukumu ya bunge na wabunge kama yalivyoelezwa katika Ibara ya 63(2) na (3).
Msimamo huo wa Bw. Pinda unadaiwa kukiuka maelekezo ya Rais, kama inavyoelezwa katika Ibara ya 52(3).
Pia imeelezwa namna ikulu na bunge zinavyotumia fedha nyingi kwa ajili ya posho za vikao, ambapo kwa mwaka 2009/10 Ikulu ilitengewa zaidi ya sh. bilioni 148, huku bunge likijigawia sh. bilioni 36, ambapo jumla ya fedha zote za posho za vikao kwa mwaka huo zilizotengwa na serikali, zilikuwa sh. bilioni 509, ambazo zingeweza kutumika kuwalipa mishahara walimu 109,000 kwa mwaka mzima.
Wiki iliyopita katika kipindi cha kila Alhamisi cha maswali ya papo kwa papo kwa Bw. Pinda alisema kuwa suala la posho haliepukiki kwani kuna zingine zipo kwa mujibu wa katiba, hivyo haziwezi kuondolewa bila kufuata utaratibu huo, huku akiongeza kuwa baadhi zinaweza kuondolewa kwa maagizo ya katibu mkuu akiona inafaa, huku pia akiwarushia kijembe CHADEMA kuwa wapo wanaozimezea mate lakini wanashindwa kusema.
Akijibu swali la Mbunge wa Mkanyangeni, Bw. Mohamed Habib Mnyaa (CUF), Bw. Pinda alisema kuwa ukweli ni kwamba posho hizo ambazo ni stahili za wabunge na watumishi wengine wa umma, zipo kwa mjibu wa taratibu zilizowekwa kikatiba na zimegawanyika katika makundi mawili.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Katibu wa Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. John Mnyika, mbali ya kumtaka asome Ilani ya CHADEMA ya 2010, aelewe msingi wa hoja yao, alisema kuwa kauli ya Bw. Pinda ya kuhalalisha posho za vikao, inahamasisha siasa za fadhila katika taifa, ambazo alidai zimekuwa zikitumiwa na CCM kupandikiza mbegu za rushwa katika uchaguzi.
"Kauli ya Waziri Mkuu Pinda inadhihirisha hana dhamira ya dhati ya kutekeleza kwa ukamilifu na kwa haraka maagizo ya Rais Kikwete, kinyume na Katiba Ibara ya 52(3), ambayo inamtaka atekeleze au asababishe utekelezaji wa jambo lolote au mambo yoyote ambayo rais ataagiza kwamba yatekelezwe," alisema Bw. Mnyika.
Hoja ya Bw. Mnyika ilijikita katika marejeo ya Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2011/12-2015/16, ambao Rais Kikwete ameshausaini na kuuzindua, ambapo ndani yake katika ukurasa wa 17, serikali imetamka wazi kuwa posho za vikao na nyinginezo zinapaswa kufutwa au kuwianishwa.
"Katibu wa Wabunge wa CHADEMA nimeshangazwa na kauli za Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alizozitoa bungeni tarehe 16 Juni 2011 wakati akijibu maswali ya papo kwa papo...ametoa kauli ya kuhalalisha posho za wabunge kwa hoja kwamba zinahitajika kwa ajili ya kuwapa watu wanawaomba fedha nje ya ukumbi wa bunge.
Anapaswa kuifuta kauli yake hiyo, kwani inapotosha majukumu ya bunge na wabunge wake yaliyotajwa kwenye ibara ya 63(2) na (3) ya kusimamia serikali, kuwawakilisha wananchi, kupitisha mipango na kutunga sheria.
Ilani ya CHADEMA 2010 ilieleza lengo la kupunguza posho hizi kwa zaidi ya asilimia 80 zikiendana na nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma kuendana na ujuzi, nafasi, wajibu ili wafanyakazi walipwe kwa haki kwa kile wanachofanya kwa haki.
