*Mbunge asema ni kubwa mno, linalodidimiza uchumi
*Alinganaisha Marekani yenye mawaziri 15, Japan 17
*Wazanzibari walia na muungano, wasisitiza uvunjwe
Na Grace Michael,Dodoma
MBUNGE wa Viti Maalum, Bi. Suzan Lyimo (CHADEMA) amekataa kuunga mkono hoja ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuwa haijazingatia
kupunguza matumizi hususan kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri, serikali kutokuwa na nia ya dhati ya kuhamia Dodoma pamoja na kushindwa kutoa maamuzi.
Mbali na suala hilo, baadhi ya wabunge waliochangia hotuba hiyo hasa wabunge kutoka Zanzibar waliomba kuvunjwa kwa muungano kwa kuwa umeshindwa kuzingatia maslahi ya pande zote mbili ambapo alitolea mfano katika uteuzi wa mabalozi
katika nchi mbalimbali.
Hayo yote yaliibuka bungeni jana wakati wa majadiliano ya hotuba ya bajeti ya Waziri Mkuu ya mwaka 2011/2012.
Akichangia hoja hiyo, Bi. Lyimo alisema kuwa pamoja na matatizo yanayoikabili nchi hii, lakini serikali imeshindwa kuangalia namna ya kupunguza hata ukubwa wa
baraza la mawaziri ambalo alisema linatumia fedha nyingi ambazo zingeweza kwenda katika shughuli zingine.
“Nasema siungi mkono hoja hii kwa sababu hizo tatu, moja ya kushindwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri, serikali kushindwa kutekeleza azma ya kuhamia Dodoma lakini pia kushindwa kutoa maamuzi hasa katika masuala ya kushughulikia matatizo ya wanafunzi,” alisema Bi. Lyimo.
Alisema kuwa ni ajabu kwa Tanzania kuwa na mawaziri 52 huku nchi kama Marekani ikiwa na mawaziri 15, Japan ikiwa na mawaziri 17 na Ujerumani ikiwa na mawaziri 15 nchi ambazo kiuchumi zinafanya vizuri sana.
“Fedha nyingi zinatumika kuhudumia ukubwa wa baraza hili la mawaziri hivyo suala hili ni vyema sasa likaangaliwa kwa umakini ili kwenda sambamba na wenzetu ambao pamoja na kuwa na uchumi mzuri mabaraza yao ni madogo,” alisema Bi. Lyimo.
Akizungumzia suala la serikali kutokuwa na nia ya dhati ya kuhamia Dodoma, alisema kuwa kama imeshindwa kufanya hivyo ni vyema ikawa wazi kuliko kila mwaka kuomba fedha za kuendeleza Ofisi Dodoma na Dar es Salaam.
Alisema kuwa anayo mifano ya nchi mbalimbali ambazo zimefanikiwa kuhamisha makao yake makuu, akitaja Nigeria na Malawi, hivyo akasisitiza kuwa kama nia ya dhati haipo serikali iwe wazi.
Bi. Lyimo alikwenda mbali zaidi kwa kumtaka Rais Jakaya Kikwete ndiye aanze kuhamia Dodoma kwa kuwa akifanya hivyo mawaziri nao watalazimika kumfuata.
“Wapo waliopendekeza kuwa spika ndiye aanze kuhamia hapa...mimi nadhani rais ndo anayepaswa kuanza kuhamia hapa,” alisema.
Bi. Lyimo pia alizungumzia suala la migomo ya wanafunzi ambapo alisema kuwa limeghubikwa na upotoshaji mkubwa kuwa vyama au viongozi wa upinzani ndio wanachochea hali hiyo.
Alisema kuwa migomo ya wanafunzi ilianza tangu mwaka 1965, 1966 ambapo wanafunzi walikuwa wakiandamana na katika kipindi hicho wapinzani hawakuwepo.
Kutokana na hali hiyo, alisema kuwa suala la upinzani kuchangia katika migomo ya wanafunzi si la kweli na akaeleza kuwa litamalizika endapo serikali itatimiza
wajibu wake.
Alitumia fursa hiyo pia kuelezea maandamano yanayofanywa na chama chake, ambapo alisema kuwa wataendelea kuandama hadi kieleweke kwa kuwa tayari wameishika pabaya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kwa upande wa wabunge wa Zanzibar waliozungumzia suala la muungano, walisema kuwa ni vyema muungano ukavunjwa kwa kuwa umejaa upendeleo kwa Tanzania Bara.
Mbunge wa Jimbo la Micheweni, Bw. Haji Khatibu Kai (CUF) alipendekeza kuwa kuvunjwa kwa muungano kwa kuwa hakuna uwiano katika mambo mbalimbali yanayofanywa na serikali.
Alisema kuwa serikali haikueleza ni kero ngapi mpaka sasa zimeshughulikiwa hatua inayowafanya Wanzanzibari kuwa nyuma ikilinganishwa na wabara, hivyo akaomba kuwa kama Zanzibar imeonekana ni mzigo, basi muungano huo uvunjwe ili uundwe upya.
Naye Mbunge wa Magogoni, Bw. Kombo Khamis Kombo (CUF) alisema kuwa kumekuwa na uwiano usiokuwa sahihi katika mambo mbalimbali ambapo alitolea mfano uteuzi wa mabalozi katika nchi mbalimbali.
