06 June 2011

Binti mbaroni kwa 'kubaka kavulana'

Na Masau Bwire

MSICHANA mwenye umri wa miaka 16 (jina linahifadhiwa), mkazi wa Kigogo, Luhanga, Dar es Salaam anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za 'kumbaka' mtoto wa
kiume mwenye umri wa miaka mitatu.

Msichana huyo anadaiwa kumbaka mtoto huyo mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo alimuiba nyumbani kwao na kumpeleka kwenye pagale, nyuma ya Shule ya Msingi Kawawa.

Mama mzazi wa mtoto aliyefanyiwa unyama huo, ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema, wakati akifanya usafi ndani ya nyumba yake siku ya tukio saa 4 asubuhi, mtoto wake alikuwa nje akicheza na wenzake.

Alisema alipomaliza ndani alitoka nje kumchukua mwanaye huyo ili ampe kifungua kinywa, lakini hakumwona ndipo, akaanza kumtafuta zaidi ya saa nzima bila mafanikio.

Mama huyo alisema, baada ya kuhangaika kumtafuta mwanaye, akili ilimtuma kuchungulia ndani ya nyumba hiyo inayojengwa na alipofanya hivyo alikuta mwanaye amelaliwa na msichana huyo.

Alisema kuona hivyo alikwenda mbio kuita mama mwingine jirani yake ili ashuhudie kitendo anachofanyiwa mwanaye.

"Nikiwa na jirani yangu tulishuhudia msichana huyo akifanya kitendo hicho kwa mtoto wangu," alisema.

Baada ya kushuhudia yote hayo, walipiga kelele na kumkamata akiwa uchi na kumpeleka Kituo Kidogo cha Polisi Kigogo- Luhanga.

Msichana huyo alishikiliwa kwa muda katika kituo hicho kidogo cha polisi kisha akahamishiwa Kituo cha Urafiki kwa hatua zaidi za kisheria ambapo mtoto aliyebakwa akilipelekwa katika Hospitali ya Amana kupatiwa matibabu.

15 comments:

  1. msichana huyu anatakiwa kupewa adhabu kubwa ili iwe fundisho kwa wenzake.

    ReplyDelete
  2. Na kidume kimyaaa! kimenyamaza kwa kula raha! Wafundishwe watoto kupiga kelele

    ReplyDelete
  3. Huyo binti apelekwe kuchekiwa akili, kwani hakuwaona wanaume wote hao mpaka hako katoto.

    ReplyDelete
  4. Naona huyo binti katoroka milembe hana akili nzuri ni kichaa au ndo mambo ya imani za kishirikina?

    ReplyDelete
  5. wampelekae muhimbili kwani wanaume wengi tu hawana wanawake

    ReplyDelete
  6. duuuh! amakweli dunia imeisha....

    ReplyDelete
  7. HILO NI PEPO AOMBEWE. LAANA TUPU.

    ReplyDelete
  8. she might have health problems. mmmmmmmh!!!!it's so bad but sometimes so funny.

    ReplyDelete
  9. INAONESHA KUWA HIYO NI AIBU KUBWA SANA NA SASA INAPELEKEA KUTOAMINIANA KWA WATU....MTOTO ANA RAHA GANI?
    KAMA UNATAKA YAANI UNA HAMU TAFUTA SAIZ YAKO USIWAHARIBIE WENZAKO MAISHA

    ReplyDelete
  10. Muhimbili haitoshi,apelekwe segerea au keko tena wafanye kimakosa aingizwe upande wa wanaume akae wiki tu akili zake zitakaa sawa.Huyo ni chizi maarifa akili zake hazina akili

    ReplyDelete
  11. baba na mama mkumbuke kuwasha redio ili kudhibiti kamlalamo ka raha kasipitilize nje ya nyumba na kuwakuna watoto...

    wazazi tujitahidi pia kumantain privacy ya hali ya juu tunapokuwa kwenye maongezi yetu...

    pia hizi sinema za siku hizi....mie nshazipiga marufuku kwangu.....

    ReplyDelete
  12. Kiutaalamu Mwanamke hawezi kubaka, maana ili kubaka ni lazima kuwepo na Kuingilia kwa nguvu au pasipo ridhaa, na kwa sababu mwanamke hana uume, hivyo hawezi kuingilia isipokuwa ataingiliwa.. Hivyo basi hii kesi si ya kubaka ila ni ya kudhalilisha kijinsia kwa mtoto ( minor)Waandishi wawe makini na maneno wanayotumia, vizuri mkauliza wataalamu kabla ya kuandika, msije mkapotosha umma bure.

    ReplyDelete
  13. tunatakatukaone hakokasichana kenyekinyegemshind tuonesheni pichayake

    ReplyDelete
  14. dah! this is to much...hako kasichana..ni mapepe..tu atafute wakubwa wenzake..aisome number..nyege zote..zitaisha..achapwe viboko kwa mwez mmoja akitoka..uko..jela..adabu..ita..mkaa..ipasavyo...

    ReplyDelete
  15. KITENDO CHA KUTOTAJA JINA LA MBAKAJI SI SAHIHI,MBONA WAKIWA WANAUME WAMEBAKA HUTAJWA TU BILA KUFICHA JINA ???????????????

    ReplyDelete