BARCELONA, Hispania
KLABU ya Barcelona ipo kwenye mazungumzo na Arsenal kwa wiki kadhaa, ili kutafuta njia ya kumrejesha kwenye kikosi chake mchezaji Cesc Fabregas.Gazeti la
El Mundo Deportivo, lilivinukuu vyanzo vya habari vikieleza kuwa majadiliano hayo yameshachukua mwezi mmoja hadi sasa, huku vikisema huenda klabu hizo zinajadiliana kuhusu bei iliyotangazwa na Arsenal, ili iweze kumwachia mchezaji huyo.
Tayari Gunners imshasisitiza kuwa inahitaji euro milioni 55, ili imwachie kiongo huyo baada ya mwaka jana kukataa euro milioni 40 kutoka kwa Barcelona.
Gazeti hilo lilieleza kuwa hata hivyo Barcelona, ina matumaini ya kufika bei kwa kumwongeza kinda wake, Thiago Alcantara katika ofa waliyotoa.
Lilieleza kuwa timu hiyo ipo tayari kutoa euro milioni 35 taslimu, pamoja na kufanya mabadilishano baina ya Thiago na Cesc.
Kocha wa Gunners, Arsene Wenger ni shabiki mkubwa wa Thiago na Barcelona ina matumani kuwa kwa kumwongeza mchezaji huyo chipukizi inaweza kuongeza uzito katika mawindo hayo.
No comments:
Post a Comment