"Nilitarajia kwamba baada ya Serikali ya CCM kuchukua msimamo huo wa kuuingiza kwenye mpango wa taifa wa maendeleo wa miaka mitano uliosainiwa na Rais Kikwete Juni 7, 2011 ambao kwenye ukurasa wa 17 unatamka bayana kwamba posho za vikao na nyinginezo zinapaswa kufutwa au kuwianishwa; waziri mkuu angeipongeza CHADEMA na wabunge wake kwa msimamo wao badala ya kubeza na kupotosha.
"Ni vizuri Waziri Mkuu Pinda na watu wengine wanaotumika ndani ya serikali kutaka kuichafua CHADEMA na wabunge wake waelewe kwamba ambacho tunataka kwa umoja wetu ni kurekebishwa kwa mfumo mzima wa posho...serikali isifanye mkakati wa kupenyeza habari ya kuupotosha umma kwa kutumia orodha na saini za wabunge za mahudhurio ya vikao sanjari na habari ya kupindisha kutaka kuonesha kuwa wabunge wa CHADEMA hawana dhamira ya dhati kuondoa posho za vikao.
"Kifungu cha 19 (d)(iv) kimempatia mamlaka rais ya kutoa posho zingine kwa wabunge kwa kadiri atakavyoelekeza; kifungu hicho kimefanya utolewe waraka wa Katibu Mkuu Kiongozi Ofisi ya Rais wa Oktoba 25, 2010...ambao umeeleza viwango vya posho, mbalimbali ikiwemo posho ya vikao.
Hivyo kwa kuwa Rais Kikwete amesaini Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano Juni 7, 2011 wenye kulenga kuondoa posho hizo rais, anapaswa kufuta posho hizo.
"Asisubiri mabadiliko ya kisheria au kikatiba kama Pinda alivyoeleza bungeni," alisema.
Aidha hatua hiyo iende sambamba Rais Kikwete kuonesha mfano kwa kupunguza gharama za posho mbalimbali za vikao na safari za nje ambazo zinatumiwa na ikulu," alisema kwa kirefu Bw. Mnyika.
KATIKA KATIBA MPYA SWALA HILI LA RAIS NA POSHO INABIDI LIANGALIWE UPYA KUNA HAJA KUBWA YA KUMTENGANISHA RAIS NA MASUALA AU UWEZO WA KUGAWA PESA KWA WABUNGE KWANI NI HATARI SANA KWA DEMOKRASIA YETU. MASUALA YANAYOHUSU MATUMIZI YA KODI ZA WANANCHI YAWEKWE MIKONONI MWA WABUNGE TU NA SIYO MWINGINE YEYOTE.
ReplyDeleteHii inaonyesha jinsi hata spika hajui alitendalo. Nilitarajia angekuwa ameanzisha uchunguzi wa nani ame'photocopy' daftari la mahudhurio ya bunge na kuwapa waandishi wa habari. Kwani kitendo hicho kinakiuka sheria ya maadili ya utunzaji wa taarifa za wabunge pasipo umuhimu wa kuikwa hadharani au ruhusa ya bunge. Lakini pia kwa watu waliomakini wataona kwamba hizo sahihi za wabunge zilikuwa chini ya kichwa cha habari Mahudhurio ya wabunge kwa hiyo kusaini kwao sio tatizo ni kukidhi matakwa ya 'monitoring attendance' tu. Hiyo register ingeonyesha kuwa ya posho hapo ingeleta sense, lakini majina na sahihi zinaweza kutumiwa kwa matumizi mengi ikiwemo kuangalia ushiriki wao au mahudhurio yao bungeni, kuandaa malipo ya posho etc. Pia nilisoma propaganda za Nauye nadhani anashindwa kuelewa kuwa CHADEMA walitoa ilani na mipango yao ya kutoa elimu bure n.k iwapo wangeingia madarakani, sasa leo hawajaingia madarakani na hawana nafasi ya kudhibiti ufisadi na hela za umma zinazopotea kwa rushwa, kudhibiti mapato ya madini, utalii, uvuvi n.k watatoaje elimu na huduma za afya bure. Kama seriakli ya ccm ina nia njema kwa nini basi wabunge wasifute posho zao ili hawa wanafunzi wanaolalamikia hela ndogo ya kujikimu wakalipwa, au hizo posho za wabunge zikawalipa hawa wanafunzi wanaohitaji kwenda kufanya mazoezi ya vitendo badala ya kupigwa marungu na polisi na kukebehiwa kana kwamba hawafai na hawatakuwa na mchango wowote serikalini. Hii ingeonyesha seriakli na bunge wanajali raslimali watu za sasa na baadaye, kwani humo humo watakuwemo wabunge na mawaziri wa baadaye.