Alisema kuwa mpaka sasa mabalozi wanaotoka Zanzibar ni wanne tu ambao wako katika nchi za Kiarabu huku idadi kubwa ya mabalozi wakitoka bara hivyo akaomba kuwepo uwiano katika teuzi mbalimbali.
Alisema kuwa serikali ina wizara 26, kati ya hizo sita tu ndizo za muungano, lakini mambo mbalimbali ambayo si ya muungano yamekuwa yakitengewa fedha hivyo akahoji usawa katika masuala hayo.
Alisema kuwa kama kuna nia ya dhati ya kutatua kero za muungano ni vyema Waziri Mkuu akalisimamia vyema suala hilo ili kurejesha imani ya Wazanzibari.
Mjadala wa hotuba hiyo utamalizika Ijumaa baada ya kuongezwa siku mbili kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wabunge wanaotaka kuchangia hotuba hiyo.
JAMANI WAZANZIBARI ANGALIENI UKUBWA WA ENEO. NYIE ENEO LENU NI DOGO. TZ BARA HAMUONI ENEO LA MRABA NI KUBWA? AU MNATAKA UWIANO WA AINA GANI? KWA SABABU KAMA TZ BARA MABALOZI WAKIWA 20 NA ZBAR MNATAKA 20? SIDHANI KAMA ITAKUWA HAKI. CHA MSINGI MUANGALIE UWIANO KULINGANA NA UKUBWA WA ENEO NDIO ITAKUWA FEAR.
ReplyDeleteDawa ya Muungano ni kuvunja na tuwe na nchi moja yenye serikali moja na Rais au viongozi wa wizara zote wahamie Dodoma mara moja.
ReplyDeleteTatizo ni kuwaachia Zanzibar kuwa na WABUNGE wengi MFANO Mbunge mmoja wa Zanzibar anachaguliwa na watu ELFU TANo(5000)sasa wanataka ubalozi tumewaachia sana hao.
ReplyDeleteTuanze kwanza kuwapunguza hao wabunge wanachezea hela za walipa kodi.
MUHIMU ni kuvunja MUUNGANO ILI KILA NCHI IJITEGEMEE MAANA WAO SISI TUNAWANYONYA
TUACHENI NA NCHI YETU ZANZIBAR TUONE KAMA TUTASHINDWA KUISHI. NYIE VIPI?
ReplyDeletezanziba ingekuwa mbali kama sikungana na wadanganyika kazi porojo tuuuu hata hilo bunge lao ukiangalia pumba tupu ndo mana nchi ina kila aina ya utajiri eti masikini kazi wizi na ufisadi hivi karibuni wanasherehekea miaka 50 ya ujinga na umasikini wazanzibari tumechoka tuachieni muone kama tutakufa njaa mnatulazimisha hatuutaki muungano c unatosha muungano wenu wa mikoa kuendeleza ujinga na umasikini tanganyika RIP
ReplyDeleteFAIDA ZA MUUNGANO KWA ZNZ MIAKA 46
Ujinga
Umasikini
Ufisadi
Ujambazi
Ukahaba
Ulevi na Vilevi
Tunaipongeza Tanganyika kwa faida za muungano huuuuuuuuuuuuuuuuuuuu Rip
Watanganyika mnajidanganya sana "Eti Zanzibar ndogo kwa hivyo hatuwezi kugawa kila kitu sawaswa" Sisi tulipoungana tulikuwa ni nchi na wala hatuangalii ukubwa au udog, sasa kama Zanzibar ni mzigo tuachieni wenyewe muone kama tutashindwa au vipi. Pumbavu sana nyinyi Watanganyika, haya kwenu na umalaya wenu !!
ReplyDeleteNyie wazanzibari acheni u ju ha! Mlo wenyewe mmoja tena boflo halafu mnajiita nchi! Nyie mkoa! Hasa hasa mnastahili kuwa wilaya! Mkija Dar kuhemea mnatanua kama mmefika London! Na hatuuvunji ng'o mpaka tuwakamue ngama! Shwaini nyie!
ReplyDeleteZanzibar mna rais, makamu wawili, waziri kiongozi, baraza la mawaziri, wawakilishi - bado mnasema tuachieni nchi...kama viongozi wote hao mnao, mnashindwaje kuwa na maendeleo eti mpaka muachane na bara? ujinga. Nyerere alishasema mkijitenga leo, kesho Unguja itakuwa nchi, na Pemba itakuwa nchi.
ReplyDeleteWanzanzibari waende kwao kama nchi watuachie nchi yetu. Wanafaidika mno hata Urais wanapewa watutawale. Nafasi za Ubunge , mawaziri, mabalozi, makatibu wakuu. waacheni jamani wanzabari wawe nchi hatuwahitaji.
ReplyDeleteNa huyu anayesema baraza la mawaziri la USA ni dogo mwambie aangalie kila wizara pale |Marekani ina mawaziri wadogo wangapi asiwe tu anasema kwa vile anajisikia kusema na kutufanya wajinga. Wizara ya mambo ya nje ya marekani pekee ina mawaziri wadogo 6 haya na zingine. Wacha kusema usichokuwa na hakika. Mh mbunge tunasema NO DATA NO TALK