ReplyDeletebana ee hiyo posho ifutwe tu kwasababu ni dharau kubwa kwa mfanyakazi wa kima cha chini afu mbona hiyo ni kazi yake mbunge na ni kama ofisi yake?
ReplyDeleteKIONA MBALI; NAPE NI MBUMBU WA KUFIKIRI KAMA ALIVYOPATA ZIRO (YAI) MWENGE SEKONDARI SINGIDA; CHADEMA hawajaingia madarakani na hawana nafasi ya kudhibiti ufisadi na hela za umma zinazopotea kwa rushwa, kudhibiti mapato ya madini, utalii, uvuvi n.k watatoaje elimu na huduma za afya bure BILA KUPATA MTAJI ULIOFICHWA KWA UFISADI WA CCM?.
ReplyDeleteHii sasa ni danganya toto! Kwamba posho ya vikao ya wabunge ni la Katiba, na hivyo haziwezi kufutwa au kubadilishwa bila kwaza kubadilisha Katiba ya nchi ni uwongo mkubwa na ni udhalilishaji wa Katiba ya nchi yetu! Kwanza zimeanza tu katika enzi ya Samuel Sitta.
ReplyDeletePinda hishima yako kwa jamii inazidi kushuka kila kukicha. Umefikia hatua ya kutuita watanzania wenzako ombaomba pale bungeni huku wakati ukiomba kura ukituita mjina yaliyitukuka kama vile waheshimiwa watanzania, ndugu zangu, n.k. Leo kulikutuma kutuletea maendeleo si kutupa mia tano tano nje ya bunge kama unanyotudhalilisha. Poa 2015 siyo mbali utatukuta wananchi wako kuomba kura tena. ENDELEA NA FADHILA ZAKO ZA PUNDA.
ReplyDeletewanaotetea posho si watanzania wenzetu kimtazamo. hawa watakuwa ni wale wanaonufaika na posho hizo kwa njia moja ama nyingine. yawezekana wakawa machangu doa au ndugu ama jamaa wa wabunge na mawazili. mtanzania mwenzetu anayepigika na maisha huku mtaani bila kujua hatima yake kesho hawezi hata kidogo kutetea hilo. ni bora kabisa hizo pesa zikatumike kuboresha hata hospitali aambako mama zetu wanajifungulia chini kwani hata vitanda hamna. au wakapewa walimu wetu ambao maisha yao na hahdi ya kazi yao havina uhusiano kabisa.
ReplyDeleteThe government of Tanzania is a government of the people by the people and for the people! Hao wabunge wanaosema serikali ya Tanzania ni ya CCM wanamaana kuwa CCM imeshawanyang'anya Watanzania (the people) serikali yao na kwamba sasa tunatawaliwa na CCM na tunatakiwa kudai uhuru! Hivi mtu ukimchagua kusimamia shirika lako (la umma) ndiyo limekuwa lake? Hao ni mbumbumbu tu wanatakiwa waelimishwe somo la uraia angalao kidogo kwa semina bila posho. Infact wanatakiwa kulipa gharama za semina siyo kulipwa.
ReplyDelete